





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Maliki bin Ausi bin Hadathani yakuwa yeye alisema: Niligeuka nikasema ni nani anayechenji pesa? Twalha bin Ubaidillah akasema wakati akiwa kwa Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yao wote: Tuonyeshe Dhahabu yako, kisha tuletee, atakapokuja mfanyakazi wetu tutakupa pesa yako, akasema Omari bin Khattwab: Hapana, ni lazima utampa haki yake, au umrejeshee Dhahabu yake, kwani Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Fedha kwa dhahabu ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na ngano isiyokobolewa ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na shairi (ngano iliyokobolewa ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na tende kwa tende ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeTaabii (Mwanafunzi wa Maswahaba) Malik bin Ausi anaeleza kuwa alikuwa na dinari za dhahabu, na alitaka kuzibadilisha kwa dirham za fedha, basi Twalha bin Ubaidillah (radhi za Allah ziwe juu yake) akamwambia: Tupe dinari zako nizione! Kisha akamwambia baada ya kuamua kununua: Njoo kwetu ikiwa mtumwa wetu atakuja baadaye tutakupe dirham za fedha, Omari bin Khattab Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alilaani aina hii ya muamala (biashara), na akaapa kwa Twalha kuwa atalipa fedha sasa, au amrudishie dhahabu yake aliyoichukua yeye, akasema kuwa kuuza fedha kwa dhahabu, au kinyume chake, lazima kupokea kuwe mkono kwa mkono, vinginevyo biashara hiyo itakuwa ni riba iliyoharamishwa na uuzaji batili, Dhahabu haiuzwi kwa fedha, wala fedha kwa dhahabu, isipokuwa mkono kwa mkono, na kufanyike kubadilishana, wala haiuzwi kwa ngano, na shayiri kwa shayiri, na tende kwa mfano wake, kipimo kwa kipimo, mkono kwa mkono; na haijuzu kuachana katika makubaliano kabla ya kuimiliki.
Kutoka kwa Othman bin Abil Aswi Ath-thaqafi radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maumivu anayoyapata katika mwili wake tangu aliposilimu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: "Weka mkono wako juu ya mahala panapoumia katika mwili wako, na usema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mara tatu, na useme mara saba: Audhubillaahi wa quduratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru (Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kutokana na shari ya kile ninachokipata na kile ninachokihofia)"
Imepokelewa Imamu MuslimOthman bin Abil Aswi alipata maumivu makali ambayo yalikaribia kumuua, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaenda kumtembelea, na akamfundisha dua ambayo Mwenyezi Mungu atamuondolea maradhi yaliyomfika; nayo ni aweke mkono wake juu ya mahala panapoumia, na aseme: "Bismillaah" mara tatu, kisha aseme mara saba: "Ninataka kinga" na ninajikinga na kujiweka na kujilinda (kwa Mwenyezi Mungu na kudura zake kutokana na shari za yale ninayoyapata) katika maumivu ya wakati huu (na kuyahofia) na ninahofia kutokea maumivu mengine baadaye miongoni mwa huzuni na hofu, au kuendelea kwa maradhi na yakasambaa maumivu yake katika mwili.
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alikuwa Mtume wa Allah -rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu kuliko watu wote, na alikuwa mkarimu zaidi anapokuwa katika mwezi wa Ramadhani pindi anapokutana na Jibrili, na alikuwa akikutana naye katika kila usiku wa Ramadhani akimsomesha Qur'ani, basi hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na Amani ziwe juu yake- ni mkarimu zaidi kwa mambo ya kheri kuliko hata upepo uliotumwa.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa mkarimu zaidi kuliko watu wote katika mwezi wa Ramadhani, kiasi ambacho alikuwa akitoa kinachostahiki kumpa anayestahiki, na sababu ya kuzidisha ukarimu huu ni mambo mawili: La kwanza: Ni kukutana kwake na Jibril amani iwe juu yake. Na jambo jingine: Ni kuirejea Qur'ani, nayo ni kuisoma pasina kutazama mahali ilipoandikwa. Kwa hiyo Jibril, amani iwe juu yake, alisoma naye kila kilichoteremshwa katika Qur'ani, na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu zaidi, na ni mtenda kheri zaidi, na ni mwepesi wa kunufaisha viumbe kuliko upepo mzuri anaoutuma Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mvua na rehema.
Kutoka kwa Abuu Zuhairi Umara bin Ruaiba radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kamwe, hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali kabla ya kuchomoza Jua na kabla ya kuzama kwake"
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali swala ya Alfajiri, na swala ya Lasiri, na akadumu nazo; na amezitaja maalumu swala hizi mbili; kwa sababu ndizo swala nzito zaidi, na kwa sababu wakati wa Alfajiri huwa ni wakati wa usingizi na ladha yake, na wakati wa Lasiri huwa ni wakati wa kushughulishwa na kazi za mchana na biashara zake, na atakayezihifadhi swala hizi mbili pamoja na kupatikana tabu ndani yake, basi bila shaka ataweza kuzihifadhi swala zingine zilizobakia.
kutoka kwa Othmani Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kisha akaufanya vizuri udhu wake, na Unyenyekevu wake na Rakaa zake, isipokuwa inakuwa ni kifuta madhambi yaliyo kuwa kabla ya Sala, kwa muda ambao hajafanya madhambi makubwa, na hivyo ndivyo ilivyo kila siku".
