





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Je mnajua ni nani aliyefilisika?" Wakasema: Aliyefilisika kwetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yule asiye na Dirham (pesa) wala mali yoyote. Akasema: "Hakika aliyefilisika katika umma wangu ni yule atakayekuja siku ya Kiyama akiwa na (ibada za) swaumu na swala na zaka, na akaja akiwa kamtukana huyu, na kamzulia machafu huyu, na kala mali ya huyu, na amemwaga damu ya huyu na amempiga huyu, hivyo atapunguziwa huyu kutoka katika mema yake, na huyu katika mema yake, yakimalizika mema yake kabla hajamaliza kulipa anayodaiwa yatachukuliwa kutoka katika makosa yao yatatupwa kwake kisha atatupwa katika moto".
Imepokelewa Imamu MuslimMtume rehema na amani ziwe juu yake aliwauliza Maswahaba zake: Je, mnamjua aliyefilisika? Wakasema: Aliyefilisika miongoni mwetu ni yule asiye na fedha wala mali. Akasema: Aliyefilisika katika umma wangu Siku ya Kiyama ni yule anayefanya mambo mema kama Swala, Saumu na Zaka, na akaja akiwa kamshutumu huyu na kamtukana huyu, na kamsingizia mabaya mtu huyu katika heshima yake, na kala mali ya huyu na akakana, na akamwaga damu ya huyu na kumdhulumu, na kampiga huyu na akamdhalilisha, hivyo mtu aliyedhulumiwa atapewa kutoka katika matendo yake mema, mema yake yakimalizika kabla ya haki za watu na dhulma hazijamalizika, yatachukuliwa madhambi ya wale aliowadhulumu na kuwekwa katika vitabu vya dhalimu, kisha atatupwa na kurushwa motoni kwani hajabaki na jema.
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna mwenye kumiliki dhahabu wala fedha, na akawa hazitolei zaka zake, isipokuwa, pindi itakapofika siku ya Kiyama, atakunjiwa Sahani la kutoka motoni, basi litachemshwa katika moto wa Jahanam, kisha zitapigwa pasi mbavu zake na paji lake la uso na mgongo wake, kila linapopoa linarejeshewa umoto, katika siku ambayo makadirio yake yatakuwa ni miaka elfu hamsini, (atadumu katika adhabu hiyo) mpaka watu watakapohukumiwa, naye akaona njia yake, ima inakwenda peponi, na ima anakwenda motoni" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, vipi kuhusu Ngamia? Akasema: "Wala mmiliki wa Ngamia asiyetekeleza haki yake, na miongoni mwa haki zake ni kuwakamua siku wanapotoka manyweshoni, isipokuwa (asipofanya hivyo) itakapofika siku ya Kiyama atalazwa kifudifudi katika eneo tambarare lenye kina kirefu kisha wataletwa wanyama wake kwa wingi zaidi ya jinsi walivyokuwa duniani, hatokosekana hata ndama mmoja, kisha wataanza kumkanyaga kwa kwato zao, na watakuwa wakimng'ata kwa midomo yao, kila anapopita wa mwanzo wao anarejeshwa mpaka wa mwisho wao, na (adhabu hii ataendelea nayo) katika siku ambayo makadirio yake yatakuwa ni miaka elfu hamsini, mpaka watu watakapohukumiwa, naye akaona njia yake ima anakwenda peponi au anakwenda motoni" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Vipi kuhusu Ng'ombe na Mbuzi? Akasema: "Wala mmiliki wa Ng'ombe na Mbuzi, asiyetekeleza haki zake, isipokuwa itakapofika siku ya Kiyama atalazwa chini katika Ardhi tambarare yenye kina, hakuna mnyama yeyote atakayekosekana, na hakuna aliyepinda pembe wala aliyejeruhiwa, wala aliyekatika pembe watakuwa wakimchoma kwa pembe zao na wakimkanyaga kwa kwato zao, kila akimpitia wa mwanzo wake, anarejeshwa wa mwisho wao, atabaki hivyo mpaka watakapohukumiwa waja, na hapo ataona njia yake, ima anakwenda peponi, na ima anakwenda motoni". Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, vipi kuhusu Farasi? Akasema: "Farasi wana aina tatu: Wapo ambao ni mzigo kwa mtu, na wapo wanaomsitiri mtu, na wapo wanaomuingizia malipo mtu, ama ambao ni mzigo kwa mtu ni mtu aliyewafunga kwa kujionyesha na kutaka ufahari kwa watu, na ama kuhusu wale ambao ni stara kwake ni wale ambao mtu amewafunga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi hakusahau haki ya Mwenyezi Mungu katika migongo yao wala shingo zao, Farasi hao kwake ni kinga na ni stara, ama ambao kwake ni malipo, ni mtu aliyewafunga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya