





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Sufiani bin Abdillah Al-Thaqafi Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nieleze ndani ya Uislamu kauli ambayo sitomuuliza yeyote zaidi yako, akasema: "Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo".
Imepokelewa na Muslim na AhmadSwahaba Sufiani bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake alimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amfundishe kauli iliyokusanya maana nzima ya Uislamu ili ashikamane nayo na wala hatomuuliza yeyote zaidi yake? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Sema: Nimempwekesha Mwenyezi Mungu, na nimemuamini kuwa yeye ndiye Mola wangu na Mungu wangu na Muumba wangu na muabudiwa wangu wa haki aisye na mshirika wake, kisha awe mtiifu katika sheria za Mwenyezi Mungu kwa kutekeleza faradhi za Mwenyezi Mungu na kuacha maharamisho ya Mwenyezi Mungu na adumu katika hilo.
Imepokelewa kutoka kwa Abdullah bin Amrou binil Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema na amani ziwe juu yake- "Kwa hakika Mwenyezi Mungu atamchagua mtu mmoja katika umma wangu mbele ya mkusanyiko wa watu siku ya Kiyama basi atamkunjulia mafaili tisini na tisa, na kila faili moja lina ukubwa sawa na upeo wa macho yanapoishia kuona, kisha atasema: Je unapingamizi katika haya yaliyopo ndani ya mafaili haya?, je waandishi wangu wenye kuhifadhi yenye kuandikwa wamekudhulumu? basi atajibu: "Hapana ewe Mola wangu, hawakunidhulumu": Basi atamwambia: Je unalakujitetea? Basi atasema: "Hapana ewe Mola wangu", atasema: Hakika wewe unayo matendo mema kwetu, na kwa hakika hautodhulumiwa chochote leo hii, basi atatolewa kadi iliyoandikwa Ash-hadu An-laa Ilaaha illa llaahu wa Ash-hadu Anna Muhammadan Abduhuu wa Rasuuluhu, hivyo atasema: Ewe Mola wangu ni kadi gani hii na ni faili gani hili? Basi atasema: Kwa hakika wewe hutodhulumiwa", Mtume akasema: Basi yatawekwa mafaili katika kipimo na kadi itawekwa upande wapili wa kipimo, basi ukawa mwepesi ule upande uliowekwa mafaili, na ukawa mzito ule upande uliowekwa kadi, na haiwezekani kitu chochote kuwa kizito kuliko neno la Tauhidi ambalo ni Laa Ilaaha illa llaah Muhammadan Rasuulullah."
Imepokelewa na Tirmidhi na bin MajahAlitoa habari Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu atamchagua mtu katika umma wake kwenye kundi la watu siku ya Kiyama atamuita ili amuhesabu, basi atamtolea mafaili tisini na tisa na mafaili hayo ni ya matendo yake mabaya ambayo alikuwa akiyafanya Duniani, na urefu wa kila faili ni mfano wa upeo wa macho, Kisha Mwenyezi Mungu atamwambia mtu huyu: Je unapinga chochote katika haya yaliyoandikwa katika mafaili? Je Malaika wangu wenye kuhifadhi wanayoandika wamekudhulumu? Basi atasema mtu yule: Hapana ewe Mola wangu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Je una chochote cha kujitetea nacho katika matendo yako uliyoyatanguliza miongoni mwa matendo ya Duniani?katika matendo uliyoyafanya kwa kusahau au kwa kukosea au kwa kutojua, Basi atasema mtu yule: Hapana ewe Mola wangu sina chochote cha kujitetea nacho. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Si hivyo, kwa hakika wewe una mambo yaliyoandikwa kwetu sisi, na kwa hakika wewe hutodhulumiwa leo hii. Akasema: Basi itatolewa kadi iliyoandikwa ndani yake: Ash-hadu An-laa ilaaha illa llaah wa Ash-hadu Anna Muhammadan Ab-duhuu wa Rasuuluhu. Basi atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Angalia Mizani yako. Basi atasema mtu yule hali ya kuona ajabu: Ewe Mola wangu! ni uzito wanini huu wa kikadi kidogo pamoja na kupimwa na mafaili yote haya? Basi atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: hautadhulumiwa leo hii. Akasema: Basi mafaili yatawekwa katika sehemu ya kupimia, na Kadi kwenye sehemu nyingine ya kupimia; Hivyo basi ukawa mwepesi upande wa kupimia palipo na Mafaili na ukawa mzito upande wa kupimia palipo na Kadi, hivyo basi Mwenyezi Mungu akamsamehe.