





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa Kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- yakwamba yeye alimsikia mtu mmoja akisema: Hapana! naiapia Al-ka'aba, akasema bin Omar: Hakuapiwi kinyume na Mwenyezi Mungu, kwani mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atayeapa kinyume na Mwenyezi Mungu basi atakuwa amekufuru au kafanya ushirikina"
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu na majina yake na sifa zake basi atakuwa kamkufuru Mwenyezi Mungu au kafanya ushirikina; kwa sababu kiapo humaanisha kutukuzwa mwenye kuapiwa, na utukufu ni wa Allah pekee; hakuapiwi ila kwa Allah na majina yake na sifa zake kutakasika machafu ni kwake. Na kiapo hiki ni katika shirki ndogo; lakini ikiwa muapaji atakitukuza alichokiapia kama anavyomtukuza Allah Mtukufu au zaidi; basi hapo itakuwa katika ushirikina mkubwa.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika swala nzito zaidi kwa wanafiki ni swala ya Ishaa na swala ya Alfajiri, na lau kama wangejua (malipo) yaliyomo, basi wangeziendea hata kwa kutambaa, na nilipania niamrishe swala ikimiwe(kusimamishwa), kisha nimuamrishe mtu mmoja awasalishe watu, kisha niondoke pamoja na wanaume wakiwa wamebeba mizigo ya kuni tuelekee kwa watu ambao hawahudhurii swala, ili niwachome na moto wakiwa ndani ya majumba yao".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu wanafiki na uvivu wao wa kuhudhuria swala, hasa hasa swala mbili, Ishaa na Alfajiri, nakuwa laiti wangelijua kiwango cha malipo na thawabu katika kuzihudhuria swala hizo pamoja na jamaa ya waislamu, basi wangeliziendea hata kwa kutambaa mfano wa kutambaa kwa mtoto kwa mikono na magoti. Bila shaka aliazimia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aamrishe swala ikimiweisimamishwe), na amuweke mtu awasalishe watu badala yake, kisha aondoke akiwa pamoja na watu watakaombebea mizigo ya kuni kwenda kwa watu wasiohudhuria swala ya pamoja (Jamaa) ili awachome wakiwa ndani ya majumba yao; kwa sababu ya ubaya wa waliyoyafanya katika madhambi, -lakini hakufanya hivyo- kwa sababu ndani ya majumba yao kuna wanawake na watoto wasio na hatia, na wengineo miongoni mwa wenye udhuru, wasiokuwa na dhambi.
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika katika watu waovu zaidi ni wale watakaokutwa na Kiyama wakiwa hai, na mwenye kuyafanya makaburi kuwa mahala pa kusalia".
Imepokelewa na AhmadAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu watu waovu, nakuwa hao ndio Kiyama kitasimama juu yao, na wale wanaoyafanya makaburi kuwa misikiti, wakisali hapo na wakiyaelekea wakati wa ibada.
Imepokelewa kutoka kwa Mahmud bin Labid -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika ninachokiogopea zaidi juu yenu ni shirki ndogo" Wakasema: Ni ipi shirki ndogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni riyaa (kujionyesha), atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama kuwaambia, pindi watu wote watakapolipwa kwa matendo yao: 'Nendeni kwa wale mliokuwa mkijionyesha kwao duniani, mtazame je mtapata kwao malipo?".
Imepokelewa na AhmadAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa jambo kubwa zaidi analoliogopea juu ya umma wake: Ni shirki ndogo nayo; ni mtu kufanya kwa ajili ya watu. Kisha akaeleza kuhusu adhabu ya wenye kujionyesha siku ya Kiyama kwa kuambiwa: Nendeni kwa wale mliokuwa mkifanya kwa ajili yao, mkatazame je wanamiliki malipo na thawabu za kukupeni kwa amali hiyo?!.
Kutoka kwa Adiy bin Hatim-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na Amani ziwe juu yake Akisoma aya hii: "Wamewafanya wanachuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu kinyume na Mwenyezi Mungu na Masihi mwana wa Mariam, na hawakuamrishwa ila ni kumuabudu Mungu mmoja, hapana Mola ispokuwa yeye, ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo" Nikasema kumwambia: Hakika sisi hatuwaabudu wao, Akasema: "Kwani hawaharamishi aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayaharamisha? na wanahalalisha aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayahalalisha? Nikasema: Ndivyo, Akasema: Basi huko ndiko kuwaabudu".
