





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abdillah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika mmoja wenu anapokufa huonyeshwa makao yake asubuhi na jioni, akiwa katika watu wa peponi basi huonyeshwa katika watu wa peponi, na akiwa katika watu wa motoni basi huonyeshwa katika watu wa motoni, basi husemwa: Haya ndiyo makao yako mpaka atakapokufufua Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mja anapokufa huonyeshwa mbele yake makao yake na sehemu yake maalumu peponi au motoni, mwanzo wa mchana na mwisho wake; mahali pake peponi, na sehemu yake motoni akiwa ni miongoni mwa watu wa motoni, na huambiwa: Haya ndiyo makao yako utakayofufuliwa kwayo siku ya Kiyama; na katika hilo kuna kuneemeka kwa muumini, na kuadhibiwa kwa kafiri.
Imepokelewa kutoka kwa Tamim Ad-Dari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Litafikia jambo hili ulipofika usiku na mchana, na wala hatoacha Mwenyezi Mungu nyumba ya mjini wala ya kijijini isipokuwa ataiingiza Mwenyezi Mungu dini hii, kwa utukufu wa yeyote au kwa udhalili wa yeyote, ni utukufu anaoutukuza Mwenyezi Mungu uislamu, na ni udhalili anaoudhalilisha Mwenyezi Mungu ukafiri" na alikuwa Tamimu Dari akisema, nililijua hilo kwa watu wa familia yangu, kwa hakika alipata aliyesilimu miongoni mwao kheri na heshima na utukufu, na aliyekuwa kafiri alipata udhalili na unyonge na ulipaji kodi.
Imepokelewa na AhmadMtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, amesema kuwa dini hii itaenea sehemu zote za ardhi, hivyo dini hii itafika sehemu yoyote ile ufikapo usiku na mchana, na hatoiwaacha Mwenyezi Mungu Mtukufu nyumba yoyote mijini na vijijini wala mabondeni na majangwani isipokuwa ataiingiza dini hii, atakayeikubali dini hii na akaiamini basi atakuwa mtukufu kwa sababu ya utukufu wa Uislamu, na atakayeikataa na akaipinga basi atakuwa dhalili mwenye kufedheheshwa. Kisha swahaba Tamim Al-Dari, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akaeleza kuwa alilijua hilo aliloambiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake kwa watu nyumba yake hasa, kwani kila aliyesilimu miongoni mwao alipata kheri na heshima, na utukufu, na aliyekufuru miongoni mwao alipata udhalili na unyonge, hii ikiwa ni pamoja na pesa anazowalipa Waislamu kama Jizia (Kodi).
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, bin Jud'aan kabla ya uislamu alikuwa akiunga udugu, na akilisha masikini, je hilo litamfaa?Akasema: "Halitamnufaisha, na hakika yeye hajawahi kusema hata siku moja: Ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu siku ya Kiyama."
Imepokelewa Imamu MuslimAmetoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu Abdullahi Bin Jad'aan, na alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kikuraishi kabla ya Uislamu, Na miongoni mwa vitendo vyake vizuri ni kuwa yeye: huunganisha ndugu zake na huwafanyia wema, na hulisha chakula masikini, na mambo mengine mengi ambayo Uislamu umeyahimiza kuyafanya, nakuwa matendo haya hayatomfaa katika Akhera yake; Na hilo ni kwa sababu ya kumkufuru Mola wake, na kuwa yeye hajawahi hata siku moja kusema: Ewe Mola wangu nisamehe mimi makosa yangu siku ya Kiyama.
Imepokelewa kutoka kwa Zaid Bin Khalid Aljuhaniy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alitusalisha Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- Sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah wakati mvua iliponyesha usiku, na alipomaliza akawageukia watu na kuwauliza: "Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri, Basi yeyote atakayesema tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu basi huyo ni mwenye kuniamini mimi, na ni mwenye kuupinga unajimu, ama atakayesema kuwa tumenyeshelezewa Mvua kwa sababu ya nyota fulani na fulani, basi huyo amenikadhibisha mimi na kaziamini nyota."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliswali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah- nacho ni kijiji kilichopo karibu na Makkah, baada ya kunyesha Mvua usiku. Na alipomaliza sala yake aliwageukia watu kwa kuwaelekea, akawauliza: Hivi mnajua alichosema Mola wenu Mtukufu? Basi wakajibu kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wajuzi zaidi, Akasema: Kwa hakika Mwenyezi Mungu ameeleza kuwa watu wamegawanyika makundi mawili wakati wa kuteremka Mvua, kuna kundi ni lenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kundi lingine ni lenye kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu; Basi atakayesema tumenyeshelezewa kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema zake, na akaegemeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu suala la kushuka mvua; Basi huyo ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu muumba mwenye kuendesha ulimwengu, na ni mwenye kupinga unajimu. Ama atakayesema: Tumenyeshelezewa mvua kwa sababu ya Nyota fulani; Basi mtu huyo ni kafiri, na ni mwenye kuamini nyota -unajimu- na kufuru ndogo ikiwa kuteremka mvua kutaegemezewa kwenye kutazamia Nyota; Na Mwenyezi Mungu hakuzifanya Nyota kuwa sababu ya kunyesha mvua na wala hakupanga iwe hivyo, Na ama atakayeegemeza suala la kuteremka mvua na matukio mengine ya Ardhini kwenye mzunguko wa Nyota wakati wa kuchomoza kwake na kuanguka kwake ya kuwa ndiyo kisababishi cha hakika, basi mtu huyo amekufuru kufuru iliyokubwa,
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Walikuja watu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi wakamuuliza: kwa kusema kuwa hakika sisi twapata katika nafsi zetu mambo ambayo yamuia uzito mmoja wetu kuyasema, akasema: "Ni kweli mnayapata hayo kwenye nafsi zenu?" Wakasema: "Ndiyo" Akasema: "Hiyo ndiyo imani ya kweli."
