





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Marthad Al-Anawiy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea".
Imepokelewa Imamu MuslimAmekataza -Rehema na amani ziwe juu yake- kukaa juu ya makaburi. Kama alivyokataza kusali kwa kuyaelekea makaburi, kwa kaburi kuwa upande wa kibla cha mwenye kusali; kwa sababu hilo ni katika njia za shirki.
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mama Salama alimsimulia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kisa cha kanisa aliloliona katika ardhi ya Ethiopia, likiitwa kanisa la Mtakatifu Maria, akasimulia aliyoyaona ndani yake miongoni mwa picha, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Watu hao anapokufa kwao mja mwema, au mwanaume mwema, wanajenga juu ya kaburi lake mahala pakuabudia, na wanachora ndani yake picha hizo, hao ndio viumbe waovu zaidi mbele ya Allah
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmesimulia mama wa waumini mama Salama radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba alipokuwa katika ardhi ya Ethiopia aliona Kanisa -linaloitwa kwa jina la Mtakatifu Maria- ndani yake kukiwa na picha na mapambo na michoro; akastaajabu kwa kitendo hicho!. Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akafafanua sababu za kuwekwa picha hizo; Akasema: Hakika hao unaowataja hapa walikuwa anapokufa kwao mtu mwema wanajenga Msikiti juu ya kaburi lake, na wanasali ndani yake, na wanachoro picha hizo, Na akabainisha kuwa mfanyaji wa hilo ni kiumbe muovu zaidi kuliko wote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu kitendo chake hicho kinapelekea katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
kutoka kwa Abdullahi bin Amry -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Umejengwa uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mja wake na Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba tukufu, na kufunga ramadhani".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeufananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Uislamu na jengo madhubuti kwa nguzo zake tano zenye kulibeba jengo hilo, na mambo mengine ya Uislamu kama nyenzo zenye kulikamilisha jengo hilo, Na nguzo ya kwanza katika nguzo hizo ni: Shahada mbili; Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hizo mbili ni nguzo moja; kila moja haitengani na nyingine, mja anazitamka kwa kukiri umoja wa Mwenyezi Mungu na kustahiki kwake kuabudiwa yeye pekee pasina mwingine, na kufanyia kazi makusudio ya nguzo hii, na kwa kuamini utume wa Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kumfuata yeye. Na nguzo ya pili: Ni kusimamisha swala, nazo ni swala tano za faradhi usiku na mchana: Alfajiri, Adhuhuri, lasiri, Maghribi, na Ishaa, kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake. Na nguzo ya tatu: Ni kutoa zaka ya lazima, nayo ni ibada ya mali ya wajibu katika kila mali iliyofikia kiwango maalumu katika sheria, ambayo hupewa wastahiki wake. Na nguzo ya nne: Ni Hija, nayo nikutia nia ya kwenda Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada, kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka. Na nguzo ya tano: Ni kufunga mwezi wa Ramadhani, nako ni kujizuia na kula na kunywa na vinginevyo miongoni mwa vyenye kufunguza kwa nia ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuzama jua.
Hadithi imepokelewa na Abii Said Alkhuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Yeyote miongoni mwenu atayeona jambo ovu na baya basi aliondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi kuliondoa kwa mkono wake basi aliondoe kwa ulimi wake, na ikiwa hawezi kuliondoa kwa ulimi basi na alichukie kutoka moyoni mwake, na kuchukia moyoni ni udhaifu wa imani".
Imepokelewa Imamu MuslimAnatuamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kuuondoa uovu, na uovu ni kila alilolikataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kadiri ya uwezo, Hivyo basi ikiwa mtu atauona uovu basi ni wajibu juu yake kuuondosha kwa mkono wake ikiwa atakuwa na uwezo wa kuuondosha uovu huo. Ikiwa atashindwa kuondosha uovu kwa mkono wake basi na auondoshe kwa ulimi wake, kwa kumkataza mwenye kufanya uovu huo, na amueleze madhara ya uovu huo na amuongoze katika kheri badala ya kufanya shari hiyo. Basi ikiwa atashindwa hatua hii ya pili, basi auondoshe uovu kwa kuchukia moyoni mwake, kwa kuuchukia uovu huo, na aazimie moyoni mwake kuwa kama angekuwa na uwezo wa kuuondosha uovu huo angeuondosha, Na kuuondosha uovu kwa moyo ni katika kiwango dhaifu zaidi cha imani katika kuuondosha uovu
Imepokelewa hadithi kutoka kwa bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, amesema: Alisema mtu mmoja: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hivi sisi tutaadhibiwa kwa tuliyoyafanya katika zama za ujinga kabla yakuwa waislamu?Akasema "Yeyote atakayefanya wema katika Uislamu basi hatoadhibiwa kwa yale aliyoyatenda katika zama za ujinga, na yeyote atakaye tenda maovu akiwa katika Uislamu ataadhibiwa kwa makosa yake ya mwanzo na ya mwisho".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnatuwekea wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ubora wa kuingia katika Uislamu, Na kuwa mwenye kusilimu na uislamu wake ukawa mzuri na akawa mtakasifu na mkweli, basi hatoadhibiwa kwa makosa aliyoyafanya kabla ya uislamu, Na atakaye fanya uovu akiwa katika uislamu, yaani kwa kuwa mnafiki au akatoka katika dini yake, basi huyo ataadhibiwa kwa aliyoyafanya akiwa bado hajaingia katika uislamu na ataadhibiwa pia kwa yale aliyoyafanya akiwa katika uislamu.
