





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake na alikuwa kapigana vita pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- takriban vita kumi na mbili (12) anasema: Nilisikia mambo manne kutoka Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, yakanifurahisha sana, anasema: "Asisafiri mwanamke mwendo wa siku mbili mpaka awe pamoja na mume wake, au maharimu yake (Ndugu asiyeweza kumuoa), hakuna kufunga ndani ya siku mbili: Idil Fitri na Idil Adh-ha, na hakuna swala baada swala ya Asubuhi mpaka lichomoze jua, na wala baada ya Lasiri mpaka lizame, na wala haifungwi safari isipokuwa katika misikiti mitatu: Msikiti mtukufu (wa Makka), na Msikiti wa Aqswa (Palestina), na msikiti wangu huu (Madina)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mambo manne: La kwanza: Kamkataza mwanamke kusafiri mwendo wa siku mbili bila kuwa na mume wake au mmoja kati ya maharimu wake, naye ni mtu aliyeharamu kwake kumuoa uharamu wa moja kwa moja (usio wa moja kwa moja, kama mume wa dada yake) kama mwanaye, na baba, na mtoto wa kaka, na kijana wa dada, na baba mdogo au mkubwa, na mjomba, na mfano wake. La pili: Katazo la kufunga siku Idil Fitri na siku ya Idil Adh-ha, sawa sawa muislamu amezifunga kwa udhuru au kwa kujitolea, au kafara. La tatu: Amekataza kusali swala ya sunna baada ya swala ya Lasiri mpaka lizame Jua, na baada ya kuchomoza asubuhi mpaka lichomoze Jua. La nne: Katazo la kusafiri kwenda eneo katika maeneo kwa itikadi kuwa kuna ubora, na kuitakidi kuwa kuna kulipwa malipo mengi, isipokuwa misikiti hii mitatu, hivyo hakuna kufunga safari kwenda misikiti isiyokuwa hiyo kwa ajili kuswali ndani yake, kwani malipo hayalipwi kwa wingi isipokuwa katika misikiti hii mitatu, Msikiti mtukufu (wa Makka), na Msikiti wa Mtume (Madina), na Msikiti wa Aqswa (Palestina).
Kutoka kwa Ukba bin Aamir Al-Juhani radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nyakati tatu alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitukataza kuswali ndani yake, au kuzika ndani yake maiti wetu: wakati linapoanza kuchomoza jua mpaka linyanyuke, na wakati linapofika kati kati mpaka lipinde, na wakati linapoanza kuzama mpaka lizame.
Imepokelewa Imamu MuslimAmekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyakati tatu za mchana kutoswali ndani yake swala za sunna, au kuzikwa ndani yake maiti: Wakati wa kwanza: Wakati linapodhihiri jua kwa kuchomoza, na hii ni wakati wa mwanzo wa kuchomoza kwake mpaka linyanyuke kiasi cha mkuki, na inakadiriwa kuwani robo saa takribani. Wakati wa pili: Pindi jua linapofika kati kati ya mbingu, linapokuwa halina kivuli upande wa Mashariki au Magharibi mpaka linapoondoka kutoka kati kati ya mbingu, na kikaonekena kivuli upande wa Mashariki, wakati ambapo unaanza wakati wa Adhuhuri, nao ni wakati mfupi mno; ambao ni kiasi cha dakika tano takribani. Wakati wa tatu: Linapopinda na likaanza kuzamia Magharibi mpaka lizame.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Asiswali mmoja wenu katika nguo moja ambayo hakuna chochote mabegani mwake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuswali katika nguo moja kutoyaacha wazi mabega yake na shingo yake kiasi kwamba haweki chochote chenye kumsitiri; kwa sababu mabega mawili hata kama si uchi; ila kuyasitiri yanawezekana wakati wa kusitiri uchi, na ni jambo lililo karibu na kumheshimu na kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kusimama mbele yake katika swala.
Imepokelewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hivi wana nini watu! wananyanyua macho yao mbinguni ndani ya swala zao", ikazidi ukali kauli yake katika hilo, mpaka akasema: "Hakika, ni ima waache kufanya hivyo, au yatapofuliwa macho yao".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAliwatahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wale wanaonyanyua macho yao mbinguni ndani ya swala wakati wa dua au kinginecho, kisha karipio lake likawa kali na akatangaza adhabu rehema na amani ziwe juu yake kwa wanaofanya hivyo kwamba yanahofiwa macho yao kupofuliwa na yakanyakuliwa kwa haraka kwa namna wasiyoitarajia, wakajikuta tayari wamepoteza neema ya macho.
Kutoka kwa Suhaib -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Utakaposujudu basi weka viganja vyako, na unyanyue viwiko vyako".
Imepokelewa Imamu MuslimAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya mikono miwili katika sijida ya swala, nayo ni kwa kuviweka vizuri viganja vyake katika ardhi na aviweke vidole vikiwa vimefungamanishwa kuelekea kibla, na viwe viwiko viwili -maungio ya mkono na muundi wake- viwe vimenyanyuka na viko mbali na kugusa Ardhi, na vimeachanishwa na mbavu.
