





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni, ukifunikwa kwenu nyinyi basi ukadirieni".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuingia kwa mwezi wa Ramadhani na kutoka kwake, akasema: Mtakapouona mwandamo wa Ramadhani basi fungeni, yakikukingeni mawingu kati yake na nyie, basi hesabuni siku thelathini za mwezi Shaaban, na mkiuona mwandamo wa mwezi Shawal basi fungueni, yakikukingeni mawingu na ukafichikana kwenu; basi hesabuni siku thelathini za mwezi Ramadhani.
Kutoka kwa Abul Hauraai Assa'di amesema: Nilisema kumwambia Hassan bin Ally radhi za Allah ziwe juu yao: Ulihifadhi nini kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake? Akasema: Nilihifadhi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake? "Acha linalokutia shaka fanya lisilokutia shaka, kwani ukweli ni utulivu, na bila shaka uongo ni shaka"
Imepokelewa naTirmidhiy na Nasai na AhmadAliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha kile ulicho na shaka nacho katika maneno na matendo nakuwa jambo hilo limekatazwa toka mwanzo, je jambo hili ni halali au ni haramu, afanye asilo na shaka nalo katika yale ambayo anaamini kuwa ni mazuri na ni halali, kwa sababu moyo unatulizana na unatulia katika hilo, na hakuna shaka ndani yake inayotia msongo na taharuki.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini, na hii ni pale mmoja wao atakapo tawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaenda msikitini hakusudii kwa kwenda kwake ila swala, hakuna kinachomnyanyua isipokuwa swala, basi hatopiga hatua yoyote isipokuwa atanyanyuliwa daraja kwa hatua hiyo, na atasamehewa makosa kwa hatua hiyo mpaka atakapoingia msikitini, na anapoingia msikitini huhesabika kuwa yuko ndani ya swala madamu swala ndio bado inayomzuia kutoka, na Malaika humuombea rehema mmoja wenu madamu akiwa bado kakaa mahala aliposwali, wakisema: Ewe Mola wetu muhurumie, Ewe Mola wetu msamehe, Ewe Mwenyezi Mungu mkubalie msamaha wake, wanaendelea kufanya hivyo kwa muda atakaokuwa hajafanya maudhi yoyote, na madam hajatengua udhu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakaposwali muislamu katika jamaa, swala yake hiyo itakuwa bora kuliko swala yake nyumbani kwake au sokoni kwake kwa zaidi ya mara ishirini. Kisha akaeleza sababu ya hilo: Nayo nikuwa mtu atakapotawadha akatimiza vizuri udhu na ukaufanya vizuri, kisha akatoka kwenda Msikitini hakuna kinachomtoa ila kukusudia kusali, hatopiga hatua yoyote isipokuwa atanyanyuliwa kwa hatua hiyo daraja na nafasi ya juu, na hufutiwa kwake kwa hatua hiyo makosa, Atakapoingia Msikitini na akakaa akisubiri swala, basi atapata malipo ya swala na thawabu zake kwa muda wote atakaokaa akisubiri swala, na Malaika wakimuombea akiwa katika kikao chake aliposwalia, wakisema: "Ewe Mwenyezi Mungu msamehe, ewe Mwenyezi Mungu muhurumie, ewe Mwenyezi Mungu mfutie makosa" Huendelea kumuombea madam hajaharibu udhu wake, au akafanya yanayowakera watu au Malaika.
Kutoka kwa bin Mas'udi radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake-: "Si halali damu ya muislamu isipokuwa kwa moja kati ya mambo matatu: Mzinifu aliyeoa, na nafsi kwa nafsi, na mwenye kuacha dini yake mwenye kusambaratisha umoja".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa damu ya Muislamu ni haramu, isipokuwa akifanya moja katika mambo matatu: La kwanza: Akatakayetumbukia katika uchafu wa zinaa, na hali yakuwa ameoa ndoa sahihi ya kisheria; ni halali kumuua kwa mpiga mawe. La pili: Atakayeua nafsi isiyo na hatia kwa makusudi pasina haki, atauwawa kwa sharti zake. La tatu: Mwenye kutoka katika umoja wa Waislamu; ima kwa kuacha dini yake ya Uislamu yote kwa kuritadi, au mwenye kutoka bila kuritadi kwa kuacha sehemu ya dini kama waasi, na vibaka, na wanaopiga vita Waislamu kama Makhawariji na wengineo.
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mweyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, lakini ushahidi ni kwa mwenye kudai na kiapo ni kwa mwenye kukanusha".
