





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abdillahi bin zaidi bin A'swim Al-maaziniy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "paliletwa mashtaka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu mtu anayepata wasiwasi kuwa anapata kitu ndani ya swala (katika vitenguzi vya udhu), Akasema: asiondoke mpaka asikie sauti, au apate harufu".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimHadithi hii (kama alivyoeleza Imamu An nawawiy) -Mwenyezi Mungu amrehemu- ni katika kanuni kuu za uislamu na msingi wake ambao hukumu nyingi tukufu zinajengeka juu yake, nayo ni kubaki vitu vilivyo na uhakika katika hukumu yake, haivuki hapo kwasababu tu ya dhana na shaka, sawa sawa shaka iwe na nguvu au isiwe na nguvu, madamu tu haijafika katika ngazi ya uhakika au dhana kuzidi, na mifano ya hilo ni mingi haifichikani, na miongoni mwake ni hadithi hii, madamu mtu ana uhakika na twahara yake, kisha akapata shaka katika kutenguka kwa twahara yake, basi asili ni kubakia kwa twahara yake, na kinyume chake pia, atakayekuwa na uhakika wa hadathi (kutokuwa na udhu) na akawa na shaka na twahara yake, basi kimsingi ni kubakia kwa hadathi yake (kutokuwa na udhu) na katika hili zinaingia nguo na maeneo, asili yake ni twahara, isipokuwa kwa uhakika wa unajisi wake, na katika hilo pia ni idadi ya rakaa za swala, atakayekuwa na uhakika kuwa ameswali rakaa tatu kwa mfano, na akawa na shaka na rakaa ya nne, asili ni kutokuwepo kwa rakaa hiyo, na atatakiwa aiswali hiyo rakaa ya nne, na katika hili pia ni yeyote atakayekuwa na shaka katika kumtaliki mke wake, basi kimsingi ni kubaki kwa ndoa, na hivyo hivyo katika maswala mengi ambayo hayafichikani.
Kutoka kwa Aisha na Abdillahi bin Omar na Anasi bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Itakaposimamishwa swala na kikatengwa chakula cha usiku basi anzeni na chakula cha usiku".
Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim katika riwaya zake zoteItakaposimamishwa swala, na chakula au kinywaji kikawa kiko tayari, inatakiwa kuanza na kula au kunywa mpaka yakatike matamanio ya mwenye kuswali, na akili yake asikaye anafikiria hilo, na aingie katika swala, na sharti ya hilo ni muda wa swala kutokuwa mfinyu, na uwepo wa uhitaji na kufikiria chakula, na hii inathibitisha ukamilifu wa sheria na kuzingatia kwake haki za nafsi pamoja na wepesi na upole.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hachukii muumini wa kiume tabia za muumini wa kike, akichukia tabia fulani basi ataridhishwa na tabia nyingine" Au alisema: "Tabia tofauti na hiyo"
Imepokelewa Imamu MuslimAmemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mume kumchukia sana mke wake hadi kupelekea dhulma, na kumuacha na kumtelekeza; Mwanadamu ana asili ya kutokamilika, na ikiwa atachukia kwake tabia moja mbaya, basi atapata tabia nyingine nzuri; ataridhia kwa tabia hiyo nzuri anayoikubali, na avumilie kwa tabia asizozipenda miongoni mwa tabia mbaya, ambazo humfanya awe mvumilivu na asimchukie kiasi cha kutaka kumuacha.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: “Mnapoingia chooni, msielekee Kibla, wala msikipe mgongo, bali elekeeni Mashariki au Magharibi.” Abuu Ayub akasema: Basi tukaenda Sham tukakuta vyoo vimejengwa kuelekea Kibla, tukawa tunageuka, na tunaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mwenye kutaka kukidhi haja kubwa au ndogo kuelekea Kibla na upande wa Al-Kaaba, na asiigeuze kwa kuiweka nyuma ya mgongo wake. Bali ni lazima ageuke akiwa ndani kuelekea Mashariki au Magharibi ikiwa Kibla chake ni kama kibla cha watu wa Madina. Kisha Abuu Ayub (radhi za Allah ziwe juu yake) akaeleza kuwa walipofika Sham walikuta vyoo vilivyotayarishwa kwa ajili ya kujisaidia vimejengwa kuelekea Al-Kaaba, hivyo wakawa wakijigeuza kutoka upande wa Kibla, pamoja na hivyo bado wanamuomba msamaha Mwenyezi Mungu.
Kutoka kwa Abuu Katada -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya adabu: Akakataza kwa mwanaume kushika uume wake kwa mkono wa kulia wakati wa kukidhi haja, na kuondoa uchafu katika utupu wa mbele au wa nyuma kwa mkono wa kulia, kwa sababu mkono wa kulia umetayarishwa kwa matendo mema, Kama ambavyo alikataza mtu kupumulia ndani ya chombo anachonywea ndani yake.
