





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao- amesema: Tulirejea tukiwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina mpaka tulipofika katika njia yenye maji, walifanya haraka baadhi ya watu kusali laasiri, wakatia udhu wakiwa na haraka, tukawakuta na hali yakuwa visigino vyao vikiwa vyeupe havijaguswa na maji, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ole wao (wasiofikisha maji katika) visigino (watakua na adhabu ya) moto, enezeni maji ya udhu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlisafiri Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina akiwa pamoja na Masahaba zake, wakiwa njiani walipata maji, wakaenda mbio kutia udhu kwa ajili ya swala ya Alaasiri baadhi ya Masahaba, mpaka ukaonekana weupe mwisho wa miguu yao kwa mtu mwenye kuitazama kwa kukosa maji, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ni adhabu na maangamivu katika moto kwa wenye kufanya uzembe wa kuosha mwisho wa nyayo wakati wa udhu, na akawaamrisha wapitilize katika kuukamilisha udhu.
Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema mmoja wenu: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu, akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu. kisha akasema: Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullahi, Akasema: Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullahi, kisha akasema: Hayya ala Swalaah, akasema: Laa Haula wala Quwwata ila Billahi, kisha akasema: Hayya ala lfalaah, akasema: Laa Haula walaa Quwwata ila Billahi, kisha akasema: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, akasema: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema: Laa ilaha ila llahu, akasema: Laa ilaha ila llahu, kutoka ndani ya moyo wake, basi ataingia peponi".
Imepokelewa Imamu MuslimAdhana ni kuwatangazia watu kuwa muda wa swala umeingia, na maneno ya adhana ni maneno yaliyokusanya itikadi ya imani. Na katika hadithi hii anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kinachotakiwa kisheria wakati wa kusikia adhana, nako msikiaji asema kama anavyosema muadhini, muadhini akisema: "Allahu Akbaru" Mwenye kusikia naye anasema: "Allahu Akbaru" ataendelea hivyo, isipokuwa katika kauli ya muadhini "Hayya alas swalaa", "Hayya alal falaah, atasema mwenye kusikia: "Laa haulaa wala quwwata illaa billaah". Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye rudia rudia nyuma ya muadhini kwa utakasifu kutoka moyoni mwake ataingia peponi. Na maana ya maneno ya adhana ni: "Allahu Akbaru": Yaani: Yeye mtakasifu ni mtakasifu na ni mtukufu na ni mkubwa kuliko kila kitu. "Ash-hadu an laa ilaaha illa llaah": Yaani: Hapana muabudiwa wa haki zaidi ya Allah. "Ash-hadu anna Muhammadan Rasuulu llaah" Yaani: Nina kiri na nina shuhudia kwa ulimi wangu na moyo wangu, yakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alimtuma Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni wajibu kumtii. "Hayya alas swalaa", Yaani: Njooni katika swala, na kauli ya mwenye kusikia: "Laa haulaa walaa quwwata illa billaah", Yaani hakuna ujanja wa kuvimaliza vikwazo vya ibada, wala nguvu ya kuzifanya na wala uwezo wa chochote ila ni kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Hayya alal falaah", Njooni katika sababu ya kufanikiwa, nako ni kufuzu kwa Pepo na kusalimika na moto.
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeisahau swala, basi aiswali atakapoikumbuka, haina kafara nyingine isipokuwa hiyo: "Na simamisha swala kwa ajili ya kunitaja mimi" [Twaha: 14].
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesahau kutekeleza swala ya faradhi mpaka ukatoka wakati wakati wake, basi anatakiwa aende mbio na afanye haraka kuilipa pale anapoikumbuka, amesema Allah katika kitabu chake kitukufu: "Na usimamishe swala kwa ajili ya kunitaja" [Twaha: 14] Simamisha swala zilizosahaulika unapozikumbuka.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akikaa itikafu katika kila ramadhani siku kumi, ulipofikia mwaka aliofishwa ndani yake alikaa itikafu siku ishirini
Imepokelewa na Al-BukhaariyAlikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akibakia msikitini akijitenga kwaajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu katika kila ramadhani siku kumi, na alikuwa akikaa itikafu katika siku kumi za katikati, kwa matarajio kuwa anaweza kuipata Lailatul Qadri (usiku wenye cheo), alipojua kuwa uko katika siku kumi za mwisho alikaa itikafu ndani ya siku hizo, kisha akakaa itikafu katika mwaka aliofishwa ndani yake siku ishirini kwa lengo la kuzidisha utiifu na kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba mwanamke mmoja alipatikana akiwa kauwawa katika moja ya vita vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akakemea vikali Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuuwawa wanawake na watoto.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume rehema na amani ziwe juu yake aliona mwanamke akiwa kauwawa katika moja ya vita, akakemea vikali kuuwawa wanawake na watoto ambao hawajafikia balehe.
