





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa".
Imepokelewa na Ibnu Maajah, Al-Bayhaqi na wengineoAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kwamba Mwenyezi Mungu ameusamehe umma wake katika hali tatu: La kwanza: Kukosea, nayo ni yale yanayotokea kwao pasina kukusudia, nayo ni muislamu kukusudia kufanya jambo lolote, kisha kitendo chake kikakutana na jambo ambalo hakulikusudia. La pili: Kusahau, nako ni muislamu kuwa na kumbukumbu ya kitu, lakini akakisahau wakati wa kufanya, hana madhambi katika hilo pia. La tatu: Kulazimishwa, mja anaweza kulazimishwa kufanya kitu ambacho hakitaki pamoja na kutoweza kuzuia kulazimishwa, na hapo pia hatopata dhambi au ubaya. Pamoja na tahadhari kuwa maudhui ya hadithi ni katika yale yalio baina ya mja na Mola wake katika kufanya maharamisho, ama kuacha maamrisho kwa kusahau hapa haiondoki, na ama kitendo chake kikiambatana na kosa la jinai hii pia haiondoki katika haki ya kiumbe, kama akiua kimakosa, atatakiwa kutoa fidia, au akaharibu gari kwa makosa atawajibika kulipa.
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alifariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hali yakuwa hakuna chochote nyumbani kwake anachoweza kukila mwenye ini (uhai) ila kiasi kidogo cha ngano kilichokuwa katika ubao wangu (wa kuhifadhia chakula), nikala mpaka kikakaa muda mrefu, nilipokipima kikamalizika
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAnaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alifariki hali yakuwa hakuna nyumbani kwake chochote isipokuwa kiasi kidogo cha ngano, na maana yake ni kiwango kidogo cha ngano, kama alivyoifasiri imamu Tirmidhiy, akaendelea kula katika chakula alichokiacha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa muda mrefu, alipokipima kikamalizika, na hii ni ishara ya kuendelea kwa baraka zake -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chakula hicho kidogo, pamoja na kutokuwepo kwa kipimo kinachoonyesha kiasi wakati wa kumtegemea Mwenyezi Mungu, kipimo wakati wa kuuziana kinahitajika kwaajili ya kuweka sawa haki ya wale wenye kuuziana, ama kipimo wakati wa kutoa sadaka haipendezi (si katika sunna).
Kutoka kwa Swafwan bin Muhrizi amesema: Mtu mmoja alisema kumwambia bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao, ulimsikia akisema nini Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu kunong'ona? Akasema: nilimsikia akisema: "Atasogezwa muumini siku ya Kiyama karibu na Mola wake Mlezi Aliyetakasika na Kutukuka, kisha atamuwekea pazia lake, hapo atamuonyesha wazi madhambi yake ili akiri, kisha atasema: Je wayajua? Atasema: Ndiyo Mola wangu ninayajua, atasema: Basi hakika mimi nilikusitiri madhambi haya ulipokuwa duniani, na mimi ninakusamehe madhambi hayo leo hii, hapo atapewa faili la mema yake, na ama makafiri na wanafiki, wataitwa hadharani mbele ya kadamnasi, (kisha patasemwa) hawa ndio waliompinga Mwenyezi Mungu"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Mwenyezi Mungu kunong'ona na mja wake muumini siku ya Kiyama, akasema: Atasogezwa muumini siku ya Kiyama karibu na Mola wake Mlezi kisha atamuwekea pazia lake la kumkinga na watu walioko katika kisimamo, hakuna atakayeona katika pazia hilo zaidi yake, hapo atamwambia: Je walijua dhambi fulani na fulani... atamtaka akiri madhambi yake yaliyokuwa kati ya mja na Mola wake Mlezi. Naye atasema: Ndiyo, ewe Mola Mlezi. Mpaka atakapofadhaika muumini na kuogopa, Mtukufu atamwambia: Mimi niliyasitiri kwako madhambi haya duniani, na mimi leo hii ninayasamehe kwa ajili yako, hapo atapewa faili la mema yake. Na ama kafiri na mnafiki wataitwa mbele ya kadamnasi: Hawa ndiyo waliomkadhibisha Mola wao Mlezi, basi tambueni kuwa laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya madhalimu.
