





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-: Yakuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Kiyama, akasema: Lini Kiyama? Akasema: “Umetayarisha nini kwa ajili yake?” Akasema: Hapana, isipokuwa ninampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake. Akasema: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Hakuna lililotufurahisha zaidi ya kauli ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Mimi ninampenda Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abubakari na Omari, na ninataraji kuwa pamoja nao kutokana na mapenzi yangu kwao, hata kama nisipofanya sawa na matendo yao.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeBedui mmoja anayeishi jangwani alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Je, saa ya Kiyama itatokea wakati gani? Basi rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Umeiandalia mambo gani mema? Akasema muulizaji: Sikutayarisha jambo kubwa kwa ajili yake isipokuwa ninampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wala hakutaja ibada nyinginezo za moyo, za kimwili, au za kifedha. Kwa sababu zote ni matawi ya upendo unaotokana na hayo, na kwa sababu upendo wa dhati humsukuma mtu kujitahidi kufanya matendo mema. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Wewe utakuwa pamoja na unayempenda peponi. Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakafurahishwa sana na habari hii njema. Kisha Anas radhi za Allah ziwe juu yake akaeleza kuwa hakika anampenda Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abubakari na Omari, na anatarajia kuwa pamoja nao, hata kama amali zake si kama amali zao.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hivi nikuhadithieni hadithi kuhusu Dajali ambayo hajawahi kuhadithia Nabii yeyote watu wake! Hakika yeye ni chongo, na hakika atakuja akiwa pamoja na mfano wa pepo na moto, anayoisema kuwa ni pepo huo ndio moto, na hakika mimi ninakutahadharisheni kama alivyo watahadharisha Nabii Nuhu watu wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnawaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake kuhusu Dajali, sifa zake, na dalili zake, kwa mambo ambayo hakuna Nabii yeyote aliyetangulia kuyasimulia kabla yake, miongoni mwa hayo ni: Chongo wa jicho. Na Mwenyezi Mungu kampa kitu mfano wa Pepo na Moto, kulingana na mtazamo wa macho. Bali Pepo yake ni Moto na Moto wake ni Pepo, mwenye kumtii atamuingiza katika Pepo hii kama watu wanavyoiona, lakini uhalisia wake ni Moto wenye kuunguza, na atakayemuasi atamuingiza Motoni kama watu wanavyouona, lakini kwa uhalisia ni Pepo nzuri. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akatuonya dhidi ya fitina yake kama vile Nuhu alivyowaonya watu wake kuhusu hilo.
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: "Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake"
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadAlibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu hufanana na rafiki na jamaa yake wa dhati katika nyenendo na tabia zake, na urafiki huathiri maadili, tabia na matendo, na kwa ajili hiyo alielekeza vyema katika uchaguzi wa rafiki. Kwa sababu atamuongoza rafiki yake katika imani na uongofu na kheri, na atakuwa ni msaada kwa rafiki yake.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza, anaamka mtu akiwa muislamu anafika jioni akiwa kafiri, na anashinda akiwa muumini anaamka asubuhi akiwa kafiri, anauza dini yake kwa thamani ndogo ya dunia"
Imepokelewa Imamu MuslimMtume rehema na amani ziwe juu yake anamtaka Muumini kufanya hima na kufanya mambo mengi ya kheri kabla hayajashindikana, na akashughulishwa na kuja kwa fitna na mambo yenye kutatiza yanayoweza kuzuia kufanya matendo mema, na kuyaziba, na hali ni kwamba, ni giza kama kipande cha usiku ambao ndani yake haki imechanganyika na batili, na kukawawia vigumu watu kutofautisha baina yake, na kwa sababu ya ukali wake (Fitina hiyo), mtu huchanganyikiwa kiasi cha kuamka muumini, na kufika jioni ni kafiri, kushinda Muumini na kufika asubuhi kawa kafiri, anaiacha dini yake kwa starehe za muda mfupi za dunia.
Kutoka kwa Zainab bint Jahshi radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia ndani kwake akiwa na mfadhaiko huku akisema: “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.” Jahshi akasema: Basi nikasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je, tuangamie na hali miongoni mwetu wamo watu wema? Akasema: "Ndio, ikiwa maovu yatakithiri".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Zainab bint Jahshi Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akiwa na mfadhaiko na khofu kubwa, akasema: Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, akiashiria kutaraji jambo baya litatokea, na hakuna kusalimika katika hilo ila kwa kurejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasema: Ole wao Waarabu kutokana na shari inayokaribia kutokea, leo imefunguliwa katika ngome ya Ya'ajuj na Ma'ajuj kiasi hiki, ambacho ni ukuta alioujenga Dhul-Qarnain, na akazungusha duara kwa kidole gumba chake na kile kinachofuata (kuonyesha kiasi kilicho funguliwa). Akasema Zainab Mwenyezi Mungu amuwie radhi: Vipi Mwenyezi Mungu atuangamize na hali wapo waumini wema miongoni mwetu? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: “Maovu yatakapokithiri, kama vile uovu, ufisadi, maasi, uzinzi, pombe na vitu vingine, maangamizo yatawakumba wote.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Majaribio hayaachi kumpata muumini wa kiume na muumini wa kike katika nafsi yake, na watoto wake, na mali yake mpaka atakapokutana na Mwenyezi Mungu ilhali hana dhambi hata moja."