Imepokelewa na Imamu TirmidhiyAliposikia swahaba huyu mtukufu kisomo cha Mtume rehema na Amani zimfikie cha Aya hii ambayo ndani yake kuna habari kwa Mayahudi na wakristo: kuwa wao wamewafanya wanachuoni wao na wachamungu wao kuwa miungu, wanawawekea sheria zinazokwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu na wakawatii juu ya hilo, ikamtatiza maana yake, kwasababu yeye alikuwa akidhania kuwa ibada inaishia katika kusujudu na mfano wake, Mtume rehema na Amani zimfikie akambainishia- kuwa katika kuwaabudu wanachuoni na watawa: ni kuwatii katika kuhalalisha haramu na kuharamisha halali, kinyume na hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake rehema na Amani zimfikie.
Imepokelewa Kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Alisema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Muadhi Ibn Jabal, alipomtuma kwenda Yemen: "Hakika wewe utaiendea jamii ya watu wa kitabu (Mayahudi na Wakristo), utakapowajia basi waite kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Ikiwa watakutii kwa hilo, basi waeleze kuwa Mwenyezi Mungu amewalazimisha juu yao swala tano katika kila usiku na mchana, ikiwa watakutii kwa hilo, basi waeleze kuwa Mwenyezi Mungu amewalazimisha juu yao zaka, huchukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kurudishwa kwa mafukara wao, ikiwa watakutii kwa hilo, basi jiepushe na mali zao za thamani, na ogopa maombi ya mwenye kudhulumiwa, kwani maombi hayo hayana baina yake na Mwenyezi Mungu kizuizi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlipomtuma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Muadhi Ibn Jabal -Radhi za Allah ziwe juu yake- kwenda katika miji ya Yemen kama mlinganizi wa kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu na kama mwalimu, alimuweka wazi kuwa atakumbana na jamii ya Wakristo; ili awe na maandalizi, kisha aanze katika kuwaita kwake na mambo muhimu zaidi kisha yanayofuatia, Atawaita kurekebisha itikadi kwanza; washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu; Kwa sababu wao kwa itikadi hiyo yakuwa hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake; wataingia katika Uislamu, ikiwa watatii hilo basi awaamrishe wasimamishe swala; kwani huo ndio wajibu mkubwa baada ya tauhidi, Watakapoisimamisha awaamrishe matajiri wao kutoa zaka ya mali zao kuwapa mafukara wao, kisha akamtahadharisha na kuchukua mali bora; kwa sababu ya wajibu ni mali ya kati na kati, Kisha akamuusia aiepuke dhulma; asijekumuombewa dua mbaya aliyemdhulumu, kwani dua yake hupokelewa.
Kutoka kwa Jaabir radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-Yakwamba Mtume rehema na Amani zimfikie aliulizwa kuhusu Nushra (kutibu uchawi kwa uchawi)? Akasema: Hiyo ni katika kazi za shetani.
Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na AhmadNikuwa Mtume rehema na Amani ziwe juu yake - Aliulizwa kuhusu kumtibu aliyerogwa kwa njia ambayo walikuwa wakiijua tangu zama za ujinga, mfano: kuondoa uchawi kwa uchawi ni ipi hukumu ya hilo, akajibu rehema na Amani zimfikie kuwa hiyo ni katika kazi za shetani, au hufanyika kupitia yeye; kwasababu inakuwa kwa aina ya uchawi na kwa kuwatumia mashetani, hiyo ni ushirikina na ni haramu. na ama kutibu uchawi kunakofaa: ni kuufungua uchawi kwa kisomo cha ruqya au kuutafuta, na kuufungua kwa mkono pamoja na kusoma Qur'ani au kwa dawa za halali.
Imepokelewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Msichupe mipaka katika kunisifu, kama walivyochupa mipaka Wakristo kwa mwana wa Mariam; Bila shaka, mimi ni mja wake, na semeni: Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAnakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kupitiliza na kuvuka mpaka wa kisheria katika kumsifu, na kumsifu kwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu na matendo yake ambayo ni yake pekee, au kusema kuwa anajua mambo yaliyo jificha, au anastahiki kuombwa pamoja na Mwenyezi Mungu, kama walivyofanya Wakristo kwa Issa mwana wa Mariam -Amani iwe juu yake- Kisha akaweka wazi kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu, na akaamrisha tuseme kuhusu yeye: Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake.
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Palisemwa ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni mtu gani atakayepata furaha zaidi ya uombezi wako siku ya Kiyama? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Nilijua kuwa ewe Abuu Huraira hatoniuliza mwingine hadithi hii kabla yako, kwa kile nilichokiona kwako, pupa yako juu ya hadithi, Mtu atakayepata furaha zaidi ya uombezi wangu siku ya Kiyama, ni yule atakayesema Laa ilaaha illa llah (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu), kwa kutakasa nia toka moyo mwake au nafsi yake".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mtu mwenye furaha zaidi kuliko wote kwa uombezi wake siku ya Kiyama ni yule atakayesema: "Laa ilaaha illa llaah kwa kutakasa nia toka moyoni mwake" Yaani: Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na asalimike na ushirikina na riyaa(kufanya mambo kwa kujionesha).