waislamu, katika malisho na viuga, isipokuwa ataandikiwa malipo ambayo idadi yake itakwenda sawa na idadi watakayokula Farasi hao, na wala hayatokatwa manyoa yake kisha yakastawi vizuri au vizuri zaidi isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuandikia mema kwa idadi ya athari zake na kinyesi chake, na wala mmiliki huyo hatowapitisha mtoni wakanywa katika mto huo, hata kama hakukusudia kuwapeleka manyweshoni, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuandikia mema kwa idadi watakayokunywa hapo"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume rehema na amani ziwe juu yake amebainisha makundi ya mali, na malipo ya mtu ambaye hatotekeleza zaka yake siku ya Kiyama, na miongoni mwake: Ya kwanza: Dhahabu na fedha na vyote vilivyo katika hukumu ya hivyo miongoni mwa mali na bidhaa za biashara, nazo ni zile za wajibu ndani yake kutolewa zaka ikawa hazikutekelezwa, itakapofika siku ya Kiyama zitayeyushwa na kumiminwa na kutengenezwa katika umbile la sahani, na zitawashwa na kuchemshwa katika moto wa Jahannam, na ataadhibiwa nazo mwenye nazo, zitapigwa pasi kwazo mbavu zake na paji lake la uso na mgongo wake, kila ikipoa inachemshwa tena, na ataendelea katika hali hii ya adhabu kwa muda wote wa siku ya Kiyama ambao makadirio ya siku yake ni siku elfu hamsini, mpaka Mwenyezi Mungu atakapohumu kati ya viumbe, hapo ima awe ni katika watu wa peponi au watu wa motoni. Wa pili: Ni mmiliki wa ngamia ambaye hatekelezi faradhi ya zaka zake na haki zake, ikiwemo kuwakamua na kumpatia maziwa anayehudhuria wakati wa kukamua miongoni mwa masikini, wataletwa ngamia hawa wakiwa wakubwa tena walionenepa, na wakiwa wengi kwa idadi zaidi ya jinsi walivyokuwa, na mmiliki wake atatupwa na kulazwa chini na kunyooshwa vizuri siku ya Kiyama katika Ardhi pana ya tambarare, watakuwa wakimkanyaga kwa miguu yao na wakimng'ata kwa meno yao, kila akipita wa mwisho wao, anarejeshwa wa mwanzo wao, na ataendelea katika hali hii ya adhabu kwa muda wote wa siku ya Kiyama ambayo kiasi chake ni siku elfu hamsini, mpaka Mwenyezi Mungu atakapohukumu baina ya viumbe, na hapo atakuwa ni miongoni mwa watu wa peponi au watu wa motoni. Wa tatu: Ni mmiliki wa ng'ombe na mbuzi -ikiwemo kondoo- ambazo mmiliki wake hatekelezi zaka yake ya faradhi, zitaletwa zikiwa kamili kwa wingi zaidi ya jinsi zilivyokuwa, hakuna mnyama atakayepungua, atanyooshwa vizuri na kutupwa na atalazwa huyo mmiliki wake siku ya Kiyama katika Ardhi pana ya tambarare, hakuna mnyama atakayekuwa na pembe zilizopinda, wala asiyekuwa na pembe, wala aliyevunjika pembe, bali watakuwa katika maumbile yao kamili, watakuwa wakimchoma kwa pembe zao, na wakimkanyaga kwa miguu yao, kila akipita wa mwisho wao anarejeshwa wa mwanzo wao, Na ataendelea kuwa katika hali hii ya adhabu kwa muda wote wa siku ya Kiyama ambayo kiasi chake ni miaka elfu hamsini, mpaka Mwenyezi Mungu atakapohukumu baina ya viumbe, na hapo atakuwa miongoni mwa watu wa peponi au watu wa motoni Ya nne: Mfugaji wa Farasi, naye ana aina tatu: Aina ya kwanza: Ni farasi ambao ni mzigo, nao ni wale ambao mtu kawafuga kwa lengo la kutaka kuonekana kwa watu, na kujifaharisha na kwa lengo la kuwapiga vita waislamu. Aina ya pili: Ambao kwake ni stara, nao ni wale ambao mtu kawaandaa kwa ajili ya kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha akawapa matunzo, akasimamia malisho yake na mahitaji yake mengine, ikiwemo kuyaachia madume haki yake. Aina ya tatu: Ambao kwake ni malipo, nao ni wale ambao mtu kawafuga kwa ajili ya kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya waislamu, akawaweka katika uwanja wa malisho kwa ajili ya chakula, hakuna watakachokula hapo isipokuwa ataandikiwa mema kwa idadi ya kile walichokula, na ataandikiwa mema kwa kila kinyesi chao na mikojo yao, na wala hawatokata kamba yao wanayofungwa nayo, wakakimbia na kutimka mbio katika maeneo yenye miinuko katika Ardhi, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuandikia