





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Thabit bin Dhwahaki- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba yeye alimuunga mkono Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- chini ya mti, nakuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Atakaye apa juu ya kiapo cha mila isiyokuwa ya uislamu kwa uongo tena kwa makusudi basi atakuwa kama alivyosema, na atakayeua nafsi kwa kitu chochote ataadhibiwa nacho siku ya kiyama, na hakuna uwajibu juu ya mtu ya kuweka nadhiri katika vile asivyovimiliki" Na katika riwaya nyingine: "Na kumlaani muumini ni sawa na kumuuwa". Na katika riwaya: "Na atakayedai madai ya uongo ili ajichumie (mali) kupitia madai hayo hatomzidishia Mwenyezi Mungu -Mtukufu- isipokuwa upungufu".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAmepokea Thabit bin Dhwahaki Al-Answariy -mmoja kati ya waliomuunga mkono Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- chini ya mti, katika mkataba wa maridhiano siku ya vita vya hudaibia, kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye amesema katika maana ya maneno yake: Atakaye apa juu ya kiapo kilicho nje ya sheria ya uislamu, mfano akasema: Yeye ni Myahudi au mkristo, au yeye ni majusi, au yeye ni kafiri au kajitenga mbali na Mwenyezi Mungu na Mtume wake itakapokuwa kadhaa wa kadhaa, akadhamiria kusema uongo katika kiapo chake basi atakuwa kama alivyojinasibishia katika moja miongoni mwa mila za kikafiri. Na atakayeiuwa nafsi yake kwa kitu chochote, kama panga, au kisu, au risasi, au kinginecho katika vifaa vya kuulia, ataadhibiwa nacho siku ya kiyama. Na atakayetia nadhiri ya kitu ambacho hakimiliki kama akiweka nadhiri ya kumuacha huru mtumwa wa fulani, au kutoa sadaka katika mali ya fulani, basi nadhiri yake imeharibika na wala haizingatiwi; kwasababu haijaangukia mahala pake, na haijashuka mahala pake. Na atakayemlaani muumini, atakuwa ni kama kamuuwa, kwa kushirikiana mtoa laana na muuwaji kuvunja maharamisho ya Mwenyezi Mungu- Mtukufu- na kuchuma madhambi, na kustahiki adhabu. Na atakayekua na kiburi na akataka wingi wa mali kwa kuleta madai ya uongo yasiyokuwepo, katika mali au elimu au nasaba au utukufu au cheo au kinginecho, akitaka kwa hilo kuongezeka, hatomzidishia Mwenyezi Mungu isipokuwa udhalili na unyonge; kwasababu yeye ametaka kuinyanyua nafsi yake kwa yasiyokuwepo, hivyo malipo yake yataendana na namna ya makusudio yake.
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnahimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumjibu muadhini wakati wa kumsikia, na hii ni kwa sisi kusema mfano wa ayasemayo, sentensi kwa sentensi, Anaposema Allaahu Akbaru nasi tunasema Allaahu Akbaru, na anapotamka shahada mbili, nasi tunazitamka baada yake, Linaondolewa tamko la: (Hayya a'las swalaa, Hayya a'lal falaah) hapo tutasema baada yake: Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah.
Kutoka kwa MughIira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema: "Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi", akafuta juu yake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika moja ya safari zake akatawadha, alipofikia kuosha miguu miwili alinyoosha Mughira bin Shu'ba Radhi za Allah ziwe juu yake mikono yake ili avue kilichokuwa miguuni kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika khufu (viatu mithili ya soksi) ili Mtume aoshe miguu yake! Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ziache na wala usizivue, kwani mimi niliingiza miguu yangu ndaniya khufu mbili nikiwa katika twahara, Akafuta Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya khufu zake badala ya kuosha miguu miwili.
