





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abdillah bin Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: "Si chochote mbingu saba na ardhi saba katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa rehema- isipokuwa ni kama punje ya ulezi katika mkono wa mmoja wenu".
Imepokelewa na Ibnu Jariri - Imepokelewa na Adh-dhahaby katika kitabu cha Uluwwi - Imepokelewa na Abdallah bin Al-Imam AhmadAnatueleza Abdillahi bin Abbasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- katika nukuu hii kuwa kiwango cha asilimia ya mbingu saba na ardhi saba pamoja na ukubwa wake katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa Rehema-, ni kama kiwango cha punje ndogo ya ulezi katika kiganja cha mmoja wetu, na hii ni kufananisha kiwango kwa kiwango, na si kufananisha kiganja kwa kiganja; kwasababu Mwenyezi Mungu sifa zake hazifanani na kitu chochote kama ambavyo dhati yake haifanani na chochote.
Kutoka kwa Abuu Dharri Al-Ghifaariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Si chochote kursiy (Mahala anapoweka miguu Ar-Rahmani) katika Arshi isipokuwa ni kama bangili la chuma lililowekwa katika ardhi ya jangwa pana".
Imepokelewa na Abii Shayba katika kitabuchake Al Arshi - Imepokelewa na Adh-dhahaby katika kitabu cha UluwwiAnaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi ya Abuu dharri kuwa kursiy pamoja na upana wake na ukubwa wake ukilinganisha na Arshi ni kama bangili la chuma lililowekwa katika jangwa la ardhi pana; Na hii inaonyesha ukubwa na utukufu wa muumbaji wake na uwezo wake uliotimia.
Kutoka kwa Anasi Bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza zaidi ni kujipa matumaini". Wakasema: Ni nini matumaini? Akasema: "Ni neno jema".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kuambukizana ambako walikuwa wakiamini watu wa zama za ujinga kuwa maradhi yanahama yenyewe kwenda kwa mwingine pasina kadari ya Mwenyezi Mungu, nikuwa madai hayo ni batili, nakuwa mikosi ya ndege ni batili, nayo ni mikosi kupitia kitu chochote chenye kuhisika au kuonekana, kama ndege au wanyama, au walemavu, au namba au siku au kinginecho, hapa ametaja ndege kwa sababu ni kitendo kilichokuwa maarufu zama za ujinga, na asili yake ilikuwa ni kumuachia ndege wakati wa kuanza kazi yoyote, kama safari au biashara au kinginecho, akiruka kuelekea kushoto mtu anaamini ni mkosi, na anaahirisha alichotaka kukifanya. Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa anafurahishwa sana na mtu kujipa matumaini, nayo ni mtu kuwa na furaha na raha, kwa maneno mazuri anayoyasikia, yatakayomfanya awe na dhana nzuri na Mola wake Mlezi.
Imepokelewa kutoka kwa Baraa -Radhi za Allah ziwe juu yake: Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake Alisema kuhusu maanswari (watu wa Madina): Hawampendi ila mtu muumini, na hawamchukii ila mnafiki, atakayewapenda Answaar na Mwenyezi Mungu atampenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu atamchukia".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa, kuwapenda Manswari katika watu wa Madina, ni alama ya ukamilifu wa imani; na hii ni kwa sababu ya kuwahi kwao kuutetea Uislamu na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kuleta amani pia, na kwenda kwao mbio kuwapa hifadhi waislamu, na kutoa kwao mali zao na nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, nakuwa kuwachukia ni alama ya unafiki. Kisha akaweka wazi -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayewapenda Manswari Mwenyezi Mungu humpenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu humchukia.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Fanyeni matendo na muwe na msimamo, na tambueni kuwa hatosalimika mmoja wenu kwa sababu ya matendo yake, wakasema: Hata wewe ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?! Akasema: Hata mimi isipokuwa atakaponifunika mimi Mwenyezi Mungu kwa huruma zake na fadhila zake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnahimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba kufanya amali njema, na wamche Mwenyezi Mungu kadiri wawezavyo, pasina kuchupa mipaka wala uzembe, na wakusudie katika amali zao kupatia kwa kuwa na ikhlasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kufuata mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili amali zao zikubaliwe, ili iwe ni sababu ya kuteremka kwa rehema juu yao. Kisha akawaeleza kuwa amali hazitomuokoa yeyote miongoni mwao kamwe; bali ni lazima kuwe na rehema ya Mwenyezi Mungu. Wakasema: Hata wewe ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hazitokuokoa amali zako pamoja na ukubwa wa kiwango chake? Akasema: Hata mimi, ila kama atanisitiri Mwenyezi Mungu kwa fadhila na rehema zake.