Imepokelewa na AlbayhaqyAmebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa lau watu wangelipwa kwa msingi wa madai yao tu, bila ya ushahidi wala vielelezo, basi watu watadai mali na damu za watu wengine, lakini mwenye kudai lazima awasilishe alama na ushahidi wa kile anachodai, ikiwa hana ushahidi basi madai hayo yanawasilishwa kwa mshitakiwa, na akikanusha ni lazima aape na kuachiliwa.
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayekula kitunguusaumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake", Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliletewa chungu kikiwa na mbogamboga, akakuta zinaharufu, akauliza akaelezwa kilichomo katika mboga hizo, akasema: Wapewe baadhi ya Maswahaba zake aliokuwa nao, alipoiona hakupendezwa nayo, akasema: "Kula kwani mimi ninanong'ona na yule usiyenong'ona naye". Na kwa Muslim kutoka kwa Jabiri bin Abdillah, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: “Mwenye kula katika mboga hii, kitunguu saumu." – na mara nyingine alisema: "Mwenye kula kitunguu maji, na kitunguu saumu – asiukaribie msikiti wetu; Kwani hakika Malaika wanaudhika kwa yale ambayo wanadamu wanaudhika nayo.”
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekula kitunguu saumu au kitunguu maji asije msikitini, ili asiwaudhi ndugu zake katika wale wanaohudhuria swala ya jamaa kwa harufu yake, nalo ni katazo la kiusafi la kutokuja msikitini, na si katazo la kula; kwa sababu ni katika vyakula vya halali, na aliletewa Mtume rehema na amani ziwe juu yake chungu kikiwa na mbogamboga, aliponusa ndani yake harufu au alipoambiwa kilichomo, alikataa kula, na akakisogeza kwa baadhi ya Maswahaba zake akasema: Kula; kwani mimi husema na Malaika kwa wahyi. Na akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika hukereka na harufu mbaya, kama wanavyokereka watu kwa harufu hiyo.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hebu nielezeni lau kama Mto ungelikua mlangoni kwa mmoja wenu akioga humo kila siku mara tano, unasemaje kuhusu hilo, kunaweza kubaki na uchafu katika mwili wake?" Wakasema: Hautobakiza uchafu wowote, akasema: " Huu ndio mfano wa swala tano, Mwenyezi Mungu hufuta makosa kwa swala hizo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmefananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- swala tano za kila usiku na mchana katika kuondoa kwake na kufuta kwake madhambi madogo ni sawa na Mto ulioko mlangoni kwa mtu akioga humo kila siku mara tano, hautobakiza chochote katika uchafu wake.
Kutoka kwa Amri Bin Shuab kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa watoto wa miaka saba, na wapigeni kwa ajili yake nao wakiwa watoto wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi".
Imepokelewa na Abu DaudAmebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa baba awaamrishe watoto wake wa kiume na wa kike kusali na umri wao ukiwa mikaa saba, na awafundishe wanayoyahitaji kwa ajili ya kuitekeleza. Na wakifikisha miaka kumi azidi kutilia mkazo, awapige wanapofanya uzembe, na awatenganishe katika vitanda.
Kutoka kwa Abdul Rahman Bin Abii Laila amesema: Alikutana nami Ka'bu bin Ujza, akasema: Hivi wataka nikupe zaidi? Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema? Akasema: "Basi semeni: Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammadi na juu ya watu wa Muhammadi, kama ulivyompa rehema Ibrahim na juu ya watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa, ewe Mwenyezi Mungu shusha baraka juu ya Muhammad na juu ya watu wa Muhammad, kama ulivyoteremsha baraka kwa watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMasahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu namna ya kumtakia rehema? baada ya kujua kwao namna kumuombea amani (salam) katika kikao cha tahiyatu ndani ya swala: "Amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake...?" Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akawaeleza namna ya kumtakia rehema, na maana yake: "Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammad na juu ya watu wa Muhammad" Yaani: Mtaje kwa sifa nzuri kwa Malaika walioko juu mbinguni, na juu ya wafuasi wake katika dini yake, na waumini katika ndugu zake wa karibu. "Kama ulivyoteremsha rehema juu ya watu wa Ibrahim" Kama ulivyotoa takrima juu ya watu wa Ibrahim amani iwe juu yake, nao ni Ibrahim na Ismail na Is'haka na kizazi chake na wafuasi wao miongoni mwa waumini, basi zipeleke fadhila zako kwa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake. "Hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa". Yaani: Mwenye kuhimidiwa katika dhati yako na sifa zako na vitendo vyako, mpana katika utukufu wako na ugawaji riziki wako. "Ewe Mwenyezi Mungu teremsha baraka kwa Muhammad na juu ya watu wa Muhammad kama ulivyoteremsha baraka juu ya watu wa Ibrahim" Yaani: Mpe katika kheri na karama zile zilizo kubwa zaidi na uzizidishe na umdumishie kheri hizo.