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Fatma bint Abii Qubaishi alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Mimi hupatwa na hedhi ya ugonjwa na sitwahariki, je niache swala? Akasema: "Hapana, hakika hilonitatizolinatokananamshipawakizazikukatika, lakini acha swala kwa kiasi cha siku ulizokuwa ukipata hedhi ndani yake, kisha oga na swali".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeFatma bint Abii Qubaishi alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika mimi damu haikatiki kwangu na huendelea hata nje ya wakati wa hedhi, je itakuwa hukumu ya damu hiyo ni hukumu ya damu ya hedhi ili niache swala? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema kumwambia: Hiyo ni damu ya ugonjwa, nayo ni damu ya ugonjwa ambayo husababishwa na kukatika kwa mshipa katika mfuko wa uzazi, na si damu ya hedhi, Unapokuja muda wa hedhi uliokuwa ukipata hedhi ndani yake kwa mujibu wa ada yako ya mwezi kabla hujaugua, basi acha swala na swaumu na mengineyo anayozuiliwa kuyafanya mwenye hedhi wakati wa hedhi. Kinapomalizika kiwango cha muda huo, hapo utakuwa umetwaharika na hedhi, osha mahali palipo na damu, kisha osha mwili wako josho kamili kwa ajili ya kuondoa hadathi, kisha swali.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wenye kuswali kunyoosha safu zao, na wasitanguliane wala wasirudi nyuma, na kwamba kuzinyoosha ni sehemu ya kukamilisha na ukamilifu wa Sala, na kuwa kupinda kwa safu ni dosari na ni upungufu ndani yake.
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke maji puani mwake kisha ayapenge, na atakayestanji kwa mawe basi afanye yawe witiri, na atakapo amka mmoja wenu toka usingizini basi na aoshe mikono yake kabla ya kuingiza ndani ya chombo chake, kwani mmoja wenu hajui ni wapi ulilala mkono wake". Na lafudhi ya Muslim: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini kwake basi asizamishe mkono wake ndani ya chombo mpaka auoshe mara tatu, kwani hajui ni wapi ulilala mkono wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baadhi ya hukumu za twahara, miongoni mwake: Ya kwanza: Nikuwa mwenye kutawadha ni lazima aingize maji puani mwake kwa kuyavuta kwa pumzi, kisha ayatoe kwa pumzi pia. Ya pili: Nikuwa atakayetaka kusafisha udhia uliomtoka na kuuondoa pasina kutumia maji kama kwa jiwe na mfano wake, basi kusafisha kwake kuwe kwa idadi ya mamoja (witiri) kwa uchache tatu na kuendelea yatakayoweza kutakatisha kilichotoka na kusafisha mahali. Ya tatu: Kuwa atakayeamka kutoka katika usingizi wa usiku asiingize kiganja chake ndani ya chombo ili atawadhe mpaka akioshe mara tatu nje ya chombo, kwani hajui ni mahali gani ulilala mkono wake, hauwezi kuaminika na kutokuwa na najisi, na huenda shetani aliuchezea na akaubebesha vitu vyenye kumdhuru mwanadamu au vyenye kuharibu maji.
imepokewaKutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake, kwani hakika fitina ya kwanza ya wana wa Israeli ilikuwa kwa wanawake"
Imepokelewa Imamu MuslimAnabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Dunia ina ladha tamu, na ni kijani katika mandhari, hivyo mwanadamu hudanganyika nayo na kuikimbilia na kuifanya kuwa ndio hamu yake kubwa. Nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amewafanya baadhi yetu kuwa warithi wa wengine katika dunia hii, ili aone ni namna gani tutafanya, je tutasimama katika utiifu wake, au maasi yake? Kisha akasema: Tahadharini sana na zisikudanganyeni starehe za Dunia na mapambo yake, zikakupelekeeni kuacha aliyokuamrisheni Mwenyezi Mungu, na kuingia katika yale aliyokukatazeni. Na miongoni mwa mambo makubwa ya wajibu kutahadhari nayo katika fitina za Dunia ni fitina ya wanawake, nakuwa ndio iliyokuwa fitina ya kwanza waliotumbukia ndani yake wana wa Israeli.
Imeokewa Kutoka kwa bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema : Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi: Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri, na muda huo ulikuwa ni wakati ambao haruhusiwi yeyote kuingia kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Hafswa ndiye aliyenisimulia kuwa alikuwa anapoadhini muadhini na ikachomoza Alfajiri anaswali rakaa mbili, na katika riwaya nyingine: Nikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali baada ya Ijumaa rakaa mbili.
Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim katika riwaya zake zoteAnabainisha Abdullahi bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake: Yakuwa miongoni mwa swala za sunna alizozihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni rakaa kumi na huitwa kuwa ni sunna zilizopangiliwa, Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, Na kabla ya Alfajiri rakaa mbili, Zikatimia rakaa kumi. Na ama swala ya Ijumaa aliswali baada yake rakaa mbili.
Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa mswaki.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mara nyingi akipiga mswaki na akiamrisha watu kufanya hivyo, na kuna baadhi ya nyakati kumetiliwa mkazo, mfano; kupiga mswaki wakati wa kuamka usiku, kwani alikuwa rehema na amani ziwe juu yake akisukutua na kutakatisha kinywa chake kwa mswaki.