Hadithi imepokelewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-akasema: "Waonaje ikiwa nitaswali swala zilizofaradhishwa, na nikafunga Ramadhani, na nikahalalisha kilichokuwa halali na nikaharamisha kilichokuwa haramu, na wala sikuzidisha zaidi ya hayo je nitaingia peponi?Akasema: "Ndiyo", Akasema mtu yule: "Namuapia Mwenyezi Mungu sizidishi zaidi ya matendo hayo kitu chochote".
Imepokelewa Imamu MuslimAnaweka wazi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayeswali swala tano zilizofaradhishwa na wala hakuzidisha zaidi ya hizo swala tano kwa kuswali swala za Sunna, na akafunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na akawacha kufunga funga za sunna, na akaamini uhalali wa vilivyo halali na akavitekeleza na akaamini uharamu wa vilivyo haramu na akajiepusha navyo, kwa hakika mtu huyo ataingia Peponi.
Imepokelea kutoka kwa Abii Maalik Al-Ash-ariy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: "Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye kuwa na msimamo na kumtii Mwenyezi Mungu, na akawa ni mwenye kuikomboa nafsi yake kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".
Imepokelewa Imamu MuslimAnafahamisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa twahara na usafi wa nje ambao ni udhu na kuoga ni sharti la usahihi wa swala. Na kuwa neno: "Alhamdulillah hujaza mizani" nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu aliyetakasika na machafu, na kumsifia kwa sifa za ukamilifu zitakazopimwa siku ya kiyama na kuijaza mizani ya matendo. Na kuwa neno: "Sub-hanallah na Alhamdulillah" na maneno hayo ni kumtakasa Mwenyezi Mungu na kumsifia kwa sifa zilizokamilika na zilizotimia ambazo anastahiki sifa hizo pamoja kumpenda yeye na kumtukuza hujaza sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi. Na kuwa "Swala ni nuru" ya mja katika moyo wake, na katika uso wake na kaburini mwake na siku ya kufufuliwa kwake. Na kuwa "Sadaka ni ushahidi" Na ni dalili ya ukweli wa imani ya muumini, na tofauti yake na mnafiki ambaye huzuia kutoa sadaka kwa kuwa mnafiki haamini malipo ya kutoa sadaka. Na "kuwa subira ni mwangaza" -na subira ni kuizuia nafsi kutoku papatika na kuwa na hasira, subira ni nuru inayokuwa na joto na kuunguza, kama vile mwanga wa Jua; kwa sababu subira ni tabu kubwa inahitaji kuilazimisha nafsi na kuizuia na kile inachokipenda; hivyo haachi kuwa na mng'ao mtu mwenye subira, mwenye kuongoka na mwenye kudumu katika usahihi, nako ni kusubiri katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kutomuasi yeye, na kuwa na subira kwenye matatizo na aina mbalimbali za mambo yenye kuchukiza katika Dunia. Na kuwa "Qur'ani ni hoja kwako wewe" kwa kuisoma na kuifanyia kazi, au yaweza kuwa " Hoja dhidi yako" kwa kuiacha pasina kuifanyia kazi au kuisoma. Kisha akafahamisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakuwa watu wote huenda mbio na hutawanyika na huamka toka usingizini mwao na wanatoka kwenye majumba yao kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali miongoni mwao kuna wenyekuwa na msimamo katika kumtii Mwenyezi Mungu, hivyo anakuwa ameikomboa nafsi yake na moto, na miongoni mwao kuna mwenye kwenda kinyume na kuacha kumtii Mwenyezi Mungu na akaingia katika maasi, hivyo akaiangamiza na kuingia motoni.
Kutoka kwa Muadhi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Nilikuwa nimepanda Punda nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Punda akiitwa Ufairu, akasema Mtume: "Ewe Muadhi hivi unazijua haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake na zipi haki za waja kwa Mwenyezi Mungu?" Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: " Basi tambua kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni wamuabudu yeye na wala wasimshirikishe na kitu chochote, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu asimwaadhibu yeyote ambaye hajamshirikisha yeye na chochote" Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwanini nisiwape watu habari hii? Akasema Mtume: "Usiwape habari hii kwani watabweteka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaziweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja ni kuwa wamuabudu yeye peke yake na wala wasimshirikishe yeye na kitu chochote. Na kuwa haki za waja kwa Mwenyezi Mungu ni kutowaadhibu wenye kumpwekesha ambao hawamshirikishi yeye na chochote. Kisha Muadhi akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwa nini nisiwape watu habari hii njema ili wafurahi kwa jambo hili bora? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamkataza kwa kuogopea kuwa watategemea habari hiyo.
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Mtu mmoja alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nini maana ya wawili wenye kustahiki? Akasema: "Yeyote atakaye kufa hali ya kuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia peponi, na atakaye kufa akiwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia motoni"
Imepokelewa Imamu MuslimMtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo mawili: ambayo yanasababisha kuingia peponi na yanayo sababisha kuingia motoni? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akamjibu kuwa mambo ambayo yanamsababishia mtu kupata pepo ni kuwa afe mtu hali yakuwa anamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na wala hamshirikishi na kitu chochote. na kuwa mambo ambayo yanapelekea kuingia motoni, ni kuwa afe mtu hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na anamuwekea Mwenyezi Mungu washirika na vifananishwa katika uungu wake na uumbaji wake na katika majina yake na sifa zake.