





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akiomba akisema: "Allaahumma inniy a'udhubika min adhaabil Qabri, wa min adhaabin naari, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil masiihiddajjaali" Ewe Mola wangu hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na kutokana na adhabu ya moto, na fitina za uhai na za kifo, na kutokana na fitina za masihi dajali".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akiomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mambo manne, baada ya tashahudi ya mwisho na kabla ya swala, na akatuamrisha tuombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mambo hayo, Jambo la kwanza: Kuomba kinga kutokana na adhabu za kaburi. Jambo la pili: Kuomba kinga ya kuepukana na adhabu ya moto siku ya Kiyama. La tatu: Kuomba kinga itokanayo na fitina za uhai ikiwemo matamanio ya dunia yaliyoharamishwa na ikiwemo pia shub-ha (utata) wenye kupoteza, na kutokana na fitina za mauti, yaani muda wa kukata roho, tusije kupinda tukatoka katika Uislamu au Sunna, au fitina za kaburini kama maswali ya Malaika wawili. Jambo la nne:Kuomba kinga zitokanazo na fitina za Masihi Dajali atakeyetokea zama za mwisho, Mwenyezi Mungu atawapa mtihani waja wake kupitia yeye; na Mtume kamtaja kwa jina kutokana na ukubwa wa fitina zake.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapotoa takbira katika swala ananyamaza kidogo kabla hajaanza kusoma, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimuweka fidia baba yangu na mama yangu, hebu nieleze kunyamaza kwako kati ya takbira na kisomo: Ni nini unasema: Akasema: Ninasema: Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Allaahumma naqqiniy- Ewe Mwenyezi Mungu nitakase mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- kamaa yunaqqath-thaubul abyadhwa -kama inavyotakaswa nguo nyeupe- minad danasi -kutokana na uchafu. Allaahumma ghsilniy -Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- bil maai wath thalji wal baradi -kwa maji na barafu na baridi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema “Allahu Akbar” kwa ajili ya swala, alikuwa akitulia kidogo kabla ya kusoma Al-Fatiha, ambamo alikuwa akiianza Swala yake kwa baadhi ya dua, miongoni mwa dua hizo zilizoripotiwa ni kauli yake: "Allaahumma baaid bainii wa baina khatwaa yaaya, kamaa baa'atta bainal mashriqi wal maghribi, Allaahu naqinii min khatwaayaaya, kamaa yunaqqah-thaubal abyadhwa minad-danasi, Allaahuma gh-silnii bil maai wath-thalji wal baradai", Hivyo anamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amtenge mbali na madhambi ili asije akaangukia ndani yake, hata kusiwe na kukutana nayo, kama vile hakuna kukutana baina ya Mashariki na Magharibi, na ikitokea katumbukia ndani yake, basi amtakase kutokana na madhambi hayo kama uchafu unavyotolewa kwenye nguo nyeupe, na amuoshe dhambi zake na kuupoza miale na joto lake, kwa vitakatishi hivi baridi; Maji, theluji na baridi.
Kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Linganeni sawa katika sijida, na asikunjue mmoja wenu mikono yake kama anavyokunjua mbwa".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAmeamrisha Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- kulingana katika sijida, na hii nikuwa, ili mwenye kuswali awe na muonekano mzuri katika sijida, kiasi kwamba aweke viganja vyake katika ardhi, na anyanyue miundi yake na aiweke mbali na mbavu zake, kwasababu hali hii ndio anuani ya uchangamfu na hamu vinavyohitajika ndani ya swala, na ni kwasababu muonekano huu mzuri unaviwezesha viungo vya kusujudu vyote kuchukua nafasi yake katika ibada. Na akakatazwa kunyoosha mikono miwili katika sijida; kwasababu hii ni dalili ya uvivu na uchovu, na kuna kujifananisha na mbwa, nako nikujifananisha na kisichofaa.
Kutoka kwa Maslama Saidi bin Yazid amesema: nilimuuliza Anas bin Malik: alikuwa Nabii Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake- akiswali na viatu vyake? akasema: ((ndio)).