Imepokelewa Imamu MuslimAnabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakuna muislamu atakayekutwa na wakati wa swala ya faradhi akatawadha vizuri udhu wake na ukaukamilisha, kisha akawa na unyenyekevu ndani ya swala yake kiasi kwamba ukawa moyo wake na viungo vyake vyote vimeelekea kwa Mwenyezi Mungu akivuta picha ya utukufu wake, na akatimiza vitendo vya swala kama rukuu na sijida na vinginevyo, isipokuwa swala hii itakuwa ni kifutio cha madhambi madogo madogo yaliyokuwa kabla yake, madam hajafanya dhambi katika madhambi makubwa, na fadhila hii ni endelevu kwa muda wote na katika kila swala.
Kutoka kwa Ka'b Bin Ujrah Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Adh-kari za baada ya sala ya faradhi hapati hasara msomaji au mfanyaji wake, kusema Sub-haana llahi mara thelathini na tatu (33), Al-hamdulillahi mara thelethini na tatu (33), Allahu Akbaru mara thelathini na nne (34)".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Adhkari (Dua) hatopata hasara wala kujuta msemaji wake, bali maneno haya yanathawabu, na yanakuja kwa kufuatana, na husemwa baada ya swala za faradhi, nayo ni: "Sub-haana llaah" -Ametakasika Mwenyezi Mungu- mara thelathini na tatu, yaani ametakasika Mtukufu na kila mapungufu. "Na Alhamdulillaah" Mara thelathini na tatu, nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu uliotimia pamoja na kumpenda na kumtukuza. "Allaahu Akbaru" Mara thelathini na nne, Mwenyezi Mungu ni mkubwa mno na ni Mtukufu na Mwenye nguvu kuliko kila kitu.
Kutoka kwa Sa'd Bin Abi Waqaas Allah amridhie kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayesema wakati anamsikia muadhini: Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Muhammadi kuwa ni Mtume na Uislamu kuwa ni dini, atasamehewa dhambi zake".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema wakati akimsikia muadhini "Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika wake", Yaani: Nina kiri na kukubali na ninatoa habari kuwa hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kila mwenye kuabudiwa kinyume na yeye ni batili, "Na kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake" Yaani: Yeye ni mja wala haabudiwi, na ni Mjumbe wake haongopi, "Nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi" Yaani: Kwa ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, "Na Muhammadi kuwa ni Mtume" Yaani: Kwa yote aliyotumwa kwayo, na akatufikishia, "Na Uislamu" Yaani: Kwa hukumu zote za Uislamu ikiwemo maamrisho na makatazo, "Dini" Yaani: Kwa itikadi na kutii, "Atasamehewa dhambi zake" Yaani: Katika dhambi ndogo.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika sisi tunasafiri Baharini, na tunabeba maji kidogo sana, tukiyatumia kutawadha tunakosa maji ya kunywa, je, tunaweza kutawadha kwa maji ya Bahari? Akasema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Ni safi Maji yake na ni halali mizoga yake".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadMtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hakika sisi tunapanda majahazi Baharini kwa ajili ya uvuvi au safari za kibiashara na mfano wa hayo, na tunabeba katika safari zetu maji kidogo katika maji yanayofaa kunywa, endapo tukiyatumia maji ya kunywa kwa udhu na kuoga basi yatamalizika, na hatutoweza kupata maji ya kunywa, je, inafaa kwetu sisi tutawadhe kwa maji ya Bahari? Akasema rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maji ya Bahari: Maji yake ni safi na yanaweza kusafisha kitu kingine; yanafaa kutawadha na kuoga, na ni halali kula vinavyotoka humo kama samaki na nyangumi na vinginevyo hata kama vitapatikana vimekufa na vinaelea juu yake pasina kuvuliwa.
Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema: Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maji, na vile vinavyoyaendea kama wanyama wa kawaida na wanyama pori, akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadAliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hukumu ya utwahara wa maji ambayo yanazungukiwa na wanyama wafugwao na wanyamapori kwa ajili ya kunywa na mfano wake, akasema rehema na amani ziwe juu yake kuwa: Maji yakifikia kipimo cha pipa mbili kubwa, ambazo zitakuwa na ujazo wa lita (210) basi hayo ni maji mengi hayawezi kunajisika; isipokuwa ikibadilika kwa najisi moja kati ya sifa zake tatu, rangi yake, au ladha yake au harufu.