





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: “Hakika mtafuata njia za walio kuwa kabla yenu, hatua kwa hatua, na dhiraa kwa dhiraa, hata wakiingia kwenye pango la mburukenge, mtawafuata.” Tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unakusudia Mayahudi na Wakristo? Akasema: “Kwa hiyo ni nani?”
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, jinsi hali ya baadhi ya watu wa Umma wake watakavyokuwa baada ya zama zake, ambako ni kufuata njia ya Mayahudi na Wakristo katika imani, matendo, desturi na mila zao, kufuata kwa undani sana, inchi kwa inchi, na dhiraa kwa dhiraa, hata wakiingia katika tundu la mburukenge, nao wataingia nyuma yao.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao, na atakayelingania katika upotofu atakuwa kwake na madhambi mfano wa madhambi ya yule aliyemfuata, halipunguzi hilo katika madhambi yao chochote".
Imepokelewa Imamu MuslimAmebainisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayewaelekeza na kuwajulisha na kuwahamasisha watu katika njia ya haki na kheri kwa kauli au kitendo, basi atakuwa na malipo mfano wa malipo atakayoyapata aliyemfuata katika hilo, na hilo halitopunguza katika malipo ya mfanyaji chochote. Na atakaye waelekeza watu na kuwaonyesha njia ya batili na shari ambayo ina dhambi ndani yake na makosa au jambo lisilo la halali, kwa kauli au kitendo, basi atakuwa na madhambi mfano wa madhambi ya yule atakayemfuata, pasina ya kupunguza hilo katika madhambi yao chochote.
Kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- yakwamba yeye alimuona mtu alishituka aliposikia mazungumzo kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika sifa (za Allah) -akafanya kama ishara ya kulipinga hilo- akasema: "Ni nini kinachowaogopesha hawa? wanapatwa na ulaini (wanazikubali) aya zilizo wazi, na wanaangamia katika aya zinazotatiza".
Imepokelewa naIbn Abii A'swim - Imepokelewa na Abdul RazaaqAnawakemea bin Abbasi watu miongoni mwa wale waliohudhuria kikao chake katika watu wa kawaida wanaopatwa na hofu pale wanaposikia chochote katika hadithi za Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu sifa, na wanatikisika kama ishara ya kulipinga hilo, haijapatikana kwao imani ya wajibu kwa yale yaliyothibiti toka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na wakajua maana yake kutoka ndani ya Qur'ani ambayo muumini hawezi kuwa na shaka, na baadhi yao huzichukulia katika maana isiyokuwa yake aliyoitaka Mwenyezi Mungu wakaangamia kwa hilo.
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, alisema hivyo mara tatu", Na hakuna yeyote miongoni mwetu isipokuwa ana chembe ya hilo, isipokuwa Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadAmetahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokana na imani ya mikosi: Nayo ni kuamini mikosi ya chochote chenye kusikika au chenye kuonekana, kama ndege au wanyama au walemavu au namba au siku au kinginecho, Na bila shaka ametaja ndege kwa sababu ndio ilikuwa maarufu kipindi cha zama za ujinga, na asili yake ni kumuachia ndege aruke katika jambo kama safari au biashara au kinginecho, akiruka pande wa kulia anajipa bishara na anatekeleza anachotaka kukifanya, na akirukia upande wa kushoto, anaamini ni mkosi na anaacha kufanya alichotaka kukifanya. Na akaeleza kuwa kitendo hicho ni ushirikina, na mikosi imekuwa ni ushirikina kwa sababu hakuna aletaye kheri ila Mwenyezi Mungu, na wala hazuii shari ila Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika. Na ametaja bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake kuwa inaweza kuingia katika moyo wa muislamu kiasi kidogo cha imani ya mkosi, lakini anatakiwa akizuie kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, ikiwa ni pamoja na kufanya sababu.
Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Shikhiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisafiri katika msafara wa Bani Aamir kwenda kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Tukasema: Wewe ni bwana yetu, akasema: "Bwana ni Mwenyezi Mungu", Tukasema: Na mbora zaidi kuliko sisi katika fadhila, na mtoaji zaidi kuliko sisi, akasema: "Semeni kwa maneno mliyozoea, au baadhi yake, na wala asikukokoteni Shetani".
Imepokelewa na Abu Daud na AhmadLilikuja kundi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, walipofika kwake wakasema -kwa kumsifu- kwa baadhi ya maneno ambayo aliyachukia -Rehema na amani ziwe juu yake-, Wakasema: "Wewe ni bwana yetu", Akasema kuwaambia -Rehema na amani ziwe juu yake- "Bwana ni Mwenyezi Mungu" Yeye ndiye mwenye ubwana uliokamilika juu ya viumbe wake nao ni waja wake. Na wakasema: "Wewe ndiye mbora wetu" na mwenye daraja na utukufu wa juu kuliko sisi na mwenye sifa nyingi. Na wewe "Ndiye mtoaji zaidi kuliko sisi" na mwingi wa ukarimu na utukufu na daraja ya juu. Kisha akawaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake waseme kauli yao iliyozoeleka na wasijilazimishe kutafuta maneno mengine, na kuwa shetani asiwavute katika kuchupa mipaka na kupitiliza kunakopelekea kuingia katika yale yaliyoharamishwa miongoni mwa shirki na njia zake.