mema kwa kila athari (alama) ya unyayo na kinyesi chao, na wala mmiliki wake hatowapitisha katika mto wakanywa katika mto huo, hata kama hakukusudia kuwanywesha isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuandikia mema kwa idadi ya fundo walizokunywa. Kisha akaulizwa rehema na amani ziwe juu yake kuhusu punda wa mjini je naye mtu atampatia malipo mfano wa farasi? Akasema kuwa: Haijateremshwa sheria yoyote kuhusu hilo isipokuwa aya hizi chache kimtazamo, ambazo zinakusanya kila aina ya ibada na maasi; nayo ni kauli yake Mtukufu: "Basi yeyote atakayefanya uzito wa chembe ndogo jema basi ataliona, na yeyote atakayefanya uzani wa chembe ndogo jambo baya basi ataliona". [Azzalza: 8], atakayefanya jambo jema katika ufugaji wa punda basi naye thawabu za hilo ataziona, na endapo atafanya maasi basi ataiona adhabu yake, na hii inajumuisha amali zote.
Kutoka kwa Ka'bu bin Hatim -radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ataongeleshwa na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama bila ya kuwapo na mkalimani yeyote kati yake na Yeye (Allah). Atatazama kuliani kwake, na wala hataona kitu chochote isipokuwa matendo yake aliyotanguliza. Kisha ataangalia kushotoni kwake, na wala hataona kitu chochote isipokuwa matendo yake aliyotanguliza. Na ataangalia mbele yake, na hataona isipokuwa Moto mbele ya uso wake. Basi uepukeni Moto hata kama ni kwa nusu ya tende."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlieleza Mtume rehema amani ziwe juu yake kuwa kila Muumini atasimama mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama peke yake, na kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atazungumza naye bila ya muwakilishi, na hakuna mkalimani baina yao wa kutafsiri maneno, hivyo atatazama kulia na kushoto kutokana na hofu kali, labda atapata njia ya kwenda ili aweze kuokolewa na moto uliombele yake. Akitazama upande ulioko kuliani kwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza katika matendo mema, na akitazama kushotoni kwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza katika matendo mabaya, na akitazama mbele yake hatoona isipokuwa moto, na hatoweza kuukwepa, kwani hakuna budi ni lazima apite juu daraja (Swirat). Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Wekeni kinga kati yenu na moto, kama kutoa sadaka na matendo mema, walau kwa kitu kidogo kama nusu ya tende.
Kutoka kwa Ukba Bin Aamir Al Juhaniy -Radhi za Allah ziwe juu yake: Yakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake lilikuja kwake kundi, akawaunga mkono watu tisa na akamuacha mmoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, umewaunga mkono watu tisa na ukamuacha huyu? akasema: "Huyo yuko na hirizi", akaingiza mkono wake akaikata, akamuunga mkono, akasema: "Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina"
Imepokelewa na AhmadWalikuja watu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na idadi yao walikuwa kumi, akawaunga mkono tisa miongoni mwao juu ya Uislamu na kufuata sheria, na hakumuunga mkono wa kumi, alipoulizwa kuhusu sababu yake, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Huyo kavaa hirizi, nayo ni kila kinachotundikwa, ikiwemo shanga na vinginevyo kwa lengo la kuzuia kijicho au madhara. Yule bwana akaingiza mkono wake mahali ilipo hirizi na akaikata na akaepukana nayo, hapo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuunga mkono, na akasema akitahadharisha kuhusu hirizi na akibainisha hukumu yake: "Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya shirki".
Kutoka kwa Abdallahi bin Amru bin A'swi -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake: Kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, yakwamba yeye alikuwa anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa uso wake mkarimu, na kwa mamlaka yake ya tangu, kutokana na shetani aliyelaaniwa" Akasema: Hivyo tu? Nikasema ndiyo. Akasema: Mtu anaposema hivyo shetani husema: Huyu kalindwa nami siku yake nzima.
