





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Ubaada bin Swaamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Hana swala yeyote ambaye hakusoma sura kifunguzi cha kitabu (suratul faatiha)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa sala haikubaliki isipokuwa kwa kusoma suratul Fatiha, nayo ni nguzo miongoni mwa nguzo za swala, katika kila rakaa.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakaye koga siku ya Ijumaa josho la janaba, kisha akatoka katika saa ya kwanza ni kana kwamba katoa sadaka ya ngamia, na atakayetoka katika saa ya pili ni kana kwamba katoa sadaka ya ng'ombe, na atakayetoka katika saa ya tatu ni kana kwamba katoa sadaka ya kondoo, na atakayetoka katika saa ya nne ni kana kwamba katoa sadaka ya kuku, na atakaye kwenda katika saa ya tano ni kama katoa yai, akitoka imamu Malaika wanahudhuria kusikiliza ukumbusho".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu fadhila za kuwahi kwenda kuswali swala ya Ijumaa mapema. Na kuwasili mapema kunaanza tangu kuchomoza jua hadi kuwasili kwa Imam; Nazo ni saa tano, na zinagawanywa katika sehemu tano kulingana na muda kati ya kuchomoza kwa jua mpaka kuingia kwa imamu na kupanda kwake juu ya mimbari kutoa hotuba. Ya kwanza: Atakayeoga josho kamili, kama kuoga janaba, kisha akaenda katika msikiti wa Ijumaa katika saa ya kwanza, ni kama katoa sadaka ya ngamia. Ya pili: Mwenye kwenda saa ya pili ni kama katoa sadaka ya ng'ombe. Ya tatu: Yeyote atakayekwenda saa ya tatu ni kama ametoa sadaka kondoo dume mwenye pembe. Ya nne: Mwenye kwenda katika saa ya nne ni kama ametoa sadaka kuku. Ya tano: Mwenye kwenda saa tano, ni kama ametoa yai katika sadaka. Anapotoka imamu kwenda kutoa hotuba; Malaika waliokaa milangoni huacha kuwaandikia thawabu wale wanaoingia msikitini mmoja mmoja, na huja kusikiliza ukumbusho na hotuba.
kutoka kwa Abdullahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnasisitiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa atakayetaka kuja kwa ajili ya swala ya Ijumaa basi inapendeza kwake kuoga, mfano wa kuoga kwake josho la janaba.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaja katika swala ya Ijumaa akasikiliza na akanyamaza atasamehewa yale yaliyoko kati ya Ijumaa yake hiyo na Ijumaa ijayo na ziada ya siku tatu, na atakayegusa kijiwe basi atakuwa kafanya mchezo"
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kutawadha na akaufanya vyema udhu wake kwa kukamilisha nguzo zake na kufuata Sunna zake na adabu zake, kisha akaswali swala ya Ijumaa na akanyamaza na kumsikiliza mhutubu, na akanyamaza pasina kuleta mazungumzo yasiyofaa; Basi Mwenyezi Mungu atamsamehe madhambi yake madogo kwa muda wa siku kumi, kuanzia sala ya Ijumaa hadi Ijumaa ya pili na ziada ya siku tatu, kwa sababu jambo jema huzidishwa mara kumi. Kisha rehema na amani ziwe juu yake akatahadharisha juu ya moyo kutojali mawaidha yanayosemwa katika hotuba, na kuchezea viungo kwa kugusa kokoto na aina nyinginezo za upuuzi na kujishughulisha, hayo yote ni katika aina ya mchezo na kujishughulisha kusikofaa, kwani mwenye kufanya hivyo atakuwa kafanya mchezo, na atakayefanya mchezo atakuwa hana fungu kamili katika ujira wa swala ya Ijumaa.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmempa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kwenda msikitini kwa ajili ya ibada au elimu kwa lengo jingine katika mambo ya kheri katika wakati wowote; mwanzo wa mchana au mwisho wake kuwa Mwenyezi Mungu amemuandalia mahali na takrima ya ugeni peponi, kila anapokuja msikitini usiku au mchana.
Kutoka kwa Abdullah bin Salam radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alipokuja Madina Mtume rehema na amani ziwe juu yake, watu walikusanyika mbele yake, pakasemwa: Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, wakasema mara tatu, nikaja pamoja na watu kutazama, na nilipouona uso wake nikajua kuwa uso wake si uso wa muongo, kwa hivyo jambo la kwanza nililomsikia akizungumza alisema kuwa: "Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadMtume rehema na amani ziwe juu yake alipokuja Madina na watu wakamuona, haraka sana walimfuata, na miongo mwa waliomfuata ni Abdallah bin Salam radhi za Allah ziwe juu yake na alikuwa ni katika Mayahudi wakati huo, alipomuona akajua kuwa uso wake haukuwa wa mtu muongo; Kwa sababu ya kile kinachoonekana kwake kama, nuru, na uzuri, na heshima na ukweli, ikawa jambo la kwanza alilolisikia kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kuwataka watu wafanye matendo yatakayopelekea kuingia Peponi, ikiwemo: La kwanza: kusambaza salamu ya amani, na kuionyesha na kuikithirisha kwa wale unaowajua na usiowajua. La pili: Kulishiza chakula kwa sadaka na zawadi na kukaribisha ugeni. La tatu: Kuunga udugu kwa wale kinachowaunganisha kizazi au ukaribu wa udugu upande wa baba au mama. La nne: Swala za sunna, kisimamo cha usiku na watu wakiwa wamelala.
