





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini mwake basi na apenge kwa maji mara tatu, kwani Shetani hulala ndani ya tundu zake za pua".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnamuhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuamka kutoka usingizini mwake kuwa apandishe maji puani na kuyapenga mara tatu; ambako ni kuyatoa maji puani baada ya kuyaingiza, na hii ni kwa sababu Shetani hulala ndani ya tundu za pua - nayo ni pua yote -.
Kutoka kwa Jabiri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amenieleza Omari Bin Khattwab: Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: "Rudi katawadhe vizuri udhu wako" Akarudi, kisha akaswali.
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimuona mtu mmoja kamaliza kutia udhu wake, akaacha kiasi cha kucha moja katika kisigino chake, hakikupatwa na maji ya udhu, akasema kumwambia huku akiashiria sehemu palipo na mapungufu: Rudi katie vizuri udhu wako, na utimize na ukipe kila kiungo haki yake katika maji, yule bwana akarudi akatimiza udhu wake kisha akaswali.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiosha, au akioga, kwa kibaba kimoja mpaka vibaba vitano, na anatawadha kwa kibaba kimoja.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akioga janaba kwa kibaba kimoja mpaka vitano, na alikuwa akitawadha kwa kibaba kimoja. Na kibaba ujazo wake ni: mud nne, na mud moja ni: kiasi cha kujaza kiganja cha mtu mwenye mwili wa wastani.
Kutoka kwa Uqba bin Amir, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, amesema: “Tulikuwa na zamu ya kuchunga ngamia, basi ikafika zamu yangu nikawapeleka jioni, nikamkuta Mtume rehema na amni ziwe juu yake akiwa amesimama akiwahadithia watu, nikamkuta akiwa katika kauli yake: “Hakuna Muislamu anayetawadha na akautia vizuri udhu wake, kisha akasimama na kuswali rakaa mbili, akielekea kwa moyo wake na uso wake ndani ya rakaa hizo, isipokuwa Pepo itastahiki kwake.” Akasema, nikasema: Ni kheri iliyoje hii, mara ghafla nikasikia msemaji mmoja mbele yangu akisema: Ile ya kabla yake ndio ilikuwa bora, basi nikatazama, mara nikamuona ni Omari, akasema: Nimekuona umekuja hivi karibuni, akasema: “Hakuna yeyote kati yenu atakayetawadha vizuri - au akaukamilisha vizuri- kisha akasema: Nashuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, isipokuwa atafunguliwa milango minane ya Pepo, aingie mlango wowote autakao".
Imepokelewa Imamu MuslimAlibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati akiwaeleza watu fadhila mbili kubwa: Ya kwanza: Mwenye kutawadha vizuri, akaupendezesha vizuri udhu, na akaukamilisha, na akaukamilisha katika namna ilivyoelekezwa, na akakipa kila kiungo haki yake katika maji, kisha akasema: Nashuhudia ya kwamba hakuna mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake; Isipokuwa atafunguliwa milango minane ya Peponi, aingie mlango autakao. Pili: Mwenye kutawadha udhu huu kamili, kisha akasimama baada ya udhuu huu na kuswali rakaa mbili; Akiwa ameelekea ndani ya swala kwa moyo wake, kwa ikhlaswi na utulivu, na akanyenyekeza uso wake na viungo vyote vya mwili wake kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa Pepo itakuwa ni wajibu kwake.
Imepokewa kutoka kwa Anas -radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakapotawadha mmoja wenu na akavaa khofu zake (au soksi zake) basi na aswali nazo, na afute juu yake kisha asizivue akitaka kufanya hivyo isipokuwa atakapokuwa na janaba".
Imepokelewa na Addar- AlqutniAnabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu atakapovaa khofu zake baada ya kutawadha, kisha akatengukwa udhu baada ya hapo, na akataka kutawadha, basi anatakiwa afute juu yake akitaka kufanya hivyo, na aswali nazo wala asizivue kwa muda maalum, isipokuwa atakapopatwa na janaba hapo atalazimika kuvua khofu na kuoga.
