





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abuu Qatada As-sulami Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi asali rakaa mbili kabla hajakaa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmemhimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mwenye kuja msikitini na akaingia katika wakati wowote, na kwa lengo lolote, asali rakaa mbili kabla hajakaa, nazo ni rakaa mbili za salamu ya msikiti.
Kutoka kwa Abuu Humaidi au kutoka kwa Abuu Usaidi Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi aseme: Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako)".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeuelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake katika dua ambayo husemwa wakati wa kuingia msikitini: "Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu amuandalie sababu za kupata rehema zake, na akitaka kutoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako), amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe katika fadhila zake na ziada ya hisani zake miongoni mwa riziki ya halali.
Kutoka kwa Salim bin Abil Ja'di amesema: Mtu mmoja alisema: Laiti ningeswali nikastarehe, wakawa kana kwamba wamelitia dosari hilo, akasema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ewe Bilali, simamisha swala, tupe raha kwayo".
Imepokelewa na Abu DaudAkasema mtu mmoja katika Masahaba: Laiti ningeliswali nikastarehe, waliokuwa naye waka kana kwamba wamemuabisha kwa hilo, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Ewe Bilali! Nyanyua adhana na simamisha swala; ilitustarehe kwayo; na hii ni kwa sababu ndani yake kuna kuzungumza na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na raha ya roho na moyo.
Kutoka kwa Abuu Hazim bin Dinari: Anasimulia kuwa watu fulani walikuja kwa Sahli bin Sa'di As-saaidi, wakiwa wamepatwa na shaka kuhusu mimbari (ya Mtume) ilitengenezwa kwa mti gani, wakamuuliza kuhusu hilo, akasema: Wallahi mimi ninajua imetokana na mti gani, na niliiona tangu siku ya kwanza ilipowekwa, na siku ya kwanza kuikalia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, aliagiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa fulani -Mwanamke aliyekuwa mke wa mmoja kati ya Maanswari (Watu wa Madina) -Sahli alimtaja kwa jina lake-: "Muamrishe kijana wako seremala anitengenezee kibao niwe nakalia ninapo zungumza na watu", akamuamrisha akatengeneza kutokana na mti wa Twarfa (Mti mfano wa mkaratusi) hupatikani msituni, kisha akaileta, yule mama akaiagiza kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akaamrisha ikawekwa hapa, kisha nikamuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa juu yake na akatoa takbira (Allahu Akbaru) akiwa juu yake, kisha akarukuu akiwa ju yake, kisha akashuka kinyumenyume akasujudu mwishoni mwa mimbari, kisha akarudi, alipomaliza swala yake akawageukia watu kisha akasema: "Enyi watu! Bila shaka nimefanya hivi ili muige na mjifunze swala yangu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeWalikuja baadhi ya watu kwa mmoja kati ya Masahaba wakimuuliza kuhusu Mimbari ya Mtume aliyoitumia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ilitengenezwa kwa kitu gani? Na walikuwa wamekwisha bishana na kuzozana katika hilo, akawaeleza kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-aliagiza kwa mwanamke wa ki Answari alikuwa na mtumishi seremala, akamwambia: Mwamrishe kijana wako anitengenezee Mimbari nikalie wakati nikizungumza na watu, mama yule akakubali ombi hilo, na akamuamrisha kijana wake amtengeneze Mimbari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokana na mti wa Twarfaa (Mti mfano wa mkaratusi), kijana alipomaliza kazi, yule mama aliaigiza kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mtume akaamrisha iwekwe mahala pake msikitini, kisha akaswali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa juu yake, na akatoa takbira akiwa juu yake, kisha akarukuu akiwa juu yake, kisha akashuka akiwa anatembea kwa nyuma bila ya kugeuka kutazama nyuma, akasujudu mwishoni mwa Mimbari, kisha akarudi, alipomaliza swala akawageukia watu, na akasema: Enyi watu!, Bila shaka nimefanya hivi ili muige na mjifunze swala yangu.