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: Alieleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "kwamba yeye atakuja asujudu kwa Mola wake na amtukuze [hatoanza na kuomba utetezi kwanza], kisha ataambiwa: "Nyanyua kichwa chako na sema yasikilizwe, na omba upewe, na taka utetezi utetewe".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAtakuja Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- siku ya kiyama atasujudu kwaajili ya Mwenyezi Mungu, na aombe, kisha amuidhinishe Mwenyezi Mungu katika utetezi mkubwa, na aseme Mola wake kumwambia: Omba upewe, na taka utetezi utetewe, Yaani ombi lako ni lenye kukubalika na utetezi wako ni wenye kukubalika.
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake asubuhi ya tukio la Akaba huku akiwa juu ya Ngamia wake: "Niokotee kijiwe" Nikamuokotea vijiwe saba, navyo ni vijiwe vya kurusha wakati wa kuwinda, akawa akivipuliza katika kiganja chake huku akisema: "Mfano wa vijiwe hivi basi rusheni" Kisha akasema: "Enyi watu, tahadharini sana na kuchupa mipaka katika dini, kwani kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni kuchupa mpaka katika dini".
Imepokelewa na Ibn Majah, Nasai na AhmadAnaeleza bin Abbasi radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake yakuwa alikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya kuchinja (Siku ya Idd kubwa) asubuhi ya kurusha vijiwe (kwa walioko Makka katika ibada ya Hija) katika Hija ya kuaga, Akamuamrisha amuokotee vijiwe vya kurusha, akamuokotea vijiwe saba, kimoja miongoni mwake kina saizi ya kijiwe cha kuwindia, akaviweka Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mkononi mwake kisha akavitikisa, na akasema: Kwa vijiwe vya mfano kama huu basi rusheni, Kisha akatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokuchupa mipaka na kujilazimisha na kuvuka kiasi katika mambo ya dini, kwani kilichowaangamiza umma waliotangulia ni kuvuka mipaka na kujiwekea mkazo katika dini.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuna kuambukizana, wala mikosi ya ndege, wala mkosi wa Bundi, wala mkosi wa Kipanga (Jamii ya ndege). Na mkimbie mwenye ukoma kama unavyomkimbia simba."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume rehema na amani ziwe juu yake alieleza baadhi ya mambo ya zama za kabla ya Uislamu, kuwa kama ni onyo dhidi yao, na kwa kuwabainishia kuwa amri yote iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna kinachotokea isipokuwa kwa amri yake, na kadari zake, nayo ni: La kwanza: Watu wa zama za kabla ya Uislamu waliamini kwamba ugonjwa huwa unaambukiza peke yake. Kwa hiyo, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akakataza kuamini kwamba ugonjwa huwa una asili ya kuambukiza kutoka kwa mgonjwa kwenda mgonjwa mwingine. Mwenyezi Mungu ndiye mwenye mamlaka ya kuundesha ulimwengu; Na Yeye ndiye anayeteremsha maradhi na kuyaondoa, na halitokei hilo ila kwa kutaka kwake na kwa Kadari Yake. La Pili: Watu wa zama za kabla ya Uislamu walikuwa wakitoka kwa ajili ya safari au biashara walikuwa wanawafukuza ndege, wakiruka kwenda kulia wanafurahi, na wakiruka kushoto wanakata tamaa na kurudi (wakiamini kuwa ni mkosi) basi, Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akakataza hali hii ya kuamini mikosi kwa sababu ya ndege, na akabainisha kuwa ni imani potofu. Tatu: Watu wa zama za kabla ya Uislamu walikuwa wakisema: Ndege bundi akitua juu ya nyumba, kuna msiba utawapata watu wa nyumba hiyo. Kwa hivyo, akakataza rehema na amani ziwe juu yake, kuamini mikosi katika hilo. Nne: Ni haramu kuamini mwezi wa Swafari kuwa ni mikosi, ambao ni mwezi wa pili katika miezi ya mwandamo. Ilisemekana kuwa Swafari ni: Nyoka tumboni anayeambukiza mifugo na watu, wanadai kuwa anaambukiza zaidi ya upele; akakanusha imani hii. Tano: Aliamrisha kujitenga mbali na mwenye ugonjwa wa ukoma kama vile mtu anavyojiweka mbali na simba. Hii ni kujikinga na kutafuta usalama kwa ajili yake na kufanya sababu alizoamrisha Mwenyezi Mungu, na ukoma ni maradhi ambayo viungo vya mtu hulika.
Na imepokelewa kutoka kwa Hassan yakwamba yeye amesema: "Hauondoi uchawi ila mchawi".
Imepokelewa na Ibn Abii Shaybah - Imepokelewa na AlkhatwabyNushra, ni kuondoa uchawi, na uwazi wa maneno ya Hassan ni kuzuia hilo moja kwa moja; kwasababu hakuna anayeweza kuuondoa uchawi isipokuwa mwenye maarifa ya uchawi, na hii inachukuliwa katika kuondoa uchawi kwa uchawi mfano wake, ambayo ni katika kazi za shetani, na aliweka wazi bin Qayyim kwa kusema: Nikuwa, kumtibu aliyerogwa kwa madawa ya halali na kusoma qur'ani ni jambo linalofaa, na kumtibu aliyerogwa kwa uchawi ni haramu.