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika swala ya Idil Adhaa au Fitri kwenda katika uwanja wa kuswali, akapita kwa wanawake, akasema: "Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini wenye kuweza kuteka moyo ya mwanaume makini kuliko nyinyi", Wakasema: Na ni upi upungufu wa dini yetu na akili zetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hivi kwani si ushahidi wa mwanamke mmoja ni sawa na ushahidi nusu wa mwanaume?" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Hilo ni katika upungufu wa akili yake, na je hivi akiingia katika hedhi si haswali wala hafungi" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Basi hilo ni katika upungufu wa dini yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika siku ya Iddi kwenda katika uwanja wa swala, na alikuwa kawaahidi wanawake kuwa atawatengea nafasi ya kuwapa mawaidha, akaitimiza siku hizo, na akasema: Enyi kundi la wanawake toeni sadaka, na zidishe kuomba msamaha; kwani mambo mawili hayo ni katika sababu kubwa za kufutiwa madhambi, kwani mimi nilikuoneni usiku niliopandishwa mbinguni mkiwa wengi motoni. Mwanamke mmoja miongoni mwao mwenye akili na mawazo mazuri na heshima, akasema: Kwani tuna nini sisi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mpaka tuwe wengi motoni? Akasema: Kwa sababu ya mambo kadhaa: Mnazidisha sana kulaani na matusi, na mnakanusha haki za waume. Kisha akawasifu kwa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: Sijapata kuona wenye mapungufu ya akili na dini wanaoweza kuwashinda wenye mioyo salama na akili na maamuzi na uwezo wa kutunza kumbukumbu zao kuliko nyinyi. Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni upi upungufu wa akili na dini? Akasema: Ama upungufu wa akili ni kuwa ushahidi wa wanawake wawili unalingana na ushahidi wa mwanaume mmoja; huu ndio upungufu wa akili, na upungufu wa dini, ni upungufu wa kufanya amali njema, kiasi ambacho mwanamke anakaa siku kadhaa haswali kwa sababu ya hedhi, na anafungua siku kadhaa za Ramadhani kwa sababu ya hedhi, na huu ndio upungufu wa dini, isipokuwa wao hawalaumiwi wala hawaandikiwi dhambi juu ya hilo; kwa sababu ni katika asili ya maumbile, kama ambavyo mwanadamu ameumbwa na asili ya kuipenda mali, na haraka katika mambo yake na ni mjinga.... na mengineyo, lakini alilitanabahisha hilo ikiwa ni tahadhari kwa wanaume wasifitinike nao.
Kutoka kwa mama Atwiya radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa kampa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: "Tulikuwa hatuchukulii maji maji ya kahawia na njano baada ya twahara kuwa ni chochote".
Imepokelewa na Abu Daud kwa matamshi haya, na amepokea Bukhari bila ya kuzidisha (baada ya kutwaharika)Ameeleza swahaba mama Atwiya radhi za Allah ziwe juu yake kuwa wanawake katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake walikuwa hawayazingatii maji maji yanayotoka katika tupu -ambayo yanaelekea katika weusi, au katika njano- baada ya kuona twahara ya kutoka katika hedhi: kuwa ni hedhi, hawaachi swala na swaumu kwa sababu yake.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Hakika mama Habiba bint Jahshi aliyekuwa chini ya Abdulrahman bin Auf alilalamika kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu damu, akasema kumwambia: "Kaa kiasi cha siku ambazo ilikuwa ikidumu hedhi yako, kisha oga". Akawa akioga kila wakati wa swala.
Imepokelewa Imamu MuslimAlilalamika mmoja kati ya Masahaba wa kike kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuendelea kushuka kwa damu yake, Akamuamrisha aache kuswali kwa kiwango cha siku alizokuwa akikaa hedhi yake kabla ya kushuka jambo hili lililojitokeza kwa dharura, kisha aoge na aswali, akawa akioga kwa hiyari kwa kila swala.
Kutoka kwa Amri Bin Suleim Al-Answari amesema: Ninamshuhudilia Abuu Saidi kuwa alisema: Ninamshuhudilia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwa alisema: "Kuoga siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila aliyebaleghe, na apige mswaki, na aguse marashi ikiwa atapata".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmebainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kuoga siku ya Ijumaa kumetiliwa mkazo ni sawa na wajibu upande wa kila aliyebalehe katika waislamu waliowajibikiwa na Ijumaa, Na asafishe meno yake kwa mswaki na mfano wake, na ajitie manukato kwa harufu yoyote nzuri ya uturi.