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa: “Balaa na mtihani havikomi kwa muumini wa kiume na wa kike, katika afya yake na mwili wake, na kwa watoto wake, kama magonjwa, kifo, uasi na mengineyo, na katika mali yake kutiwa umasikini, kutoweka kwa biashara, kuibiwa, kuvurugika kwa maisha na dhiki katika riziki, na ugumu wa maisha, mpaka Mwenyezi Mungu atamfutia dhambi zake zote kwa mateso haya, ili atakapokutana na Mwenyezi Mungu atakuwa kasafishika na madhambi na maovu yote aliyoyafanya.
Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Msimfanyie Mwenyezi Mungu washirika na hali nyinyi mnajua, Amesema bin Abbas katika aya hii: Washirika, ni ushirikina, uliofichikana kuliko mkanyago wa mdudu chungu katika jiwe kubwa jeusi katika giza nene la usiku". Nayo ni mtu kusema: Namuapa Mwenyezi Mungu na maisha yangu ewe fulani, naapa kwa maisha yangu, na kusema: laiti kisingekuwa kimbwa hiki wezi wangetuvamia, na lau kama si bata huyu wezi wangetujia, na kauli ya mtu kusema kumwambia mwenzie: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukitaka wewe, na kauli ya mtu: lau kama si Mwenyezi Mungu na fulani, usimuweke ndani yake fulani hii yote ina ushirikina".
Imepokelewa na Abii HaatimAmesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Msimfanyie Mwenyezi Mungu washirika na hali nyinyi mnajua", akawakataza watu wasimfanyie mifano wanaoelekezewa chochote katika ibada zake; na hali wao wanajua kuwa kweli Mwenyezi Mungu yeye pekee ndiye muumbaji na mgawaji wa riziki; nakuwa hawa washirika hawajiwezi bali ni mafakiri (wahitaji) hawamiliki jambo lolote, na ameelezea bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa vijiungu kwa maana ya washirika, na akataja mifano ya kuwafanya hivyo, nayo imefichikana (hiyo shirki) kuliko athari (kishindo cha kukanyaga) cha sisimizi juu ya jiwe jeusi katika giza nene la usiku, kisha akataja mifano juu ya hilo: nayo ni mtu kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kubwa zaidi kuliko hilo ni kumsawazisha huyo na Mwenyezi Mungu ukasema: Namuapa Mwenyezi Mungu na maisha yangu, au ukaitazama sababu bila kumjali msababishaji, na wala usilirudishe jambo kwa Mwenyezi Mungu, ukasema: Lau kama si mbwa huyu anayetulinda basi wangetujia wezi, au mtu akasema: laiti isingekuwa bata hapa nyumbani anayetuzindua anapoingia yeyote mgeni basi wezi wangelitujia, na ni katika shirki pia: kauli ya mtu kumwambia mwenzie: akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, na kauli ya mtu: lau kama si Mwenyezi Mungu na fulani, kisha akatilia mkazo juu ya hayo yote kuwa ni shirki ndogo, na ikiwa ataitakidi kuwa mtu au bata au mbwa ndiyo inayoathiri yenyewe bila Mwenyezi Mungu basi hiyo ni shirki kubwa.
Imepokewa Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiseme: Ni kwakutaka Mwenyezi Mungu na fulani, lakini semeni: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani".
Imepokelewa naAbu Daud na Nasai katika Sunan Alkubra na AhmadAmekataza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa muislamu kusema katika maneno yake: "Akitaka Mwenyezi Mungu na akitaka fulani", Au akitaka Mwenyezi Mungu na fulani; Na hii ni kwa sababu matashi ya Mwenyezi Mungu na maamuzi yake ni ya moja kwa moja na hakuna yeyote anaye shirikiana naye, Na katika matumizi ya kiunganishi "Na" hii inamaanisha kuwa kuna mtu anayeshirikiana pamoja na Mwenyezi Mungu na kuwa wako sawa katika maamuzi. Lakini aseme: Akitaka Mwenyezi Mungu, kisha fulani, Hivyo basi afanye matashi ya mja yanafuata matashi ya Mwenyezi Mungu kwa kauli yake: " Kisha" badala ya "Na", kwa sababu kiunganishi "Kisha" humaanisha kuja baada ya kitu kingine na kuchelewa pia.
Kutoka kwa Abdillahi bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "kuapa kwangu kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa uongo napenda zaidi kuliko kuapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu nikisema ukweli".
Imepokelewa na Ibn Abii Shaybah - Imepokelewa na Abdul RazaaqAnasema bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuapa kwangu kwa jina la Mwenyezi Mungu juu ya kitu ambacho mimi ninasema uongo -tukichukulia kutokea hilo- kunapendeka zaidi kwangu kuliko kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu juu ya kitu ambacho mimi ni mkweli ndani yake; na hii nikuwa kuapa kwa Mwenyezi Mungu kwa uongo kumeshinda kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu kwa ukweli; kwasababu kuapa kwa Mwenyezi Mungu katika hali hii kuna uzuri wa tauhidi, na kuna ubaya wa dhambi la uongo, na kuapa kwa asiyekuwa yeye kwa ukweli, kuna uzuri wa ukweli na dhambi ya ushirikina, na zuri la tauhidi ni kubwa zaidi kuliko zuri la ukweli, na dhambi la uongo ni jepesi sana kuliko dhambi la ushirikina.