





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Masudi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Si miongoni mwetu atakayepiga mashavu, na akachana mifuko, na akaomboleza kwa maombolezo ya watu wa zama za ujinga".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmekataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- na akatahadharisha kuhusu baadhi ya vitendo vya watu zama za ujinga akasema: Si miongoni mwetu: La kwanza: Atakayepiga mashavu, na ametaja mashavu pekee kwa sababu ndio watu hufanya mara nyingi katika hilo, na vinginevyo kupiga sehemu zingine kunaingia ndani uso. La pili: Kuchana uwazi wa nguo ili aingize kichwa kwa sababu ya huzuni kubwa. La tatu: Akaomboleza kwa maombolezo ya za zama za ujinga kama kujiombea maangamivu na laana, na malalamiko, na makelele na mengineyo.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: “Amesema Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka: “Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali Ewe mwanadam lau madhambi yako yangefika mawinguni kisha ukaniomba msamaha ningekusamehe wala sijali Ewe mwanadam, lau ungenijia na thamani ya dhambi za dunia, kisha ukakutana nami bila kunishirikisha na chochote, ningekuletea msamaha ujazo sawa na ardhi".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithil Qudsi (tukufu): Ewe mwanadam, madam unaniomba na kutaraji rehema yangu, wala hujakata tamaa; Nitayasitiri madhambi yako na kuyafuta, bila kujali, hata kama madhambi na maasi haya ni katika madhambi makubwa. Ewe mwanadam! Lau madhambi yako yangekuwa mengi sana kiasi cha kuijaza nafasi ya baina ya mbingu na ardhi mpaka kiasi cha kufikia upenyo wake na kufunika pembe zake, kisha ukaniomba msamaha, basi ningekufutia na kukusamehe madhambi yote, bila kujali wingi wake. Ewe mwanadam: Lau ungenijia mimi baada ya kufa ukiwa na madhambi na maasi ujazo wa ardhi, na ukafa haliyakuwa unanipwekesha hukunishirikisha na chochote; Ningekutana na madhambi na maasi haya nikiijaza ardhi kwa msamaha; kwa sababu mimi ni mwingi wa msamaha, na ninasamehe madhambi yote isipokuwa shirki.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri, Pupia yenye manufaa na wewe, na utake msaada kwa Allah na wala usishindwe, na likikusibu jambo usiseme: Lau ningelifanya kadha basi ingelikuwa kadhaa wa kadhaa, lakini sema: Hili ni kwa makadirio ya Allah naye hufanya alitakalo, maana neno "Lau" hufungua matendo ya shetani".
Imepokelewa Imamu MuslimAnabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muumini ni mtu wa kheri maisha yake yote, lakini muumini mwenye nguvu katika imani yake na maamuzi yake na mali yake na mengineyo yenye kuendana na nguvu huyu ni bora zaidi na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko muumini dhaifu. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuusia muumini kuchukuwa sababu katika yale yenye kumnufaisha katika mambo ya Dunia na Akhera, ikiwa ni pamoja kuegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutaka msaada kwake, na kutegemea kwake. Kisha akakataza rehema na amani ziwe juu yake kuhusu kushindwa, na uvivu, na uzembe wa mtu kufanya yale yenye manufaa Duniani na Akhera. Muumini akijitahidi katika matendo, na akachukua sababu, huku akitaka msaada kwa Mwenyezi Mungu, na kwa kutaka kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi hapo hana la kufanya zaidi ya kukabidhi jambo lake lote kwa Mwenyezi Mungu, na ajue kuwa uchaguzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndio wenye kheri, ukimpata msiba baada ya hapo, basi asiseme: "Laiti ningelifanya kadha wa kadha"; "Kwani neno "Lau" Hufungua kazi ya Shetani" kuanzia kupingana na mipango ya Allah, na kuhuzunika kwa yale aliyoyakosa, bali anatakiwa aseme tena kwa kujisalimisha na kuridhika: "Ni mipango ya Mwenyezi Mungu na alitakalo hufanya", kilichotokea ni kwa mujibu wa yale aliyoyataka Mwenyezi Mungu, kwani yeye ni mfanyaji asiye na mipaka wa yale ayatakayo, na hakuna awezaye kuzuia maamuzi yake, na hakuna awezaye kuhukumu baada ya hukumu yake.