Imepokelewa Imamu MuslimLilikuja kundi la maswahaba kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na wakamuuliza kuhusiana na yanayowatokea katika nafsi zao miongoni mwa mambo makubwa ambayo yanakuwa kwao ni mazito kuyasema kutokana na ubaya wake na kupenda kwao kujiepusha nayo Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: kwa hakika hiki ambacho mnakipata kwenye nafsi zenu ndiyo imani ya kweli na uhakika ambao unawapa msukumo ili kuzuia anayoyaweka shetani katika nyoyo na kuwazuieni kuyasema na kuyaona ni mazito kwenye nafsi zenu, na shetani kutoweza kuimiliki mioyo yenu, tofauti na yule ambaye ametawaliwa na shetani kwenye moyo wake akashindwa kupata chenye kumzuia kusema .
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika mmoja wetu anatokewa na jambo kwenye nafsi yake kiasi yakuwa anaona bora akachomwa mpaka akawa jivu ni bora kwake kuliko kulizungumza jambo hilo, akasema: "Allahu Akbar, Allahu Akbar Mwenyezi Mungu ni mkubwa Mwenyezi Mungu ni mkubwa, namshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amevirudisha vitimbi vya Shetani na vikageuka kuwa ni wasiwasi".
Imepokelewa na Abu Daud na Nasai katika AlkubraaAlikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mmoja wetu hutokewa na jambo kwenye nafsi yake kiasi yakuwa anaona bora akachomwa mpaka akawa jivu ni bora kwake kuliko kulizungumza jambo hilo. Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga Takbira mara mbili na akamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kurudisha vitimbi vya shetani na kuvigeuza kuwa ni wasiwasi,
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Shetani humjia mmoja wenu na akamwambia: Ni nani aliumba kitu fulani? Mpaka anafikia kusema ni nani alimuumba Mola wako? Basi ikiwa atafikia kuuliza hivyo basi na ajikinge kwa Mwenyezi Mungu na awache kuuliza maswali hayo."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu tiba sahihi ya kujiepusha na maswali ambayo Shetani huyatumia kumtia wasiwasi muumini, Basi Shetani husema: Ni nani aliyeumba kitu fulani? Ni nani aliyeumba mbingu? Ni nani aliyeumba Ardhi? Hivyo basi muumini kutokana na dini yake na maumbile yake na akili yake humjibu kwa kusema kuwa ni Mwenyezi Mungu, Lakini Shetani haishii hapo kwenye kutia wasiwasi, bali anahama mpaka anafikia kusema; Ni nani aliyemuumba Mola wako? Basi wakati huo muislamu atajizuilia na wasiwasi huu kwa kufanya mambo matatu: Kwa kumuamini Mwenyezi Mungu. Na kwa kujikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani, Na kuacha kuendekeza wasiwasi.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu muumini kwa jema alilofanya, huandikiwa thawabu za wema wake hapa Duniani na hulipwa thawabu hizo huko Akhera Ama kafiri hulishwa kwa mema aliyoyafanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hapa duniani, mpaka akifika Akhera anakuwa hana jema lolote ambalo atalipwa nalo."
Imepokelewa Imamu MuslimAnaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu kwa waumini, na uadilifu wake kwa makafiri. Ama muumini hazipungui thawabu za mema aliyoyafanya; Bali hulipwa hapa duniani wema kwa utiifu wake, pamoja na kulimbikiziwa malipo yake huko Akhera; Na huenda akahifadhiwa malipo yake yote huko Akhera. Ama kafiri, Mwenyezi Mungu humlipa malipo kutokana na wema alioufanya kwa malipo ya mambo yaliyo mazuri hapa Duniani, mpaka inakuwa akifika Akhera, anakuwa hana thawabu na malipo atakayo lipwa huko, kwa sababu matendo mema ambayo yatamfaa hapa Duniani na Akhera lazima awe mtendaji wake ni muumini.
Imepokelewa kutoka kwa Hakiim Bin Hizaam -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni upi mtazamo wako katika mambo ambayo nilikuwa nikifanya ibada kupitia mambo hayo kabla ya kuwa muislamu, miongoni mwa sadaka, au kumwacha huru mtumwa, au kuunganisha udugu, je katika mambo hayo kuna malipo? Basi akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: " Umekwisha pokea malipo yako kutokana na mema uliyoyatanguliza".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kafiri anaposilimu hulipwa kwa mema aliyokuwa akiyafanya kabla ya kusilimu miongoni mwa sadaka au kuacha huru mtumwa au kuunganisha udugu.