Kutoka kwa Abdallah bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Walishuhudia kwangu wanaume wanaoridhiwa -na ninaye mridhia zaidi kwangu ni Omar- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amekataza kuswali baada ya swala ya sub-hi mpaka lichomoze jua, na baada ya laasiri mpaka lizame" Na kutoka kwa Abuu Saidi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye amesema: "Hakuna swala baada ya sub-hi mpaka linyanyuke jua, na wala hakuna swala baada ya laasiri mpaka litoweke jua".
Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim kwa riwaya zakeAmekataza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hizi mbili kuswali baada ya swala ya sub-hi mpaka lichomoze jua na linyanyuke toka msitari wa mawingu katika mtazamo wa macho kwa kiasi cha urefu wa mshale, na hili linaweza kukadiriwa kwa dakika kadhaa, wametofautiana wanachuoni katika kiwango chake, kuanzia dakika tano (5) mpaka kumi na tano (15). Na amekataza pia kuswali baada ya swala ya laasiri mpaka litoweke jua, kabla ya adhana ya magharibi kwa dakika chache; kwasababu katika kuswali ndani ya nyakati hizi kuna kujifananisha na washirikina wale wanaoliabudu wakati wa kuchomoza kwake na kuzama kwake, na tumekatazwa kujifananisha nao katika ibada zao; kwasababu atakayejifananisha na watu fulani basi nayeye ni miongoni mwao.
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hivi haogopi mmoja wenu (Au: Hachelei mmoja wenu) atakapoinua kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu akifanye kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye Mwenyezi Mungu sura yake kuwa sura ya punda".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ahadi ya adhabu kali kwa mwenye kunyanyua kichwa chake kabla ya imamu wake, kuwa Mwenyezi Mungu kukifanya kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye sura yake kuwa sura ya punda.
Na kutoka kwa Ibn Omari Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake: Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Alikuwa akinyanyua mikono yake usawa wa mabega yake anapofungua swala, na anapotoa takbira ya kurukuu, na anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu anainyanyua pia, na akasema: "Sami'a llaahu liman hamidahu" Yaani: Amemsikia Mwenyezi Mungu yule aliyemuhimidi, "Rabbanaa walakal hamdu" Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, na alikuwa hafanyi hivyo katika sijida.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume, rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akinyanyua mikono yake katika sehemu tatu wakati wa kuswali, usawa wa mabega ni: Pale panapounga kati ya mfupa wa bega na mkono. Sehemu ya kwanza: Anapofungua swala wakati wa takbira ya kuhirimia swala. Sehemu ya pili: Anapotoa takbira kwa ajili ya rukuu. Sehemu ya tatu: Anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu, na akasema: Sami'allahu liman hamidah, Rabbanaa walakal hamdu. Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi, Mola wetu Mlezi, na sifa njema ni zako. Na alikuwa hanyanyui mikono yake wakati wa kuanza kusujudu, wala wakati wa kunyanyua kutoka katika sijida.
Kutoka kwa bin Masoud radhi za Allahi ziwe juu yake amesema: Alinifundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake, namna ya tashahudi iletwayo ndani ya sala, na kiganja changu kikiwa kati ya viganja vyake, kama anavyonifundisha sura ndani ya Qur'ani: "Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu" Tafsiri yake: Maamkizi (Amani) ni ya Mwenyezi Mungu, na swala na vile vilivyo vizuri, amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, nashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni mjumbe wake. Na katika lafudhi yao nyingine: "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Amani, atakapokaa mmoja wenu katika swala basi na aseme: Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, akisema hivyo, basi dua hii itampata kila mja mwema wa Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu, kisha baada ya hapo atachagua maombi yoyote anayotaka kuomba".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume Rehema na amani ziwe juu yake alimfundisha bin Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake tashahudi inayosemwa ndani ya swala, akiwa kaweka mkono wake ndani ya mikono yake, ili asogeze karibu umakini wa bin Masoud. Na alifanya hivyo kama anavyomfundisha sura ndani ya Qur'ani jambo linaloonyesha kuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake aliitilia umuhimu tashahudi kwa matamshi na maana yake pia. Akasema: "Attahiyyaatu lillaah" (Maamkizi Mema ni ya Mwenyezi Mungu): Nayo ni kila kauli au kitendo kinachojulisha kutukuza, vyote hivyo vinastahiki kufanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Swala": Nazo ni swala zinazofahamika za Faradhi na za sunna zote hizo ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Mambo mazuri": Nayo ni maneno na matendo na sifa njema zinazojulisha ukamilifu, zote hizo zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Amani iwe kwako ewe Nabii na Rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake": Hii ni dua yake ya kuomba amani na uzima dhidi ya kila maafa na yenye kuchukiza, na kuomba ziada na wingi kutoka katika kila kheri. "Amani iwe juu yetu na kwa waja wema wa Mwenyezi Mungu": Hii ni dua ya kuomba uzima kwa kila mwenye kuswali na kwa kila mja mwema aliye mbinguni na ardhini. "Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu": Yaani ninakiri kukiri kwenye kuondoa shaka kabisa yakuwa hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. "Na kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake": Ninakiri kwake kuwa ni mja na kapewa ujumbe wa mwisho. Kisha akamhimiza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuswali achague katika dua aitakayo.