Kutoka kwa Abuu Waaqidi All-laithi radhi za Allah ziwe juu yake. Yakuwa Mtume rehema na amani zimfikie alipotoka kwenda katika vita vya Hunaini alipita katika mti wa washirikina ukiitwa: Dhata anwatwi (Mahala pa kutundika silaha) wakitundika silaha zao hapo, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tuwekee nasi mahala pa kutundikia kama ambavyo wao wana mahala pa kutundikia, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Sub-haanallaah (Ametakasika Mwenyezi Mungu)! Maneno haya ni kama yale waliyosema watu wa Mussa: "Tufanyie nasi mungu kama walivyo wao na mungu" [Al-A'raaf: 138] Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu".
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadAlitoka Mtume rehema na amani zimfikie kwenda Hunaini: Nalo ni bonde liko kati Twaif na Makka, na walikuwa pamoja naye baadhi ya Masahaba waliokuwa hawana muda mrefu tangu kuingia ndani ya Uislamu, wakapita katika mti ukiitwa: "Dhaata anwaatwi", yaani: Wenye vifaa vya kutundikia, washirikina walikuwa wakiutukuza na wakitundika hapo silaha zao na vitu vingine kwa kutaka baraka, wakaomba kutoka kwa Mtume rehema na amani zimfikie awawekee mti mfano wake, wakitundika hapo silaha zao, kwa kutafuta baraka, kwa kudhani kwao kuwa jambo hilo linafaa, Mtume rehema na amani zimfikie akamtukuza Mwenyezi Mungu kwa kukemea kauli hiyo, na kwa kumtakasa Mwenyezi Mungu, na akawaeleza kuwa kauli hii inafanana na kauli ya watu wa Mussa kwake: "Tuwekee nasi mungu kama ambavyo wao walivyo na mungu", walipowaona wenye kuabudu masanamu wakaomba nao wawe na masanamu kama washirikina walivyo na masanamu, nakuwa kitendo hiki ni katika kufuata njia yao, kisha akaeleza Mtume rehema na amani zimfikie kuwa Umma huu utafuata mfumo wa Mayahudi na Wakristo na utafanya vitendo vyao, na akatahadharisha hilo.
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi ya mambo, akasema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Umenifanya mimi kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu? sema: Akitaka Mwenyezi Mungu pekee".
Imepokelewa na Nasai katika Sunan Alkubra na Ibn Majah na AhmadAlikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani zimfikie akamsemesha kuhusu jambo lake binafsi, kisha akasema: "Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka wewe", Mtume rehema na amani zimfikie akaikemea kauli hii, na akamueleza kuwa kuunganisha matashi ya kiumbe na matashi ya Mwenyezi Mungu kwa kiunganishi "na" ni shirki ndogo, haifai kwa muislamu kuitamka, kisha akamuelekeza katika kauli ya sawa na ya haki: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake", ampwekeshe Mwenyezi Mungu katika matashi, na wala asiunganishe matashi ya yeyote kwa aina yoyote ya kiunganishi.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alingia kwangu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikiwa nimeweka pazia lenye picha kwa kusahau, alipoliona akalichana na akaghadhibika mpaka uso wake ukabadilika rangi, na akasema: "Ewe Aisha, Watu wenye adhabu kali zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, ni wale wenye kutengeneza mfano wa vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu" Aisha anasema: "Tukalichana vipande vipande vingine tukavifanya kuwa mto au mito miwili ya kulalia".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia nyumbani kwake kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake akamkuta akiwa kafunika ghala dogo ambalo huhifadhiwa humo bidhaa kwa kitambaa ambacho kina picha za viumbe hai, ikabadilika rangi ya uso wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa hasira kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akalifunua, na akasema: Watu wenye adhabu kali zaidi siku ya Kiyama ni wale wenye kufanya mfano kwa kutengeneza picha za vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu. Aisha akasema: Tukakifanya kitambaa kile kuwa ni mto mmoja au miwili.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Amesema Mwenyezi Mungu: kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na amenitukana na hakustahiki kufanya hivyo, na ama kunipinga kwake ni kauli yake: Mwenyezi Mungu hatonirudisha kuwa hai, kama alivyonianzisha, na si kuanza kuumba ni kwepesi zaidi kwangu kuliko kurudisha, na kunitukana kwake ni kauli yake: kuwa Mwenyezi Mungu kajifanyia mwana, na mimi ndiye mmoja mwenye kukusudiwa, sikuzaa wala sikuzaliwa, na wala hakuna anayefanana nami hata mmoja".