





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- muislamu kumhama ndugu yake muislamu zaidi ya siku tatu, wanakutana wote hamsalimii wala hamsemeshi. Na mbora kati ya hawa wagomvi wawili ni yule anayejaribu kuondoa kuhamana huku, na akaanza kwa salamu, na makusudio ya kuhamana hapa ni sababu ya kujikweza, ama kuhamana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kama kuwahama waovu na wazushi na marafiki waovu, hili halina muda maalum, bali limeambatana na masilahi katika kuhama, na linamalizika kwa kuondoka maslilahi yake.
kutoka kwa Abuu Swirma -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakayewatia watu ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtilia ugumu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadAmetahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutomuingizia madhara muislamu, au kumtia tabu katika jambo lolote katika mambo yake; Yeye mwenyewe au mali yake au familia yake, nakuwa atakayefanya hivyo basi Mwenyezi Mungu atamlipa na atamuadhibu kwa jinsi alivyomfanyia mwenzake.
Imepokelewa kutoka kwa Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikuwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akautazama mwezi usiku (yaani: Usiku wa tarehe 15) akasema: "Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi huu, hamtokingwa katika kumuona kwake, ikiwa mtaweza kufanya hima msizidiwe mkashindwa kusali kabla ya jua kuchomoza na kabla ya kuzama kwake basi fanyeni hivyo" Kisha akasoma: "Na umtukuze Mola wako kwa himdi zake njema kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeWalikuwa Masahaba pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika usiku mmoja akatazama katika mwezi (Usiku wa terehe kumi na nne (14), akasema: Hakika waumini wote watamuona Mola wao Mlezi kwa hakika kabisa kwa macho bila kutatizika, nakuwa hawatosukumana na wala hawatopata tabu wala uzito wakati wa kumuona Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kisha akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ikiwa mtaweza kuzizuia sababu ambazo zinakuzuieni kuto swali swala ya Alfajiri na swala ya Alasiri basi fanyeni hivyo, na zitekelezini kikamilifu ndani ya wakati wake na katika jamaa, kwani hilo ni miongoni mwa sababu za kuuona uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasoma -Rehema na amani ziwe juu yake- Aya "Na utakase sifa za Mola wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuzama kwake"
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Musa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi" Anasema: Kisha akasoma: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali" [Hud:102]
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokuendelea kubaki katika dhulma kwa kufanya maasi na ushirikina na kuwadhulumu watu haki zao, kwani Allah Mtukufu humpa muda dhalimu na humchelewesha na humpa umri mrefu na mali nyingi hamharakishii adhabu; ikiwa hatotubia basi humchukua mara moja na huwa hambakishi na huwa hamuachi kwa sababbu ya wingi wa dhulma zake. Kisha akasoma -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika adhabu yake ni chungu na ni kali" [Hud:102]
Kutoka kwa Abul Hayyaji A-Asady amesema: Ally bin Abii Twalib alisema kuniambia: Hivi sikutumi katika yale aliyonituma kwayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-? (Nenda) Kamwe usiache sanamu au picha ila uifute, wala kaburi refu kupita kiasi isipokuwa umelisawazisha.
Imepokelewa Imamu MuslimAlikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwatuma Masahaba wake wasiache "Sanamu" nayo ni picha ya kiumbe hai yenye kiwiliwili- isipokuwa wameliondoa au kuifuta. Na wasiache kaburi lililonyanyuka ila wamelisawazisha na ardhi, na wayabomoe yaliyomo katika majengo, au walisawazishe lisinyanyuliwe sana kupita usawa wa ardhi, bali linyanyuliwe kiasi cha shibri moja (kipimo cha kiganja).
Imepokewa kutoka kwa Imran bin Huswain - Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa, au akafanya ukuhani au akafanyiwa, au akaroga au akarogewa, na atakayefunga fundo lolote, na atakayemuendea kuhani na akamsadikisha kwa yale ayasemayo atakuwa amekufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammadi Rehema na amani ziwe juu yake".