Kutoka kwa Waili bin Hujari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Niliswali pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa akitoa salaam kuliani kwake: "Assalaam alaikum warahamatullah wabarakaatuh", na kushotoni kwake: "Assalaam alaikum warahmatullah".
Imepokelewa na Abu DaudAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kumaliza swala yake anatoa salaam kuliani kwake na kushotoni kwake kwa kugeuka kwa uso wake upande wa kulia, pamoja na kusema: "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", na anatoa salaam kushotoni kwake, kwa kugeuza uso wake upande wa kushoto, pamoja na kusema: "Assalaam alaiku warahmatullah".
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakaye msabihi Mwenyezi Mungu mwisho wa kila swala mara thelathini na tatu (33), na akamhimidi Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu (33), na akamtukuza Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu, hizo ni tisini na tisa (99) Na akasema ili kukamilisha mia moja (100): Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku walahul hamdu, wahuwaa'laa kulli shai in qadiir, basi yatasamehewa madhambi yake, hata kama yalikuwa na wingi mfano wa povu la Bahari".
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema baada ya kumalizika kwa swala za faradhi: Mara thelathini na tatu (33): (Sub-haanallaah) Nako ni kumtakasa Mwenyezi Mungu dhidi ya mapungufu. Na mara thelathini na tatu (33): (Alhamdulillaah) Nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu kwa sifa kamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza. Na mara thelathini na tatu (33): (Allaahu Akbar) Nayo ni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkuu na Mtukufu kuliko kila kitu. Na kwa kukamilisha idadi ya mia moja (100) "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku, walahul hamdu, wahuwa alaa kulli shai in-Qadiir" Na maana yake: Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yeye pekee asiye na mshirika, nakuwa Yeye Mtukufu ndiye alipwekeka kwa Ufalme kamilifu, na ndiye mwenye kustahiki kutukuzwa na sifa pamoja na mapenzi na kukwezwa pasina mwingine, nakuwa Yeye ni muweza hakuna kinachomshinda. Yeyote atakayesema hivyo, dhambi zake zitafutwa na kusamehewa, hata zikiwa nyingi, kama povu jeupe litokalo juu ya bahari inapochafuka na kutibuka.
Kutoka kwa Abuu Umama -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayesoma Ayatul Kursiy mwisho wa kila swala ya faradhi hakuna kitakachomzuia kuingia peponi isipokuwa kufa".
Imepokelewa na Nasai katika kitabu AlkubraaMtume rehema na amani ziwe juu yake amesema kuwa mwenye kusoma Ayatul-Kursi baada ya kumalizika kwa swala ya faradhi, hakuna kitakachomzuia kuingia Peponi isipokuwa kifo; nayo iko katika Suratul Baqarah, Mwenyezi Mungu anasema: "Mwenyezi Mungu - hapana mungu isipokuwa Yeye, Aliye hai, Msimamizi wa mambo yote milele. Hashikwi na kusinzia wala kulala. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo duniani. Ni nani huyo awezaye kufanya uombezi mbele yake isipokuwa kwa idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao, na yaliyo nyuma yao, wala wao hawajui vyema chochote katika elimu yake isipokuwa kwa kile akitakacho. Kuti chake cha enzi kimeenea mbingu na dunia, na wala halemewi na kuvilinda vyote viwili. Na Yeye ndiye aliye juu zaidi, Mkuu." [Al-Baqara: 255]
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapopata shaka mmoja wenu katika swala yake, akawa hajui kaswali rakaa ngapi tatu au nne? Basi aachane na shaka na ajenge yakini (uhakika), kisha atasujudu sijida mbili kabla hajatoa salamu, ikiwa atakuwa kaswali rakaa tano basi zitamtetea katika swala yake, na kama aliswali kukamilisha nne; basi hiyo itakuwa ni kumvunja moyo shetani."
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ikiwa mwenye kuswali atasita katika swala yake na akashindwa kujua ameswali rakaa ngapi, tatu au nne? Hebu aondoe idadi iliyozidi yenye shaka na asiihesabu; tatu ndiyo ana uhakika nazo, basi ataswali rakaa ya nne, kisha atasujudu sijida mbili kabla ya kutoa salamu. Ikiwa aliswali nne kweli; basi zitakuwa tano kwa kuongeza rakaa moja, na sijida mbili za kusahau zitakuwa ni mbadala wa rakaa moja, basi idadi itakuwa ni shufa si witiri, na ikiwa kaswali rakaa nne kwa rakaa iliyozidi; basi atakuwa katekeleza wajibu wake pasina kuongeza wala kupunguza. Sijida mbili za kusahau zilikuwa ni kumdhalilisha Shetani na kumshinda, na kumrudisha akiwa kafedheheka, na kashindwa kufikia lengo lake; Kwa sababu alimvurugia swala yake, na akataka kuiharibu, na ikakamilika swala ya mwanadamu alipotekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kusujudu, sijida ambayo Ibilisi aliasi, alipokataa kumtii Mwenyezi Mungu kwa kumsujudia Adamu.