Kutoka kwa Abuu Tha'laba Al-khushaniy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Nilimuendea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hakika sisi tuko katika ardhi ya watu wa kitabu, je tule katika vyombo vyao? na katika ardhi ya mawindo, ninawinda kwa upinde wangu na kwa mbwa wangu ambaye hajafunzwa, na kwa mbwa aliyefunzwa, ni kipi kinachofaa kwangu? Akasema: Ama ulichokisema- yaani kuhusu vyombo vya watu wa kitabu- : mkipata vyombo vingine basi msile katika vyombo hivyo, msipopata vingine basi viosheni, na kuleni ndani yake, na ulichokiwinda kwa upinde wako, ukataja jina la Mwenyezi Mungu juu yake basi kula, na ulichokiwinda kwa mbwa wako aliyefunzwa, na ukataja jina la Mwenyezi Mungu juu yake basi kula, na ulichowinda kwa mbwa wako ambaye hajafunzwa ukaweza kukichinja basi kula".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimAlieleza Abuu Thaalaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakuwa wao wamepewa mtihani wa ujirani wa watu wa kitabu, na makusudio ya hao ni mayahudi na wakristo, je ni halali kwao wale katika vyombo vyao pamoja na dhana ya unajisi wake? Akamjibu kuwa inafaa kula ndani yake, Na ni bora zaidi kuvitumia katika matumizi yasiyokuwa kula kwa sharti mbili: 1- Kutopatikana vyombo vingine tofauti na hivyo. 2- Na wavioshe. Na akamueleza kuwa wao wako katika ardhi ya mawindo, nakuwa yeye anawinda kwa upinde wake na kwa mbwa wake aliyefunzwa juu ya uwindaji na adabu zake, na kwa mbwa wake ambaye hajafunzwa, ni kipi kinachofaa kwake na cha halali katika viwindwa vya hivi vifaa? Akamjibu kuwa alivyoviwinda kwa upinde wake basi hivyo ni halali, kwa sharti ataje jina la Mwenyezi Mungu -Mtukufu- wakati wa kurusha mshale. Na ama unavyoviwinda kwa mbwa, wakiwa wamefunzwa na ukataja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kumtuma hicho ni halali pia, na ama ambao hawajafunzwa, si halali viwindwa vyake isipokuwa atakapokikuta mtu kikiwa hai na akichinje kichinjo cha kisheria.
Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Amekataza kuweka nadhiri, na akasema: "Hakika nadhiri haiji kwa kheri, bali hutolewa kwayo (vilivyo) kwa bahili"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka nadhiri, nayo ni mtu kujiwajibishia kitu ambacho sheria haijamlazimisha kukifanya, na akasema kuwa: Nadhiri haiwahishi kitu na wala haikicheleweshi, bali hutolewa vilivyo kwa mtu bahili ambaye hafanyi ila yale ya wajibu pekee, nakuwa nadhiri haileti kitu ambacho hakikukadiriwa.
Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ary radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake nikiwa na kundi la Ash’ari ili kumuomba atuchukue, akasema: “Wallahi sitokuwa na chochote cha kukubebeni ” Kisha tukakaa muda kidogo aliopenda Mwenyezi Mungu tukae, tukaletewa ngamia, akaamrisha tupewe wanyama watatu kwa ajili yetu, tulipoondoka wakasema baadhi yetu kuwaambia wengine: Mwenyezi Mungu hatotubariki, tumemuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake tukamuomba atubebe katika vipando lakini akaapa kuwa hatotubeba, kisha akatubeba, akasema Abuu Musa: Basi tukaja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake tukamueleza hilo, akasema: “Si mimi niliyekubebeni, bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyekubebeni Wallahi – akipenda Mwenyezi Mungu - sitokula kiapo cha jambo fulani isipokuwa ninapoona kilichobora zaidi basi huwa ninatoa kafara ya kiapo changu kisha ninafanya lililo bora zaidi.”
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnasimulia Abuu Musa Al-Ash’ari radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akiwa na kundi la kabila lake, na makusudio yao yalikuwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, ili awape ngamia wapande, ili kuweza kushiriki katika jihadi, aliapa rehema na amani ziwe juu yake kuwa hatowabeba, na hakuwa hana chochote cha kuwabeba, basi wakarudi na kukaa kwa muda, kisha wakaletewa ngamia watatu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawatumia wale mabwana, baadhi yao wakaambiana: Mwenyezi Mungu asitubariki kwa ngamia hawa; Kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliapa kutotubeba, basi wakamjia na wakamuuliza, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Aliyekubebeni ni Mwenyezi Mungu Mtukufu; Kwa sababu yeye ndiye aliyetoa ufanikishaji na akaruzuku, lakini mimi ni sababu ya haya kutokea kupitia mikono yangu, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Wallahi, akipenda Mwenyezi Mungu, sitaapa kufanya au kuacha chochote, na nikaona kuwa kisichokuwa kiapo hicho ni heri na bora zaidi, isipokuwa nitafanya lililo bora zaidi, na kuyaacha niliyoapa, na ninalipa kafara ya kiapo changu.
Kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mtu anayepigana kwa kutaka kuonekana jasiri, na anayepigana kwa hamasa za ukabila, au anayepigana kwa kutaka kuonekana. Ni yupi kati ya hao anayepigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: “Mwenye kupigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, basi huyo yuko katika Njia ya Mwenyezi Mungu."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume rehema na amani ziwe juu yake aliulizwa kuhusu kutofautiana kwa malengo ya wapiganaji hao; mwenye kupigana kwa kutaka kuonekana jasiri, au kwa hamasa, au ionekane nafasi yake kati ya watu, au mengineyo, ni lipi kati ya haya lipo kwa ajili ya Allah? Akaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu ni yule anayepigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu.