





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hamtazami Mwenyezi Mungu mtu ambaye kamuingilia mwanaume au mwanamke katika tupu yake ya nyuma".
Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasai katika kitabu AlkubraaAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ahadi kali ya adhabu kuwa Mwenyezi Mungu hatomtazama mtazamo wa huruma mwanaume aliyemuingilia mwanaume mwenzake katika utupu wake wa nyuma, au mwanamke katika utupu wake wa nyuma, nakuwa hilo ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.
Kutoka kwa Muawia Al-Qushairi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni zipi haki za mke wa mmoja wetu juu yake?, Akasema: "Ni umlishe pale unapokula, na umvishe unapovaa, au utakapopata kipato, na wala usipige uso, na wala usitoe maneno machafu, na wala usihame isipokuwa ndani ya nyumba".
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na AhmadAliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni zipi haki za mke juu ya mume wake? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akataja mambo kadhaa, miongoni mwa hayo ni: La kwanza: Usijipendelee kwa chakula ukamuacha yeye; bali umlishe kama ulivyo kula wewe. La pili: Usijipendelee kwa mavazi mazuri, bali umvishe utakapovaa wewe, na ukipata kipato na ukaweza. La tatu: Usipige ila kuwe na sababu na haja ya kufanya hivyo, na akihitaji kumpiga ima kwa kumuadabisha au kwa kuacha kwake mambo ya faradhi, basi kiwe ni kipigo kisichovunja wala kujeruhi; na uso haupigwi;kwa sababu uso ndio kiungo kitukufu zaidi na kilicho wazi zaidi na kimekusanya viungo vitukufu, na viungo laini. La nne: Usitukane au kusema: Mwenyezi Mungu auchafue uso wako; usimnasibishe yeye wala chochote katika mwili wake na ubaya ambao ni kinyume na uzuri; kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye aliutengeneza uso wa mwanadamu na mwili wake, na akakipa umbile zuri kila kiumbe, na kutukana umbile kunarudi katika kumtukana muumbaji, Mwenyezi Mungu atuepushe na hilo. La tano: Usihame ila kitandani, na wala usiondoke hapo, na wala usimhamishie katika nyumba nyingine; na huenda hilo ni katika mambo yaliyozoeleka kutokea baina ya wanandoa.
Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- amesema: Kamlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuunga nywele na mwenye kuungwa, na mwenye kuchora chata na mwenye kuchorwa.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDua ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kulaaniwa na kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa makundi ya aina nne: La kwanza: Mwanamke mwenye kuunga nywele zake au za mwenzake kwa nywele zingine. La pili: Na mwenye kutaka kuungwa nywele, kwa kumuomba mwenzake amuunganishe nywele zake kwa nywele zingine. La tatu: Mwenye kupiga chata, na anayejichoma sindano katika sehemu ya mwili wake, kama uso au kiganja au kifua, na kuweka wanja au mfano wake, ili kubakie alama ya bluu, au kijani; kwa kutaka kujipamba au uzuri. La nne: Mwenye kutaka kupigwa chata, ni yule anayeomba kupigwa chata. Na matendo haya ni katika madhambi makubwa.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayekuwa na wake wawili akaegemea kwa mmoja wao atakuja siku ya Kiyama upande wake mmoja ukiwa umepinda".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekuwa na mke zaidi ya mmoja, akawa hakufanya uadilifu baina ya wake zake uadilifu unaowezekana, ikiwemo kuwafanyia usawa katika matumizi na makazi na mavazi na malazi, nikuwa adhabu yake siku ya Kiyama nusu ya mwili wake itakuwa imepinda, na kupinda kwake ni adhabu kwake kwa sababu ya dhulma yake, kama alivyopinda katika muamala wake.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi zao, madamu hayajafanyiwa kazi au kuzungumzwa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Muislamu haadhibiwi kwa mazungumzo ya shari ya nafsi yake kabla ya kuyafanyia kazi au kuyazungumza, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu ameondolea uzito na kusamehe, na hakuuandikia makosa umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake kwa yale yanayopatikana akilini na yakazunguka katika nafsi bila ya kutulizana nafsi katika hiyo; yakitulizana katika moyo wake, mfano kama kiburi na kujiona au unafiki, au akafanya kwa viungo vyake au akasema kwa ulimi wake basi hapa atahesabiwa.
Imepokelewa kutoka kwa Othman -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abalehe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na AhmadAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kubeba wajibu ni lazima kwa mwanadam isipokuwa hawa watatu: Mtoto mdogo mpaka akue na abalehe. Na kwa mwendawazimu aliyepoteza akili mpaka akili irudi. Na kwa aliyelala mpaka aamke. Kubeba wajibu kumeondolewa kwao, na kutenda kwao madhambi hakuandikwi, lakini mtoto huandikiwa kheri anapofanya, isipokuwa mwendawazimu na aliyelala; kwa sababu wote hawa wako katika kundi la mtu asiyekubalika ibada yake kwa kupoteza hisia.
kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- "kila kilevi ni haramu, na atakayekunywa pombe duniani na akafa akiwa mlevi kupindukia na hakutubia, hatoinywa huko akhera"
Imepokelewa na Muslim, vile vile Bukhari ikiwa na ibara ya mwisho ndani ya kitabu chakeAmebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kila kinachoondosha akili na kuiondoa hicho ni pombe yenye kulewesha, sawa iwe ni kunywa, au kula, au kuvuta kwa pumzi au vinginevyo, na kuwa kila kinacholevya na kuondoa akili Mwenyezi Mungu Mtukufu amekiharamisha na amekataza, kiwe kidogo au kingi, Na kuwa kila mwenye kunywa aina yoyote ya vileo, na akaendelea kuvinywa, wala hakutubia mpaka akafa; Anastahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kumnyima kuinywa Peponi.
