





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapooga kwa ajili ya janaba, anaosha mikono yake, na anatawadha udhu wake ule wa swala, kisha anaoga, kisha anaachanisha nywele zake kwa mkono wake, mpaka pale anapohisi kuwa ngozi yake yote imeenea maji, anajimwagia maji kwa michoto mitatu, kisha anaosha mwili wake wote uliobakia, na Aisha akasema: Nilikuwa nikioga mimi na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake katika chombo kimoja, tukichota sote katika chombo hicho.
Imepokelewa na Al-BukhaariyAlikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuoga janaba anaanza kwa kuosha mikono yake, kisha anatawadha kama anavyotawadha udhu wa swala, kisha anajimwagia maji katika mwili wake kisha anaachanisha nywele za kichwa chake kwa mikono yake, mpaka anapohisi kuwa maji yamefika katika maoteo ya nywele zake, na yameloanisha ngozi, anajimwagia maji kichwani mara tatu kisha anaosha mwili mzima. Na akasema Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nikioga mimi pamoja na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutoka katika chombo kimoja, tukichota sote.
Kutoka kwa Ally bin Husein: "Yakwamba yeye aliona mtu mmoja anakuja toka katika kiupenyo kidogo kilikuwa katika kaburi la Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anaingia na anaomba hapo, akamkataza, na akasema: Hivi nikusimulieni hadithi niliyoisikia toka kwa baba yangu toka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- amesema: "Msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, wala nyumba zenu kuwa makaburi, na nitakieni rehma, kwani dua zenu hunifikia popote mlipo".
Imepokelewa na Ibn Abii ShaybahAnatueleza Ally bin Husein -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba yeye alimuona mtu mmoja akimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kaburi la Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, nakuwa yeye alimkataza juu ya hilo kwa ushahidi wa hadithi ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ambayo limekuja ndani yake katazo la kulifanyia mazoea kaburi lake kwa ziara, na katazo la kuzitelekeza nyumba kwa kutokuwa na ibada ya Mwenyezi Mungu ndani yake na dhikri, na kuifananisha kwake na kaburi, na akaeleza kuwa salamu ya muislamu itamfikia yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- mahala popote atakapokuwa muislamu.
Imepokewa Kutoka kwa Ally -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa ni mtu mwenye kutokwa na madhii kwa wingi na nilikuwa nikiona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutokana na nafasi ya binti yake kwangu, nikamuamrisha Mikidadi bin Aswadi, akamuuliza, akasema: "Aoshe tupu yake na atawadhe" Na katika sahihi Bukhari: Akasema: "Tawadha na uoshe tupu yako".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Ally bin Abiy Twalib Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye ilikuwa mara nyingi akitokwa na madhii -nayo ni maji meupe mepesi yenye utelezi hutoka katika tupu wakati wa matamanio au kabla ya tendo ya ndoa-, Na wala hajui afanye nini yakitoka, akaona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake; kwa sababu yeye ni mume wa Fatma binti wa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, Akamuomba Mikidadi bin Aswadi amuulize Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuhuus hilo, Basi akajibu Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa aoshe tupu yake kisha atawadhe.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu".
Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na AhmadImetilia mkazo hadithi ya Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake swala la kuanza na kulia katika mambo mazuri, ikapokelewa kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Mtakapo vaa" Yaani mkitaka kuvaa. "Na mtakapo tawadha" Yaani mkitaka kufanya. "Anzeni na kuliani kwenu" ni wingi wa kulia nacho ni kinyume cha kushoto, aingize upande wa kulia wa kanzu, kabla ya kushoto na atangulize kulia katika mikono yake na miguu yake katika udhu, kisha tambua kuwa katika viungo vya udhu vipo ambavyo si sunna kuanza na kulia, navyo ni masikio mawili na viganja viwili na mashavu mawili, bali husafishwa vyote kwa wakati mmoja, ikiwa litakuwa gumu hilo kama ilivyo kwa aliyekatwa mkono na mfano wake atatanguliza kulia.
Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni swala kwa wakati wake", Akasema: Kisha ipi? Akasema: "Kisha wema kwa wazazi wawili" Akasema: "Kisha ipi? "Akasema: "Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu" Akasema: Alinihadithia mambo hayo, na lau ningemtaka ziada angenizidishia.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliulizwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni amali ipi inapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu?. Akasema: Ni swala za faradhi katika wakati wake uliopangwa na sheria, Kisha wema kwa wazazi wawili, kwa kuwafanyia wema, na kusimamia haki zao, na kuacha kuwaasi, kisha Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuitetea dini ya Uislamu na waislamu, na kudhihirisha alama zake, na hii inakuwa kwa nafsi na mali. Akasema bin Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake: Alinieleza amali hizi; na lau kama ningelimwambia: Kisha ipi? Basi angenizidishia.
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa kuna Malaika wawili wanateremka, anasema mmoja wao: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mtoaji badala, na anasema mwingine: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mzuiaji (Bahili) hasara".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika kila siku inayochomozewa na Jua ndani yake kuna Malaika wawili wanateremka na kunadi, anasema mmoja wao: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mwenye kutoa katika njia za utiifu na kwa familia na kwa wageni na sadaka za hiyari mrejeshee na mpe badala bora kuliko kile alichotoa, na umbariki. Na anasema mwingine: Ewe Mwenyezi Mungu mpe bahili mzuiaji uharibifu katika mali yake na uiteketeze mali yake anayoizuia na kutompa mwenye kustahiki.
Kutoka kwa Huswain bin Abdirrahman amesema: Nilikuwa kwa Saidi bin Jubair akasema: Ni nani kati yenu aliyeiona nyota iliyodondoka jana usiku? Nikasema: Mimi, kisha nikasema: Ama mimi sikuwa katika swala, lakini niling'atwa na Nge, akasema: nini ulifanya? nikasema: nilijisomea Ruqya, akasema: Ni nini kilikupelekea kufanya hivyo? Nikasema: Ni hadithi aliyotuhadithia Sha'abiy, akasema: Aliwahadithia nini? Nikasema: Alituhadithia kutoka kwa Buraida bin Huswaib yakwamba yeye amesema:"Hakuna kisomo cha ruqya isipokuwa kwa kijicho au homa", Akasema: Amefanya vizuri aliyeishia pale aliposikia, lakini alituhadithia sisi bin Abbasi kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Nilikusanyiwa mimi Ummati, nikamuona Nabii akiwa pamoja na kundi na Nabii akiwa pamoja na mtu mmoja na watu wawili, Na Nabii akiwa hana hata mtu mmoja, Ghafla ukanyanyuliwa kwangu weusi mkubwa, nikadhania kuwa hao ni umma wangu, nikaambiwa: Huyu ni Musa na watu wake, nikatazama tena, Ghafla nikaona weusi mkubwa, nikaambiwa: Huu ni umma wako, Ukiwa pamoja na watu elfu sabini wanaingia peponi bila hesabu wala adhabu, kisha akanyanyuka akaingia nyumbani kwake, watu wakazungumza mengi kuhusu watu hao (wanaoingia peponi bila hesabu wala adhabu); Wakasema baadhi yao: Huenda hao ni wale waliosuhubiana (walioambatana) na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Na wakasema baadhi yao: Huenda hao ni wale waliozaliwa katika uislamu na wakawa hawakumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, Na wakataja mambo mengi! Basi akatoka kwao Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- wakamueleza, Akasema: Hao ni wale ambao hawaombi watu kuwasomea ruqya, na wala hawajitibu kwa moto, na wala hawaamini mikosi ya ndege, na kwa Mola wao ndiko wanakotegemea, hapo akasimama (bwana mmoja akiitwa) Ukasha bin Mihswani akasema: Muombe Mwenyezi Mungu anifanye kuwa miongoni mwao, akasema: Wewe ni miongoni mwao, kisha akasimama mtu mwingine akasema: Muombe Mwenyezi Mungu anifanye kuwa miongoni mwao, Akasema: kakutangulia kwa hilo Ukasha".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAnatueleza Huswain bin Abdirrahman -Mwenyezi Mungu amrehemu- kuhusu mazungumzo yaliyojiri kati yake na Saidi bin Jubair -Mwenyezi Mungu amrehemu- kuhusu swala la kisomo cha Ruqya,Na hiyo ni kwasababu Huswain aling'atwa na nge na akajisomea kwaajili ya hilo ruqya ya kisheria, na alipomuuliza Saidi kuhusu ushahidi wake akamueleza kwa hadithi ya Sha'biy ambayo ina halalisha ruqya kwasababu ya kijicho au sumu,Saidi akamsifia kwa hilo,lakini yeye akampokelea hadithi ambayo inayopendekeza kuacha kufanya ruqya, nayo ni hadithi ya bin Abbasi ambayo inaambatana na sifa Nne ambazo atakayesifika nazo atastahiki kuingia peponi bila hesabu wala adhabu, nazo ni kutotafuta kisomo cha ruqya, na kutojitibu kwa moto,na kutoamini mikosi, na ukweli wa kutegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu,na alipoomba Ukasha toka kwa Nabii-Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa amuombee ili awe miongoni mwao akamueleza kuwa yeye ni miongoni mwao,na aliposimama mtu mwingine kwa lengo hilo hilo akamjibu kwa upole Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa kumzuilia hilo na kwa kufunga mlango na kukata muendelezo wa watu wengine.