Kutoka kwa Muadhi bin Jabali -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, nikajikuta siku moja niko karibu naye tukiwa tunatembea, nikasema: Ewe Mtume wa Allah nieleze ibada ambayo nikiifanya itaniingiza peponi, na itaniweka mbali na moto, akamjibu: "Umeniuliza kuhusu jambo kubwa, lakini nijepesi kwa yule atakayefanyiwa wepesi na Mwenyezi Mungu Mtukufu: ni kumuabudu Mwenyezi Mungu bila kumshirikisha na chochote, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kuhiji. kisha akasema Mtume: Je, nikujulishe milango ya kheri? Funga ni kinga, na sadaka inaondosha madhambi kama maji yanavyo uzima moto, na swala ya mtu katikati ya usiku, kisha akasoma kauli ya Mwenyezi Mungu: "Mbavu zao zinaachana na vitanda..." mpaka alipo fikia mwisho wa aya "wanao jua". Kisha akasema Mtume: Je nikueleze kichwa cha mambo yote na nguzo yake na kilele chake? nikajibu ndio ewe mjumbe wa Allah, akasema: Kichwa cha mambo yote ni Uislam, na nguzo yake ni Swala, na kilele chake ni Jihadi. kisha akasema: Je nikujulishe kinacho yahifadhi na kuyatunza matendo hayo? nikasema ndio ewe Mtume wa Allah, akaushika ulimi wake kisha akasema: uzuwie ulimi wako, nikamuuliza: Ewe Mtume wa Allah je tutahesabiwa kwa kila tunacho kizungumza? Akasema: akukose mamako, hakuna kitakacho waingiza watu wengi motoni kama chumo za ndimi zao".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadAmesema Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, siku moja nikawa karibu naye tukiwa tunatembea, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nieleze amali itakayoniingiza Peponi na kuniweka mbali na moto, akasema: Bila shaka umeuliza kuhusu jambo kubwa kulifanya kwake katika nafsi, na bila shaka ni jepesi na ni rahisi mno kwa atakayerahisishiwa na Mwenyezi Mungu kulifanya; tekeleza faradhi za Uislamu; Ya kwanza: Umuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na wala usimshirikishe na chochote. Ya pili: Usimamishe swala tano za faradhi mchana na usiku: Alfajiri, Adhuhuri, Alasiri, Magharibi, Ishaa, kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake. Ya tatu: Utoe zaka ya wajibu, nayo ni ibada ya mali ya wajibu kwa kila mali iliyofikia kiwango katika sheria, na wanapewa wastahiki wake. Ya nne: Ufunge mwezi wa Ramadhani, nako ni kujizuia na kula na kunywa na mengineyo katika mambo yenye kufunguza kwa nia ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuzama kwa Jua. Ya tano: Utaizuru nyumba kwa kwenda Makka ili kutimiza ibada, kwa lengo la kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Je nikufahamishe kuhusu njia inayokufikisha katika milango ya heri? Nayo ni kwa kutekeleza faradhi na sunna hizo: Ya kwanza: Ni funga ya hiyari, nayo inamzuia mtu kuingia katika maasi, nayo ni kwa kuvunjavunja matamanio, na kuzidhoofisha nguvu. Ya pili: Sadaka ya kujitolea inazima madhambi baada ya kuyafanya na huyaondosha na kufuta athari zake. Ya tatu: Swala ya tahajudi katika theluthi ya mwisho ya usiku, kisha akasoma rehema na amani ziwe juu yake kauli yake Mtukufu: "Hunyanyuka mbavu zao" Yaani: Hujiweka mbali, na "malazi" Yaani: Mahali pa kulala, "wakimuomba Mola wao Mlezi" Yaani: kwa swala na dhikri na kusoma Qur'ani na dua, "kwa hofu na tamaa, na katika yale tuliyowaruzuku wanatoa, hakuna nafsi ijuayo yale waliyofichiwa, katika yale yenye kutuliza macho" Yaani: Yale yenye kutuliza macho yao siku ya Kiyama na katika pepo miongoni mwa neema, "ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyafanya". Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hivi nikueleze msingi wa dini? na nguzo yake inayosimamia? na kiini cha kilele chake? Akasema Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake: Ndio, nieleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kichwa cha mambo yote ni: Uislamu nao ni shahada mbili, na kwa shahada hizi mbili ndio mtu anapata msingi wa dini. Na nguzo yake: Ni swala, hakuna Uislamu bila swala, kama ambavyo nyumba haiwezi kusimama pasina nguzo, atakaye swali dini yake itakuwa na nguvu na itanyanyuka; Na kiini cha kilele chake na kimo chake ni Jihadi na kutoa juhudi katika kupambana na maadui wa dini ili kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu. Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hivi nikuelezeni umadhubuti na ufanisi wa yaliyopita? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akashika ulimi, na akasema: Zuia huu na wala usizungumze yale yasiyokuhusu. Akasema Muadhi: Je atatuchukulia makosa na kutuhesabu Mola wetu Mlezi na kutuadhibu kwa kila tunachozungumza?! Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Amekupoteza mama yako! Na makusudio yake si kumuombea dua mbaya, bali ni katika maneno ya waarabu yaliyokuwa yakitumika kumtanabahisha mtu kuwa jambo hili unatakiwa kulichukulia tahadhari kubwa na kulielewa, kisha akasema; na unadhani ni kipi kitawatupa watu na kuwadondosha kwa nyuso zao ndani ya moto zaidi ya chumo za ndimi zao, ikiwemo ukafiri na kumzulia mtu machafu na matusi na utesi na usengenyaji, na uongo na mfano wa hayo.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii, akasema Allah Mtukufu: "Enyi Mitume! Kuleni katika vile vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" [Al-Muuminuun: 51] Na akasema Allah Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kuleni katika vizuri miongoni mwa vile tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa kweli nyinyi mnamuabudu yeye peke yake" [Al-baqara: 172] akasema: Kisha akataja tukio la mtu mmoja mwenye safari ndefu, nywele zake zimetimka, kajaa vumbi, ananyanyua mikono yake kuelekea mbinguni (anasema) Mola wangu Mola wangu! (wakati huo) chakula chake ni cha haramu, na mavazi yake ni ya haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na lishe yake yote ni ya haramu, itawezekana vipi kujibiwa kwa mtu kama huyo?!".