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Wapigeni vita washirikina kwa mali zenu na nafsi zenu na ndimi zenu".
Imepokelewa na Abu Daud, Nasai na AhmadAliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga vita makafiri, na kutumia juhudi katika kukabiliana nao kwa kila nyenzo kwa kadri iwezekanavyo, ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, na miongoni mwake: Kwanza: Kutoa mali katika kuwapiga vita; ikiwemo kununua silaha, na kutoa mahitaji kwa wapiganaji, na mfano wake. Pili: Kutoka kwa nafsi na mwili ili kukabiliana nao na kuwazuia. Tatu: Kwa kuwalingania waingie katika dini hii kwa ulimi, na kuwasimamishia hoja juu yao, na kuwakemea na kuwajibu hoja zao.
Imepokelewa kutoka kwa Khuraimu Bin Faatik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Matendo yapo ya aina sita na watu wapo wako aina nne, basi kuna watu wa aina mbili wanaostahiki malipo, na malipo yao huwa sawa na matendo yao, na jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na jema moja huzidishwa mpaka kufikia mema mia saba, Basi wawili wenye kustahiki malipo ni: Yeyote atakaye kufa hali yakuwa hajamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia Peponi, na atakaye kufa hali ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote basi ataingia Motoni, na ama yule ambaye atalipwa kwa namna alivyokusudia ni yeyote atakaye kusudia kufanya jambo jema mpaka moyo wake ukahisi kuwa umetenda na Mwenyezi Mungu akajua kutenda kwake huko basi mtu huyo ataandikiwa jema moja, na atakaye fanya kosa ataandikiwa kosa moja, na atakaye fanya jema moja basi hulipwa kwa kumi mfano wake, na mwenye kutoa chochote katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi atalipwa kwa kila kimoja kwa mara mia saba, ama watu walivyogawanyika kuna miongoni mwao waliokunjuliwa mambo yao hapa Duniani na wakawa na maisha duni huko Akhera, na kuna wenye maisha Duni hapa duniani na wakakunjuliwa maisha yao huko Akhera, na kuna wenye maisha duni hapa duniani na pia Akhera, na wakakunjuliwa maisha yao hapa duniani na kesho Akhera."
Imepokelewa na AhmadAlieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yapo aina sita, na watu wamegawanyika katika makundi manne, nayo ni: Kundi la kwanza: Yeyote atakaye kufa na hakumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote anastahiki kuingia peponi. Kundi la pili: Yeyote atakaye kufa hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu kingine anastahiki kuingia motoni na atakaa humo milele. Na matendo hayo mawili ndiyo haki mbili za msingi. Kundi la tatu: Kukusudia kufanya wema, basi yeyote atakaye kusudia kufanya jema na akawa mkweli katika makusudio yake mpaka akahisi kweye moyo wake kuwa hili ndilo kusudio langu, kisha likamtokea jambo la kumzuia asifanye alichokikusudia katika wema huu, basi huandikiwa thawabu za wema kamili. Kundi la nne: Kufanya tendo baya; Yeyote atakaye fanya tendo baya basi huandikiwa kosa moja. Na matendo hayo mawili: Ndiyo hulipwa sawa sawa bila ya kuzidisha. Kundi la Tano: Jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na malipo hayo ni kwa mwenye kukusudia kufanya wema na akaufanya wema huo, basi huandikiwa mema kumi. kundi la sita: Jema moja hulipwa sawa na mema mia saba, na malipo hayo ni kwa mwenye kutoa kitu kimoja katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hulipwa kwa kitu hiki kimoja kwa mema mia saba, na haya ni kutokana na fadhila za Mwenyezi Mungu aliyetakasika na Kutukuka, na ukarimu wake kwa waja wake. Ama aina Nne ya watu ni hawa: Aina ya kwanza: Ni mtu ambaye amekunjuliwa mambo yake hapa Duniani kwa upande wa riziki, ananeemeka humo na hupata akitakacho, lakini ni mwenye dhiki na tabu kubwa Akhera na mwisho wake ni kuingia motoni, na huyo ni tajiri wa kikafiri. Aina ya pili: Ni mtu mwenye dhiki hapa Duniani upande wa riziki, lakini amekunjuliwa huko Akhera, na mwisho wake ni kuingia Motoni, na huyo ni muumini fakiri. Aina ya tatu: Ni mtu mwenye dhiki hapa Duniani na Akhera, naye ni kafiri fukara. Aina ya nne: Ni mtu aliyekunjuliwa mambo yake hapa Duniani na Akhera, naye ni muumini tajiri.