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema siku ya vita vya Khaibari: "Kesho nitampa bendera hii mtu ambaye Mwenyezi Mungu ataleta ushindi kupitia mikononi mwake, ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda." Akasema: Watu wakalala usiku kucha wakijadili hilo, ni nani kati yao atakayepewa! Palipopambazuka watu walikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake wote wakitaraji kuwa atapewa, akasema: “Yuko wapi Ally bin Abi Twalib?" pakasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, anaumwa macho, akasema: “Basi mtumieni mtu akamuite.” Akaletwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akamtemea mate machoni mwake na akamuombea, akapona kana kwamba hakuwa na maradhi, hivyo akampa bendera, na Ally akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nipigane nao mpaka wawe kama sisi? Akasema: “Songa mbele, mpaka utue kwenye uwanja wao, kisha uwaite kuja katika Uislamu, na uwafahamishe yale yaliyo wajibu juu yao katika haki za Mwenyezi Mungu kwake, Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako, hilo ni bora zaidi kwako kuliko ngamia wekundu."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume rehema na amani ziwe juu yake aliwaeleza Maswahaba kuhusu ushindi wa Waislamu dhidi ya Mayahudi wa Khaibar siku ya kesho, na hilo litakuwa mikononi mwa mtu atakayempa bendera, nayo ni bendera ambayo hutumiwa na jeshi kama nembo yake. Na mtu huyu miongoni mwa sifa zake ni pamoja na kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda. Kwa hiyo Maswahaba walipitisha usiku kucha wakijadiliana na kuzungumza juu ya nani atapewa bendera? Kwa kutamani kuipata heshima hii kubwa, Ilipofika asubuhi walikwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wote wakiwa na matumaini ya kupata heshima hii. Basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuulizia Ally bin Abi Twalib Allah amuwie radhi? Pakasemwa: Ni mgonjwa na analalamika kuhusu macho yake. Basi rehema na amani zimshukie, akamtumia watu wakamlete, akamtemea Ally machoni katika mate yake matukufu na akamuombea, akapona ugonjwa wake kana kwamba hakuwa na maradhi, akampa bendera na akamwamuru aende kwa upole mpaka aikaribie ngome ya maadui na awaite katika Uislamu, ikiwa watamjibu; Awaambie ni wajibu gani wanapaswa kufanya. Kisha rehema na amani ziwe juu yake, akamueleza Ally ubora wa kumuita mtu kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba ikiwa mlinganiaji atakuwa ni sababu ya kuongoka kwa mtu mmoja, hiyo ni bora zaidi kwake kuliko kuwa na ngamia wekundu ambao ndio utajiri wa thamani zaidi kwa Waarabu, azimiliki au azitoe sadaka.
Kutoka kwa Zaidi bin Khalid radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na atakayemsimamia mpiganaji kwa wema katika familia yake basi na yeye atakuwa kapigana".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayemuandalia mwenye kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu sababu za safari yake na anachohitaji katika silaha muhimu, vipando, chakula, gharama na vitu vingine; basi yuko katika nafasi sawa na mpiganaji, na atapata malipo ya mpiganaji. Na atakayesimamia jambo la mpiganaji kwa wema, na akakaa badala yake katika kulea familia yake wakati asipokuwepo basi naye yuko katika hukumu ya mpiganaji.