Imepokelewa Imamu MuslimAlieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu ni mzuri na ni mtakasifu ametakasika na kila mapungufu na aibu na amesifika kwa yote yaliyokamilika, na wala hakubali katika matendo kauli na itikadi isipokuwa ile itakayokuwa nzuri, nayo ni ile iliyotakaswa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, yenye kwenda sambamba na muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na haitakiwi mtu ajikurubishe kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa hayo, na katika mambo yanayosababisha amali kuwa nzuri kwa muumini ni chakula chake kuwa kizuri, na kiwe kimetokana na halali, kwa hilo amali zake zinakuwa njema, na ndio maana Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waumini kwa lile alilowaamrisha Mitume, ikiwemo kula halali na kutenda mema, akasema: "Enyi Mitume! Kuleni katika vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" Na akasema: "Enyi mlioamini kuleni katika vizuri katika vile tulivyokuruzukuni". Kisha akatahadharisha rehema na amani ziwe juu yake kula haramu,ambako kunaharibu matendo na kunazuia kukubalika kwake kwa sababu yoyote ile inayoonekana; ikiwemo: Ya kwanza: Kuwa na safari ndefu iliyo katika misingi ya kumtii Mwenyezi Mungu kama Hija na Jihadi na kuunga udugu na mengineyo. Ya pili: Nywele kukaa hovyo kwa kutotanwa, na kubadilika rangi ya ngozi na rangi ya nguo kwa sababu ya udongo, basi mtu huyu anakuwa kadharurika. Ya tatu: Ananyanyua mikono yake juu mbinguni kwa dua. Ya nne: Anamuomba Mwenyezi Mungu kupitia majina yake na anang'ang'ania katika hilo: Ewe Mola wangu Ewe Mola wangu! Na pamoja na sababu hizi za kujibiwa dua hakusikilizwa; na hii ni kwa sababu chakula chake na kinywaji chake na mavazi yake ni vya haramu, na afya yake imetokana na haramu, ni mbali sana kwa mtu mwenye sifa kama hizi kujibiwa, na atajibiwa vipi?!
Kutoka kwa Mikidadi bin Amri Al-Kindi radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba yeye alisema kumuuliza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Unaonaje ikiwa nitakutana na mtu miongoni mwa makafiri, tukapigana, akapiga moja ya mikono yangu kwa upanga akaukata, kisha akajificha katika mti, akasema: Nimejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, je nimuue ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu baada ya kuwa amelisema neno hilo? Akasema: "Usimuue" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kakata moja ya mikono yangu, Kisha akasema hivyo baada ya kuwa kaukata?! Akasema: "Usimuue, kwani ukimuuua basi yeye atakuwa katika nafasi yako kabla hujamuua, na wewe utakuwa katika nafasi yake kabla hajasema neno lake alilolisema".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMikidadi bin Aswadi radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi atakapokutana na mtu miongoni mwa makafiri katika mapambano, wakapambana kwa mapanga, mpaka yule kafiri akakata mmoja kati ya mikono yake kwa upanga, kisha kafiri akamkimbia na akajikinga katika mti, akasema: Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, je, ni halali kwangu kumuua baada yakuwa amekata mkono wangu? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Hapana, usimuuwe. Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lakini yeye kakata moja ya mikono yangu, pamoja na hivyo bado tu nisimuuwe?! Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hapana, usimuuwe, kwa sababu tayari damu yake ishakuwa haramu, kwa sababu ikiwa utamuua baada ya kusilimu kwake; basi hakika yeye atakuwa katika nafasi yako ya kulindwa damu kwa Uislamu wake, na wewe utakuwa katika nafasi yake, itakuwa halali damu yako kwa kukuua kwa kisasi kwa sababu ya kumuuwa.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Barza Al Aslamia -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hautonyanyuka unyayo wa mja siku ya Kiyama mpaka aulizwe kuhusu umri wake aliumaliza katika mambo yapi? Na kuhusu elimu yake aliifanyia kazi katika nini? Na kuhusu mali yake ni wapi aliichuma? Na aliitoa katika mambo gani? Na kuhusu mwili wake aliumaliza katika mambo yapi?"