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAnabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithil Qudsi yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameeleza kuhusu washirikina na makafiri kuwa wao humkanusha na humsifu kwa sifa za mapungufu na za aibu, na hawakutakiwa kufanya hivyo. Ama kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu: Ni kudai kwao kuwa Mwenyezi Mungu hatowarejesha kwa mara nyingine baada ya kufa kwao kama alivyowaumba mara ya kwanza kutoka katika kutokuwepo, akawajibu kuwa aliyeanza kuumba mwanzo anauwezo wa kuwarudisha, bali hilo ni jepesi mno, japo kuwa uhalisia kwa Mwenyezi Mungu yote ni mepesi, kuumba kwanzia mwanzo na kurudisha, kwani Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni muweza. Na ama kutukana kwao: Ni kauli yao: Kuwa yeye ana mtoto, akawajibu kuwa yeye ni wa pekee aliyepwekeka kwa ukamilifu wote katika majina yake na sifa zake na vitendo vyake, aliyetakasika na kila mapungufu na aibu, wa pekee asiyehitaji kwa yeyote, na anahitaji kwake kila mmoja, na hakuwahi kuwa mzazi wa yeyote, na hakuwahi kuwa mtoto wa yeyote, na hakuna yeyote anayefanana naye hata mmoja kwa kuwa na mfanano au mwendano, ametakasika na kutukuka.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu amesema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake, na akawa bado mja wangu anaendelea kujiweka karibu yangu kwa ibada za sunna (zisizokuwa za lazima) mpaka nitafikia mahala nitampenda, nikishampenda: Nitakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analotazamia, na mkono wake anaoshikia, na mguu wake anaotembelea, na hata akiniomba hakika nitampa, na hata akinitaka kinga hakika nitamlinda, na sijawahi kusita katika jambo lolote ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika (kuitoa) nafsi ya muumini, hapendi kufa na mimi sipendi kumuudhi".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithil Qudsi yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Atakayemuudhi kipenzi miongoni mwa vipenzi vyangu na akamkasirisha na akambughudhi basi nitakuwa nimemtangazia uadui. Na walii (Kipenzi) ni: Muumini mchamungu, na kwa kadiri imani na uchamungu wa mja unavyokuwa ndivyo nafasi yake ya ukaribu inavyokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na hajawahi muislamu kujiweka karibu kwa Mola wake kwa jambo alipendalo zaidi kuliko lile alilomfaradhishia na akamuwajibishia juu yake, ikiwemo kufanya mambo yote ya utiifu, na kuacha maharamisho, na kwa kadiri anavyoendelea muislamu kujikurubisha kwa Mola wake kwa yale ya sunna pamoja na faradhi; mpaka atapata mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akimpenda, atakuwa akimtimizia mambo yake katika viungo hivi vinne: Atampa umakini katika kusikia kwake, hatosikia ila yale yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu. Na humpa umakinifu katika macho yake, hatotazama ila yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu kuyatazama na anayaridhia. Na anampa umakinifu katika mkono wake, hatofanya kwa mkono wake ila yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu. Na anampa umakinifu katika mguu wake, hatokwenda ila katika yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu, na wala hatoyaendea ila yale yenye kheri ndani yake. Pamoja na haya yote, akimuomba Mwenyezi Mungu chochote basi Mwenyezi Mungu humpa alichoomba, anakuwa ni mtu mwenye kujibiwa maombi, na ikiwa atataka hifadhi kwa Mwenyezi Mungu na akaomba ulinzi kwake kwa kutaka hifadhi, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu humkinga dhidi ya yale anayoyahofu. Kisha akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na sijawahi kusita katika jambo ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika kuichukua nafsi ya muumini, kwa kumhurumia; kwa sababu yeye anachukia kifo kwa kuwa ndani yake kuna maumivu, na Mwenyezi Mungu hapendi yanayomuudhi muumini.
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri: Kutiana doa katika nasaba (ukoo), na kulia kwa kumuomboleza maiti".
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mambo mawili kwa watu kuwa ni katika matendo ya makafiri, na ni tabia za enzi za ujinga, nayo ni: La kwanza: Kutukana nasaba (koo) za watu na kuzishushia heshima na kujikweza juu yao. La pili: Kunyanyua sauti wakati wa msiba kwa kulalamika juu ya kadari, au kukata nguo kwa sababu ya mfadhaiko mkubwa.