Kutoka kwa Abdillah Bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- amesema: "Kila mmoja miongoni mwenu ni mchunga hivyo ataulizwa kuhusu raia wake, kiongozi anayewaongoza watu ni mchunga naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mwanaume ni mchunga kwa watu wa nyumbani kwake naye ndiye wa kuulizwa kuhusu wao, na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mumewe na watoto wake naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mja ni mchunga juu ya mali ya bosi wake, naye ndiye atakayeulizwa juu ya mali hiyo, tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ni mchunga na kila mmoja ataulizwa kuhusu raia wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume rehema na amani zimfikie kuwa kila muislamu katika jamii anamajukumu anayoyasimamia na anayoyabeba, Imamu na kiongozi ni mchunga katika majukumu aliyopewa na Allah kuyasimamia, anatakiwa kuhifadhi sheria zao, na kuwalinda dhidi ya mwenye kuwafanyia uadui, na kumpiga vita adui yao, na kutopoteza haki zao, Na mwanaume kwa watu wa nyumba yake amelazimishwa kuwasimamia kwa matumizi, na kuishi nao vizuri, na kuwasomesha na kuwaadabisha, Na mwanamke katika nyumba ya mumewe ni mchunga kwa kuipangilia vizuri nyumba yake, na kuwalea watoto wake, naye ataulizwa kuhusu hilo, Na mfanyakazi mmilikiwa na mwajiriwa ataulizwa katika mali ya bosi wake kwa kusimamia kuhifadhi kile kilicho mkononi mwake, na huduma zake, naye ataulizwa kuhusu hilo, kila mmoja ni mchunga katika vile alivyopewa kuvichunga, na kila mmoja ataulizwa kuhusu raia wake.
Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Enyi kongamano la vijana mwenye uwezo miongoni mwenu wa kuoa na aoe, kwani ndoa ni sababu ya kuinamisha macho na kulinda tupu, na asiekuwa na uwezo basi ajilazimishe kufunga, hakika funga kwake itakata matamanio".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume rehema na amani ziwe juu yake amewahimiza wenye uwezo wa tendo la ndoa na gharama ya ndoa waoe; kwani hilo Iinahifadhi macho yake kutokana na mambo yaliyokatazwa, linalinda usafi wake wa mwili, na linamzuia asiingie katika uasherati, ambaye hawezi kukidhi mahitaji ya ndoa hali ya kuwa ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa basi ni lazima afunge, kwani hii itakata matamanio ya tupu na shari ya manii.
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah bin Aamir -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Tahadharini sana na kuingia/kukaa kwa wanawake" Mtu mmoja katika Maanswari akasema: Ewe Mtume wa Allah vipi kuhusu shemeji? Akasema: "Shemeji ni kifo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala la kuchanganyikana na wanawake wa kando, na akasema: Jiepusheni sana kuingia kwa wanawake, na wanawake watahadhari kuingia kwa wanaume. Akasema mtu mmoja miongoni mwa Manswari (watu wa Madina): Wasemaje kuhusu ndugu wa karibu wa mume; kama kaka wa mume na mtoto wa kaka yake, na ami yake na mtoto wa ami yake, na kijana wa dada yake, na mfano wa hao katika wale wa halali kwao kumuoa akiwa hajaolewa? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Mtahadharini kama mnavyokitahadhari kifo! Kwa sababu kukaa faragha na mashemeji kunapelekea fitina na maangamivu katika dini, ndugu wa mume wasiokuwa baba zake na wanawe, hawa wanatakiwa zaidi kuzuiliwa kuliko hata mtu wa kando; kwa sababu kukaa faragha na ndugu wa mume ni zaidi ya kukaa faragha na mtu mwingine, na shari iko karibu zaidi kwake kutokea kuliko hata kwa asiyekuwa yeye, na kuna uwezekano mkubwa wa kutokea; kwa sababu anauwezekano mkubwa wa kumfikia mwanamke na kukaa naye faragha pasina mtu wa kuwakemea, na ni kwa sababu hana budi lazima aonane naye kwakuwa ni ndugu wa mume, na ni vigumu kumzuia, kwa sababu tamaduni za watu zimezoeleka kulipuuza hilo, mtu akakaa faragha na mke wa kaka yake; hivyo anafanana na kifo katika ubaya na madhara, tofauti na mwanaume wa kando kwani huyo watu humtahadhari.