Imepokelewa Imamu TirmidhiyAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa hatovuka mtu yeyote kisimamo cha hesabu siku ya Kiyama kwenda peponi au motoni mpaka aulizwe kuhusu mambo kadhaa: La kwanza: Maisha yake aliyatumia na kuyamaliza katika nini? La pili: Elimu yake, je aliitafuta kwa lengo la kupata radhi za Allah? na je aliifanyia kazi? na je aliifikisha kwa wenye kustahiki? La tatu: Mali yake ni wapi aliichuma, je ni katika halali au haramu? Na aliitoa katika mambo gani, ni katika yale yenye kumridhisha Allah au yenye kumchukiza?. La nne: Mwili wake na nguvu zake na afya yake na ujana wake, aliutumia na kuumaliza katika mambo gani?
Imesimuliwa kutoka kwa Abuu Huraira, Mwenyezi Mungu amridhie, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake, alisema siku ya (vita vya) Khaibar: "Hakika nitampa bendera hii mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Mwenyezi Mungu ataleta ufunguzi kupitia mikono yake". Akasema Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- sikuwa napenda uongozi wakati huo, fikra zikanipelekea kuwa na matarajio ya kuitwa kwa ajili ya bendera hiyo, akamuita Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Ally bin Abii Twalib -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akampa bendera hiyo, na akasema: "Nenda na usigeuke mpaka Mwenyezi Mungu akufungulie" Akatembea Ally mwendo kidogo kisha akasimama na wala hakugeuka kisha akazungumza kwa sauti ya juu: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa lipi niwapige watu? Akasema: "Pigana nao mpaka washuhudie kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wakifanya hivyo watakuwa wamekinga kwako damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki yake, na hesabu yao iko juu ya Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa Imamu MuslimAliwaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba kuhusu ushindi wa waislamu kesho dhidi ya Mayahudi wa mji wa Khaibar ambao ni mji uko karibu na Madina, na hii ni kupitia mkono wa mtu atakayempa bendera, nayo ni bendera inayofanywa na jeshi kama nembo, na mtu huyu miongoni mwa sifa zake nikuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda pia. Na alieleza Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake kuwa hapendi uongozi na hapendi kuwa yeye ndiye anayelengwa isipokuwa kwa siku hiyo; kwa kutaraji yampate aliyoyasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Omari akanyanyua mwili wake ili auone Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kutaraji kuwa anaweza kuitwa kwa ajili ya hilo, na akiwa na pupa na tamaa ya kuchukua bendera hiyo. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuita Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake akampa bendera, na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaamrisha jeshi litembee, na lisiondoke katika vita baada ya kukutana na maadui sawa iwe ni kwa mapumziko au kwa kusitisha au kutuliza vita, mpaka Mwenyezi Mungu amfungulie ngome hizi kwa ufunguzi na ushindi. Akatembea Ally radhi za Allah ziwe juu yake, kisha akasimama isipokuwa hakugeuka; ili asiende kinyume na amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi Ally radhi za Allah ziwe juu yake akanyanyua sauti yake: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nipigane na watu kwa lipi?. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Pigana nao mpaka washuhudie kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ikiwa watalikubali hilo, na wakaingia ndani ya Uislamu; watakuwa wamezizuia kwako damu zao na mali zao, na zitakuwa haramu kwako, isipokuwa kwa haki yake, yaani: Isipokuwa kama watafanya uhalifu au kosa la jinai watakalostahiki kuuawa kwa kosa hilo kwa mujibu wa hukumu za Uislamu, na hesabu yao itakuwa kwa Mwenyezi Mungu.
kutoka kwa Nu'man Bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake -: "Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na kufanyiana kwao upole, ni kama mfano wa kiwiliwili, kinapopata tabu kiungo kimoja vinaitana kwa ajili ya hicho kimoja viungo vyote kwa kukesha na maumivu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa inatakiwa kuwa hali ya waislamu baadhi yao kwa baadhi katika kupendeleana kheri na kuhurumiana na kusaidizana na kuteteana, na kuudhika kwa yale madhara yanayowafika, kama mfano wa kiwiliwili kimoja, kikiugua kiungo kimoja, mwili mzima unashiriki kwa kukesha na maumivu pia.