Imepokelewa na Al-BukhaariyKatika madhumuni ya sheria ni kutofautiana na watu wa kitabu, (Mayahudi na wakristo), nakuondoa kila kitu ambacho ndani yake kina tabu na uzito juu ya muislamu, na alimuuliza Saidi bin thabit naye ni katika waaminifu wakubwa miongoni mwa wanafunzi wa maswahaba, kamuuliza Anas bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuhusu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Hivi je alikuwa akiswali na viatu vyake; ili iwe kwake ni kiigizo? Au ni kwasababu aliliona hilo haliwezekani kwasababu yakuwa mara nyingi huwa na uchafu na udhia, Anasi akamjibu, Ndiyo, alikuwa akiswali na viatu vyake, nakuwa hilo ni katika sunna zake takatifu, na hili si maalumu kwa ardhi fulani au zama maalumu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba". Na kwa Muslim: "Moja kati ya mara hizo aoshe kwa udogo"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake chombo hicho kioshwe mara saba ikiwa mbwa ataingiza ulimi wake ndani yake, mara ya kwanza iwe kwa mchanga, ili yaje maji baada yake, hivyo usafi kamili utakuwa umepatikana kutokana na najisi yake na madhara yake.
Imepokewa Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msalani anasema: "Allaahumma inniy Auudhubika minal khubuthi wal khabaa ithi" (Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na mashetani wa kike na mashetani wa kiume).
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuingia mahali ambapo atakidhi haja yake hapo, haja ndogo au kubwa, anaomba kinga kwa Mwenyezi Mungu, na anajielekeza kwake amkinge na shari za mashetani wa kiume na wa kike, Na limetafsiriwa neno khubuthi na khabaaithi (Mashetani wa kiume na wa kike) kwa maana ya shari na najisi.
Kutoka kwa Sahali bin Hunaif radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake"
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayeomba shahada na kuuawa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akawa mkweli na mwenye ikhlasi katika nia yake hiyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu atamjaalia kupata daraja za mashahidi kwa nia yake ya kweli, hata akifa kitandani katika hali isiyokuwa jihadi.
Kutoka kwa Abdillahi bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema "Waliamrishwa watu kuwe kuagana kwao kwa mwisho ni katika nyumba (Alka'ba), isipokuwa likaondoshwa hilo kwa mwanamke mwenye hedhi".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimNyumba tukufu inaheshima na takrima; yenyewe ni alama ya ibada za Mwenyezi Mungu na utulivu na unyenyekevu mbele yake yeye, ikapata heshima ndani ya vifua, na utukufu ndani ya nyoyo, na mapenzi na kufungamana nayo. Na kwaajili hiyo akamuamrisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mwenye kuhiji iwe kuaga kwake ni hapo, na hii ndiyo twawafu (mzunguko) wa mwisho ambao ndio mzunguko wa kuaga, isipokuwa mwanamke mwenye hedhi; ni kwasababu huenda akauchafua msikiti kwa kuingia kwake, ikaondolewa kwake twawafu (mzunguko) bila kuufidia, na hii ni dalili katika hija hivyo haijumlishi na Umrah.
Imepokelewa kutoka kwa Maimuna mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Nilimuandalia kuoga Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikamfunika nguo, na akamimina maji juu ya mikono yake na akaiosha, kisha akamimina maji kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto, kwa hiyo, akaosha sehemu zake za siri na kuzisafisha, akapiga ardhi kwa mkono wake, akaufuta, kisha akauosha, kisha akasukutua kinywa chake na akapandisha maji puani, na akaosha uso na mikono, kisha akamwagia maji kichwani kwake na akaeneza mwili mzima, kisha akasogea pembeni na akaosha miguu yake, nikampa nguo, lakini hakuichukua, akaondoka huku akifuta mikono yake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMama wa Waumini Maimuna Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alitueleza jinsi Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake alivyokuwa akioga janaba, kiasi kwamba alimuwekea maji ya kuoga, na akamfunika kwa pazia, basi Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, akafanya yafuatayo: Kwanza: Alimimina maji kwenye mikono yake na akaiosha kabla ya kuiingiza katika chombo. Pili: Alimimina maji kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto na kuosha sehemu zake za siri ili kuisafisha kutokana na athari yoyote ya janaba. Tatu: Aliipiga ardhi kwa mkono wake, akaufuta, kisha akauosha ili kuondoa udhia. Nne: Alisukutukua; Kwa kuingiza maji katika kinywa chake na kuyazungusha, kisha kuyatema; na akavuta maji puani kwa pumzi yake, kisha akayatoa nje ili kuisafisha. Tano: Aliosha uso wake na mikono yake. Sita: Alimimina maji juu ya kichwa chake. Saba: Alimimina maji katika mwili wake mzima. Nane: Alitoka mahali alipoogea na akaosha miguu yake katika mahali pengine, kwani hakuiosha mwanzo. Kisha akamletea kitambaa ili ajifute kwacho, akawa hakukichukua, na akaanza kufuta maji kutoka mwilini kwake kwa mkono wake, na anayapangusa.