Imepokelewa na Abu DaudAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu" Yaani: Ninashikamana na kuegemea kwa Mwenyezi Mungu na sifa zake. "Na kwa uso wake Mkarimu" Yaani: Mkarim mtoaji, "Na kwa mamlaka yake) Yaani: Ushindi wake na uweza wake kwa amtakaye katika viumbe wake "Wa tangu" Yaani: Wa zamani na wa milele. "Kutokana na Shetani aliyelaaniwa" Yaani: Aliyetengwa na kufukuzwa kutoka katika rehema ya Mwenyezi Mungu, yaani: Ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi kutokana na wasi wasi wake na upotoshaji wake na hatua zake na hatari zake, na udanganyifu wake na upotoshaji wake, kwani yeye ndiye sababu ya upotofu, na ndio mchochezi wa upotofu na ujinga, akaulizwa Abdillah bin Amri "Hivyo tu" Yaani: Je, alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni hivyo tu? Akasema: Ndio. Atakaposema dua hii mwenye kuingia msikitini; Shetani husema: Muingiaji kaihifadhi nafsi yake dhidi yangu wakati wake wote, mchana wake na usiku wake.
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: “Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na Kutukuka, atawaambia watu wa Peponi: Enyi watu wa Peponi? Watasema: Labeka tumekuitikia na umetukuka, atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Tuna nini mpaka tusiridhike hali yakuwa umetupa mambo ambayo hujampa yeyote katika viumbe wako? Atasema: Mimi nitakupeni kilicho bora zaidi kuliko hilo, Watasema: Ewe Mola Mlezi, ni kitu gani kilicho bora kuliko hili? Atasema: Ninawapeni radhi zangu, wala sitowachukia baada yake milele".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Peponi wakiwa humo: Enyi watu wa Peponi, nao watamjibu kwa kusema: Labeka, tumekuitikia Mola wetu Mlezi! na utukufu ni wako, Atasema kuwaambia: Je! mmeridhika? Watasema: Ndiyo, tumeridhika; Kwa nini tusiridhike wakati umetupa ambacho hukumpa kiumbe wako yeyote! Atasema Mtukufu: Je, nisikupeni kilicho bora kuliko hicho? Watasema: Ewe Mola Mlezi, na ni kitu gani kilicho bora kuliko hicho? Atasema: Ninakuteremshieni juu yenu radhi zangu daima; na sitokukasirikieni baada yake milele.
Kutoka kwa Abuu Dharri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hatomtuhumu mtu mwenzake kwa machafu, na wala hatomtuhumu kwa ukafiri, isipokuwa hurejea kwake, ikiwa ndugu yake hatokuwa hivyo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema kumwambia mwingine: Wewe ni muovu, au: Wewe ni kafiri, ikiwa hatokuwa kama alivyosema, basi yeye ndiye atakayestahiki sifa iliyotajwa, na kauli yake itarudi kwake, na ama akiwa kama alivyosema basi hakuna kitakachorejea kwake; kwa sababu atakuwa mkweli katika hayo aliyoyasema.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawaingii Malaika nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika wa rehema hawaingii nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa au picha za viumbe hai; Hii ni kwa sababu sura ya kitu ambacho kina roho ni dhambi kubwa, na kuna uigaji wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, na ni njia katika njia za ushirikina, na baadhi yake ni picha ya vile vinavyoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu. Ama sababu ya kujiepusha na nyumba ambayo ndani yake kuna mbwa; ni kwa sababu anakula uchafu mwingi, na ni kwa sababu baadhi mbwa huitwa mashetani; Na malaika wako dhidi ya mashetani. Na kwa sababu ya harufu mbaya ya mbwa; Malaika wanachukia harufu mbaya, na kwa sababu ni haramu kuwafuga; Hivyo mwenye kuwafuga akaadhibiwa kwa kunyimwa Malaika kuingia nyumbani kwake, na kuswali humo, na kumuombea msamaha, kumbariki yeye na nyumba yake, na kumzuilia udhia wa Shetani.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawafuatani Malaika na jamaa ambao ndani yao kuna mbwa au kengele".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika hawafuatani na msafara katika safari, na ndani ya msafara kuna mbwa, au kengele inayotundikwa kwa wanyama ikitoa sauti mnyama anapotembea.