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu katika umma wowote kabla yangu, isipokuwa kunakuwa katika umma wake na watu wake wapendwa na watu wanaoyachukua mafundisho yake na wanafuata amri yake, kisha wanakuja kutofautiana baada yao watu wanaowafuata, wanazungumza yale wasiyoyafanya, na wanafanya ambayo hawakuamrishwa, atakayepigana nao kwa mkono wake basi huyo ndio muumini, na atakayepigana nao kwa moyo wake basi naye ni muumini, na atakayepigana nao kwa ulimi wake basi naye ni muumini, na hakuna zaidi ya hapo katika imani punje ndogo ya Haradali" (yaani kwa asiyefanya hivyo hana imani hata punje ndogo).
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakuna Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwa umma kabla yake isipokuwa huwa na watu safi na watetezi, na mujahidina wa kweli kutoka katika umma wake wanaofaa kwa ukhalifa (uongozi) baada yake, wanaofuata Sunna zake na kufuata amri yake, kisha baada ya hao watangulizi wema wanakuja watu ambao hawana kheri ndani yake; Wanasema wasiyoyafanya, na wanafanya yale ambayo hawakuamrishwa kuyafanya, na atakayepigana nao kwa mkono wake basi huyo ni Muumini, atakayepigana nao kwa ulimi wake pia ni Muumini, na atakayepigana nao kwa moyo wake pia ni Muumini, na hakuna imani hata chembe ya haradali (ulezi) baada yake.
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Nimepewa mambo matano ambavyo hakupewa mtu mwingine miongoni mwa Manabii kabla yangu. Nimenusuriwa na hofu kwa umbali wa safari ya mwezi mmoja. Na nimefanyiwa ardhi kuwa mahali pa kuswalia na ni twahara (safi). Hivyo, yeyote katika umma wangu atakapokutwa na swala, basi na aswali (popote). Na nimehalalishiwa ngawira. Na kila Nabii alikuwa akitumwa kwa umma wake tu, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote. Na nimepewa uombezi (Siku ya Kiyama)”.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu amempa mambo matano ambayo hakupewa yeyote katika Manabiii kabla yake: La kwanza: Nimeepushwa na hofu, na hofu hiyo inatiwa katika nyoyo za maadui zangu hata kukiwa kati yangu na wao mwendo wa kutembea mwezi mzima. La pili: Tumefanyiwa Ardhi kwetu kuwa Msikiti tuswali mahala popote tutakapokuwa, na udongo wake ni twahara (safi) pale tunaposhindwa kutumia maji. La tatu: Tumehalalishiwa ngawira za vita, nazo ni zile wanazozichukua waislamu katika vita vyao na makafiri. La nne: Nimepewa utetezi mkubwa katika kuwapumzisha watu na misukosuko ya kisimamo cha siku ya Kiyama. La tano: Nimetumwa kuja kwa viumbe wote binadam wao na majini wao, kinyume na Manabii walikokuwa kabla yake, walikuwa wakitumwa kwa watu wao pekee.
Kutoka kwa Haritha bin Wahabi Al-Khuzaai radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hivi nisikuelezeni watu wa peponi? Kila mnyonge mwenye kujishusha, na lau kama angeliapia kwa Mwenyezi Mungu basi angelimuepusha (na kutopokea kiapo chake), hivi nisikuelezeni watu wa motoni? kila jeuri mkaidi mwenye kiburi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya sifa za watu wa peponi na za watu wa motoni. Asilimia kubwa ya watu wa peponi ni: "Kila mnyonge mwenye kujishusha", yaani: Mnyenyekevu mwenye kujishusha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, mwenye kuidhalilisha nafsi yake kwake, mpaka baadhi ya watu wakamdhoofisha na kumdharau, na huyu mwenye kujidhalilisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu lau kama ataapa kwa Mwenyezi Mungu kiapo cha kutamani jambo katika karama za Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu angemuepusha na kutopokea kiapo chake, na angelimtimizia alichokiapia na angelijibu ombi lake na dua yake. Na asilimia kubwa ya watu wa motoni ni: Kila "Mkaidi" Naye ni fidhuli mkorofi mwingi wa ugomvi, au muovu asiyetii kwa kufata jambo la kheri, "Jeuri" Naye ni mwenye kiburi, mlafi, mwenye mwili mkubwa, mwenye kutembea kwa maringo, mwenye tabia mbaya, "Mwenye kufanya kiburi" kwa kuikataa kwake haki, na kwa kumdharau mtu mwingine.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Hakika peponi kuna daraja mia moja kaziandaa Mwenyezi Mungu kwaajili ya wenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya daraja mbili ni kama masafa ya baina ya mbingu na ardhi".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAnaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hii kuhusu fadhila za wenye kupigana katika njia yake nakuwa Mwenyezi Mungu kawaandalia peponi daraja mia moja, masafa kati ya daraja mbili ni kama yaliyo baina ya mbingu na ardhi.