Imepokelewa na AlbazzarKatoa onyo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa atakayefanya baadhi ya matendo katika umma wake kwa kauli yake: "Si miongoni mwetu" Miongoni mwayo: La kwanza: "Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa" Na asili ya hili: Ni kumuachia ndege wakati wa kuanza kazi kama safari au biashara au mengineyo, akiruka upande wa kulia anajipa matumaini na anaendelea na analolitaka, na akirukia upande wa kushoto anaamini ni mkosi anaacha alichokikusudia, haifai kufanya hivi au kumlipa mwenye kumfanyia hivi, na inaingia hapa kupiga bao kwa kitu chochote sawa sawa chenye kusikika au kuonekana, kama ndege au wanyama au wenye ulemavu au namba au siku au mengineyo. La pili: "Atakayefanya ukuhani au akafanyiwa" Atakayedai kujua elimu ya yaliyofichikana kwa kutumia nyota na vinginevyo, au akaja kwa anayedai kujua elimu ya yaliyofichikana kama kuhani na mfano wake, akamsadikisha kwa yale ayasemayo kwa kudai kwake kujua elimu ya ghaibu, basi atakuwa kakufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake. La tatu: "Atakayeroga au akarogewa" Naye ni yule atakayefanya uchawi yeye mwenyewe, au akampa kazi atakayemfanyia uchawi; ili amnufaishe yeyote au amdhuru, au akafunga fundo lolote kwa kufunga na nyuzi na kuzirogea kwa kusoma kinga za kishirikina zilizoharamishwa na akazipuliza.
Kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayemuendea mpiga ramli akamuuliza kuhusu lolote hazitokubaliwa sala zake siku arobaini".
Imepokelewa Imamu MuslimAnatahadharisha Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- kuwaendea wapiga ramli na hili ni jina la kiujumla la kuhani na mtabiri wa nyota na mpiga ramli na mfano wao, katika wale wanaotumia ishara za vitanguliza ili kudai kujua elimu ya ghaibu, nakuwa kumuuliza pekee mambo ya ghaibu Mwenyezi Mungu atamnyima thawabu za swala yake siku arobaini; na hiyo ni adhabu kwake kwa kosa hili na dhambi kubwa.
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, atazidi kuwa mchawi mkubwa kila anavyozidi kujifunza uchawi".
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na AhmadAnaeleza Mtume -Rehema amani ziwe juu yake- yakuwa atakayejifunza na akachukua katika elimu ya nyota na mashukio yake na kutumia harakati zake kama ushahidi wa matukio ya ardhini kama kifo cha mtu fulani au uhai wake au maradhi yake, na mfano wake katika yatakayotokea siku za mbeleni, basi atakuwa kajifunza sehemu ya uchwi, nakuwa kadiri mwanadamu anavyokithirisha elimu hii basi anakithirisha uchawi.
Kutoka kwa Abdillahi bin Masoud Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake yakwamba yeye amesema: "Madhambi makubwa kuliko yote: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kujiaminisha na vitimbi vya Mwenyezi Mungu, na kukata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, Na kufa moyo katika huruma za Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa na Abdul RazaaqAmetaja Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hii madhambi ambayo yanazingatiwa kuwa ni katika madhambi makubwa, nayo: ni kuwekewa Mwenyezi Mungu Mtukufu mshirika katika uumbaji wake na kuabudiwa kwake, na ameanza na hili, kwasababu ndiyo dhambi kubwa kuliko yote, na kukata matarajio na matumaini kwa Mwenyezi Mungu; kwasababu huko ni kumdhania vibaya Mwenyezi Mungu na ni kutojua upana wa rehema zake, na kujiaminisha kwa kumvuta taratibu mja kwa kumpa neema ili mpaka aje kumchukua akiwa kaghafilika, na si makusudio ya hadithi kudhibiti idadi ya madhambi makubwa kuwa hakuna zaidi ya haya yaliyotajwa, lakini makusudio yake ni kubainisha makubwa yake.