Kutoka kwa Hittwan bin Abdillah Ar-Raqashi amesema: Nilisali pamoja na Abuu Mussa Al-Ash'ariy swala moja, tulipofika katika kikao (cha tahiyatu) mtu mmoja akasema: Swala imefungamanishwa na wema na zaka, akasema: Abuu Mussa alipomaliza swala na akatoa salamu, akageuka na akasema: Ni nani kati yenu aliyesema neno kadhaa wa kadhaa? Akasema: Watu wote wakanyamaza, kisha akasema: Ni nani kati yenu aliyesema neno kadhaa wa kadhaa? Watu wote wakanyamaza, akasema: Huenda ukawa ni wewe uliyesema ewe Hittwan? Akasema: Hakika niliogopa utaninyamazisha kwa neno hilo, akasema mtu mmoja katika jamaa waliokuwepo: Mimi ndiye niliyesema, na sikukusudia kwa neno hilo ila kheri, Abuu Mussa akasema: Hivi hamjui ni vipi mtasema ndani ya swala zenu? hakika Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alituhutubia na akatubainishia sunna zetu na akatufundisha swala yetu, akasema: "Pindi mtakaposwali basi nyoosheni safu zenu, kisha akuongozeni mmoja wenu, atakapotoa takbira basi toeni takbira, na anaposema: "Ghairil maghdhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" [Suratul Fatiha: 7], basi semeni: Aaamiin (Ewe Mola wetu Mlezi tukubalie maombi) Atakujibuni Mwenyezi Mungu, atakapotoa takbira na akarukuu basi nanyi toeni takbira na mrukuu, kwani imamu anatakiwa kurukuu kabla yenu, na anyanyuke kabla yenu", akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:"Hiyo itakwenda na ile, na akisema: Samia'llaahu liman hamidah, semeni: Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, Mwenyezi Mungu anakusikieni, kwani Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- alisema kupitia ulimi wa Nabii wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi, na akitoa takbira akasujudu basi sujuduni, kwani imamu anatakiwa asujudu kabla yenu na anyanyuke kabla yenu", akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hiyo inakwenda ile, na akifika mahali pa kukaa basi kauli ya mwanzo ya mmoja wenu iwe ni: Attahiyyatut twayyibaatu as swalawaatu lillaah, assalaam alaika ayyuhan nabiyyu warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu alainaa wa alaa ibaadillaahis swaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu wa ash-hadu anna Muhammadan abduhu warasuuluhu".
Imepokelewa Imamu MuslimSwahaba Abuu Mussa Al-Ash'ary -Radhi za Allah ziwe juu yake- alisali swala moja, alipofika katika kikao cha tahiyatu ambacho kinatashahudi, mtu mmoja akasema miongoni mwa wasaliji walioko nyuma yake: Swala imeunganishwa ndani ya Qur'ani na wema na zaka, Abuu Mussa -Radhi za Allah ziwe juu yake- alipomaliza swala aliwageukia maamuma, akawauliza: Ni nani kati yenu aliyesema neno: Swala imeunganishwa ndani ya Qur'ani na wema na zaka?!, Watu wote wakanyamaza, na hakuzungumza yeyote kati yao, akarudia kuwauliza swali mara nyingine, alipoona hakuna alliyemjibu, Abuu Mussa -Radhi za Allah ziwe juu yake- akasema: Huenda ukawa ni wewe Hittwan ndiye uliyesema! Kwa ujasiri wake na ukaribu wake kwake, na mahusiano yake kwake, jambo ambalo haliwezi kupelekea kumtuhumu, na ili ampe msukumo msemaji wa uhakika kukiri, Hittwan akalikanusha hilo, na akasema, nilihofia unaweza kunikaripia kwa kudhani kuwa mimi ndiye niliyesema; na hapa sasa yule bwana akazungumza: Mimi ndiye niliyesema, na sikukusudia ila jambo la kheri, Abuu Mussa akasema kwa kumfundisha: Hivi hamjui ni nini mtasema ndani ya swala yenu?! Alisema hivi kwa kukemea kitendo hicho, kisha Abuu Mussa akaeleza kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwahutubia siku moja, akawabainishia sheria zao, na akawafundisha swala yao, akasema -Rehema na amani ziwe juu yake-: Mtakaposali basi nyoosheni safu zenu, na mlingane sawa, kisha mmoja miongoni mwao awasalishe watu, imamu atakapotoa takbira ya kuhirimia swala, basi toeni takbira mfano wake, na akisoma suratul Fatiha na akafikia: "Ghairil magh-dhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" [Fatiha: 7], Semeni: Aaamiin; mkifanya hivyo Mwenyezi Mungu atakujibuni maombi yenu, akitoa takbira na akarukuu basi toeni takbira na mrukuu; kwani imamu anarukuu kabla yenu na ananyanyuka kabla yenu msimtangulie; kwa sababu mahali alipowatangulia imamu ni katika