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto alimtuma Malaika Jibril -Amani iwe juu yake- aende peponi Akamwambia: Iangalie hiyo pepo na yale niliyo waandalia humo watu wa peponi, basi Jibrili akaiangalia Pepo kisha akarudi, akasema: Naapa kwa utukufu Wako ewe Mwenyezi Mungu hatozisikia mtu yeyote habari za pepo kisha asiingie humo, kisha akamuamrisha kuizungushia Pepo hiyo mambo yenye kuchukiza, kisha akamwambia nenda tena ukaiangalie na uangalie yale niyowaandalia watu wake humo peponi. Basi akaiangalia ghafla akaiona imezungushwa vyenye kuchukiza, akasema: Naapa kwa utukufu Wako kwa hakika ninahofia kuwa hatoingia mtu yeyote. Akasema kumwambia Jibrili nenda na uuangalie Moto na yale niliyo waandalia humo watu wa Motoni. Basi akauangalia Moto na akauona Moto ulivyopambwa, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu Wako hatoingia yeyote humo, basi akaamrisha ukazungushwa mambo yenye kutamanisha, basi akamwambia: Rudi na uuangalie tena. Basi akauangalia akaukuta umepambwa na kuzungushwa yenye kutamanisha, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu wako kwa hakika nahofia yakuwa hatosalimika mtu yeyote isipokuwa ataingia Motoni."
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na NasaaiAlitoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto, alimwambia Jibril -Amani iwe juu yake- nenda mpaka Peponi na uangalie humo, basi akaenda na akaangalia ndani ya Pepo kisha akarudi, Basi Jibrili akasema: Ewe Mola wangu, nina apa kwa utukufu wako kuwa hatosikia yeyote habari za Pepo na yaliyo humo miongoni mwa neema na mazuri na kheri mbalimbali isipokuwa atapenda kuingia humo, na atafanya matendo ili aweze kuingia humo, Kisha Mwenyezi Mungu baada ya kauli hiyo akaizungushia pepo mambo yenye kuchukiza na magumu, yakiwemo kutekeleza maamrisho na kujiepusha na makatazo, basi ikawa mwenye kutaka kuingia humo anatakiwa akivuke kizingiti cha hayo yenye kuchukiza. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Ewe Jibril nenda na utazame Pepo", Baada ya kuwa amekwisha izungusha mambo yenye kuchukiza, Basi akaenda kisha akaitazama, kisha akaja na akasema: Nina apa kwa utukufu wako ninahofia kuwa hatoingia yeyote kwa sababu ya mambo mazito na magumu ambayo yapo kwenye njia ya kuweza kuingia katika Pepo. Na Mwenyezi Mungu alipoumba Moto, alisema: Ewe Jibril! nenda nauutazame Moto, basi akaenda na akautazama, Kisha Jibril akaja na akasema; Ewe Mola wangu, nina apa kwa utukufu wako, kuwa hatosikia yeyote habari ya vilivyomo humo miongoni mwa adhabu na matatizo mateso isipokuwa atachukia ili asiingie humo na atajiweka mbali na vitakavyomsababishia kuingia humo. Kisha Mwenyezi Mungu akauzungushia Moto na akaweka njia ya kuufikia Moto huo ni vitu vyenye kutamanisha na vyenye ladha, kisha akasema: Ewe Jibril, nenda na uutazame Moto, Basi Jibril akaenda na akautazama moto, kisha akaja na akasema: Ewe Mola wangu naapa kwa utukufu wako kwa hakika nimepatwa na hofu na uoga na nimepatwa na huruma yakuwa hatosalimika yeyote na moto huo kwa namna ulivyozungukwa moto na vyenye kutamanisha na vyenye ladha.