kuwatangulia kurukuu, kutamalizika kwa kuchelewa kwenu kidogo baada ya yeye kunyanyuka kidogo, kitambo hicho kidogo kitapishana kidogo na kunyanyuka kwake, na hapo kiwango cha rukuu yenu kitakuwa sawa na rukuu yake, na imamu akisema: Samiallaahu liman hamidah, basi semeni: Allaahumma Rabbanaa walakal hamdu, waswaliji wakisema hivyo basi hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anasikia dua zao na kauli zao, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema kwa ulimi wa Nabii -Rehema na amani ziwe juu yake-:Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumuhimidi, kisha imamu akitoa takbira na kusujudu basi na maamuma wanatakiwa kutoa takbira na kusujudu, kwani imamu anatakiwa asujudu kabla yao, na anyanyuke kabla yao, kiwango hicho kidogo cha kusubiri kitakuwa sawa na kiwango chake, na hapo kiwango cha maamuma kitakuwa sawa na kiwango cha imamu, ana akifika katika kikao cha tahiyatu, na iwe kauli ya mwanzo ya mwenye kusali ni: "Attahiyyatut twayyibaatu asswalawaatu lillaah" Ufalme na kubakia na utukufu wote unamstahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, na vile vile swala tano zote ni za Mwenyezi Mungu, "Assalaamu alaika ayyuhan nabiyyu warahmatullaahi wabarakaatuh", "Assalaamu alainaa walaa ibaadillaahis swaalihiin, muombe Mwenyezi Mungu akusalimishe na kila aibu na maafa, na mapungufu na maovu; na tunamtaja Muhammadi pekee kwa kumtakia amani, kisha tunajitakia amani wenyewe, kisha tunawatakia amani waja wema wa Mwenyezi Mungu wale wenye kutekeleza haki zilizo juu yao za Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za waja wake, kisha tunashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na tunashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na Mtume wake.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Anasimulia yakuwa yeye alikuwa akitoa takbira katika swala zote za faradhi na zinginezo, ndani ya ramadhani na nje ya ramadhani, anatoa takbira anaposimama, kisha anatoa takbira wakati anarukuu, kisha anasema: Sami'allaahu liman hamidah, kisha anasema: Rabbanaa walakal hamdu, kabla hajasujudu, kisha anasema: 'Allaahu Akbaru' wakati anapoporomoka kwenda kusujudu, kisha anatoa takbira wakati ananyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, kisha anatoa takbira wakati anasujudu, kisha anatoa takbira wakati ananyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, kisha anatoa takbira wakati ananyanyuka kutoka katika kikao kwenda katika rakaa ya pili, na anafanya hivyo katika rakaa zote, mpaka anamaliza swala, kisha anasema anapomaliza swala: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi ndiye mtu niliyekaribu zaidi kwenu nyinyi swala yangu kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, bila shaka hii ndio ilikuwa swala yake mpaka alipoondoka duniani.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAbuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- anapokea sehemu katika sifa ya swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na anaeleza kuwa alipokuwa akisimama katika sala anatoa takbira wakati ananyanyuka, nayo ni takbira ya kuhirimia swala, kisha anatoa takbira wakati anahama kwenda katika rukuu, na wakati anasujudu, na wakati anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, na wakati anasujudu sijida ya pili, na anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida hiyo, na anaponyanyuka katika rakaa mbili za mwanzo baada ya kikao cha tashahudi ya kwanza katika swala yenye rakaa tatu au nne, kisha anafanya hivyo katika swala nzima mpaka anamaliza, na alikuwa akisema anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu: Sami'allaahu liman hamidah, kisha anasema akiwa wima: Rabbanaa lakal hamdu. Kisha anasema Abuu Huraira wakati anapomaliza swala: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi swala yangu iko karibu zaidi kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- zaidi yenu, bali hii ndio ilikuwa sifa ya sala yake mpaka alipoondoka duniani.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni yule anayeiba swala yake" Akasema: Ataiba vipi swala yake? Akasema: "Hatimizi rukuu zake wala sijida zake".
Imepokelewa na Ibnu HibanAnabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwizi mbaya zaidi kuliko wote ni yule anayeiba swala yake; na hii ni kwakuwa; kuchukua mali ya mtu mwingine huenda mtu akanufaika nayo duniani, tofauti na mwizi huyu, kwa sababu kaiba haki ya nafsi yake katika thawabu na malipo, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na vipi mtu anawezaiba kutoka katika swala yake? Akasema: Kwa kutotimiza rukuu zake wala sijida zake; na hii ni pale anapofanya haraka kutoka katika rukuu na sijida, hazileti katika namna ya ukamilifu.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Aufaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu anasema: "Sami'allaahu liman hamidah, Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati wamil al Ardhwi wamil amaashi ita min shai in ba'ad".
Imepokelewa Imamu MuslimAlikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuuu ndani ya swala, anasema: " Sami'allaahu liman hamidah", Yaani: Atakayemhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamjibu, na atakubali himidi zake na atamlipa, kisha atamhimidi kwa kusema: Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati, wamil al Adhwi wamil amaa shi ita min shai in baad", himdi zenye kujaza mbingu na ardhi na vilivyo kati yake, na zinajaza ayatakayo Mwenyezi Mungu.
Kutoka kwa Warraadi mwandishi wa Mughira amesema: Alinisomea Mughira bin Shu'ba katika kitabu kilichoandikwa kwenda kwa Muawia: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikua akisema mwishoni mwa kila swala ya faradhi: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul mulku walahul hamdu, wahuwa a'laa kulli shai in qadiir, Allaahumma laa maania limaa a'twaita walaa mu'twiya limaa mana'ta, walaa yanfa'u dhal jaddi minkal jaddu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema kabla kidogo ya mwisho wa kila swala ya faradhi: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul mulku walahul hamdu, wahuwa a'laa kulli shai in qadiir, Allaahumma laa maania limaa a'twaita walaa mu'twiya limaa mana'ta, walaa yanfa'u dhal jaddi minkal jaddu" Yaani: Nina kiri na kulikubali neno la kumpwekesha Allah, la Laa ilaaha illa llaah, -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah-, ibada ya kweli naithibitisha kwa Mwenyezi Mungu, na ninaikanusha kwa asiyekuwa yeye, hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allah, na ninakiri kuwa ufalme wa kweli uliotimia ni wa Mwenyezi Mungu, na sifa zote za viumbe wa mbinguni na ardhini zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, kiasi kwamba yeye ndiye muweza juu ya kila kitu, na aliyoyakadiria Mwenyezi Mungu katika vipawa au kunyimwa hakuna awezaye kuyazuia, na hapo basi utajiri hauwezi kumsaidia mwenye nao, bali kinachoweza kumfaa ni amali zake.