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Amrou Bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, akasema: Na Arshi yake ilikuwa juu ya maji."
Imepokelewa Imamu MuslimAnatoa habari Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu aliandika mambo yote ambayo yatatokea miongoni mwa mambo ya kuwakadiria viumbe kwa uchanganuzi kuanzia kuishi na kufa na riziki na mambo mengineyo aliyaandika katika Lauhil Mah-fuudh kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, na hayo aliyoyaandika hutokea kwa mujibu wa alivyopanga Hivyo basi kila kitu chenye kutokea, basi kinatokea kwa mipango ya Mwenyezi Mungu na kukadiria kwake. Basi jambo lolote linalompata mja lisingeweza kumkosa, na lenye kumkosa lisingeweza kumpata.
Imepokewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika kilicho kati ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala".
Imepokelewa Imamu MuslimAnatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuacha swala ya faradhi, na akaeleza kuwa kati ya mtu na baina ya kuingia katika shirki na ukafiri ni kuacha swala, swala ni nguzo ya pili katika nguzo za Uislamu, na jambo lake ni kubwa katika Uislamu, atakayeiacha kwa kupinga uwajibu wake amekufuru kwa makubaliano ya waislamu, na akiiacha moja kwa moja kwa uzembe na uvivu pia ni kafiri, na yamenukuliwa makubaliano ya Masahaba juu ya hilo, na ikiwa anaiacha baadhi ya wakati na wakati mwingine anaswali, basi anajitia katika makemeo haya makubwa.
Kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni sala, na atakayeiacha sala basi huyo ni kafiri".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadAnabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ahadi na mkataba kati ya waislamu na wasiokuwa wao katika makafiri na wanafiki ni swala, atakayeiacha atakuwa amekufuru.
Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anakukatazeni kuapa kwa baba zenu", akasema Omari: Wallahi sikuwahi kuapa tena kwa kiapo hicho tangu nilipomsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alipokataza hivyo, kwa kutamka mwenyewe wala kwa kunukuu kiapo cha mtu mwingine.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakataza kuapa kwa baba, atakayetaka kuapa basi asiape ila kwa jina la Mwenyezi Mungu, na wala asiape kwa jina la mwingine. Kisha Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake akaeleza kuwa hakuwahi tena kuapa tangu alipomsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akikataza kufanya hivyo, si kwa makusudi wala kwa kunukuu kiapo cha mtu mwingine aliyeapa kinyume na Mwenyezi Mungu.
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa jambo la kwanza litakalohukumiwa baina ya watu katika dhulma zao wao kwa wao siku ya Kiyama: Itakuwa katika damu, kama kuua na kujeruhi.
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, akasema: "Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo, na ama mwingine alikuwa akitembea kwa kuchonganisha watu" Kisha akachukua kuti bichi, akalikata vipande viwili, akapanda katika kila kaburi kipande kimoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa nini umefanya hivi? Akasema: "Huenda yakawapunguzia kinachowapata kwa muda kabla hayajakauka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili akasema: Hakika watu wa makaburi haya mawili wanaadhibiwa; na wala hawaadhibiwa katika jambo kubwa, hata kama ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, Ama mmoja wao alikuwa hajali katika kuhifadhi mwili wake na nguo zake kutokana na mkojo anapokidhi haja yake, Na mwingine alikuwa akitembea kati ya watu kwa uchonganishi, akinukuu maneno ya mtu mwingine kwa lengo la kuwadhuru na kuleta sintofahamu baina yao na ugomvi kati ya watu.