Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way






























Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa miongoni mwa sharti za kusihi swala: Ni twahara, ni wajibu kwa atakayetaka kuswali atawadhe ikiwa kimetokea kwake kitenguzi cha udhu; kama haja kubwa au ndogo au usingizi au kinginecho.
Anatueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kusafisha meno kwa kijiti cha mti wa Arak na mfano wake husafisha kinywa kutokana na uchafu na harufu mbaya, Nakuwa ni katika sababu za kumridhisha Allah Mtukufu kwa mja; kwa sababu ndani yake kuna kumtii Allah na kuitika amri yake, na pia kuna usafi anaoupenda Allah Mtukufu.
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa swala tano za faradhi za usiku na mchana, na swala ya ijumaa kila wiki, na funga ya Ramadhani kila mwaka, vyote hivi hufuta madhambi madogo madogo yaliyo kati yake, kwa sharti la kuyaepuka madhambi makubwa, Ama madhambi makubwa kama zinaa na kunywa pombe haya hayafutwi isipokuwa kwa toba.
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Kuwa mwanadamu kamili katika kuunga udugu na kuwatendea wema ndugu wa karibu si yule mtu mwenye kulipa wema aliotendewa, Bali muunga udugu halisi na kamili katika kuunga udugu ni yule ambaye ukikatwa udugu wake anauunga, hata wakimtendea ubaya; basi yeye huwalipa wema.
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayefunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Mwenyezi Mungu, na kwa kuitakidi ulazima wa swaumu na yale aliyoyaahidi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wafungaji kuwa na malipo makubwa na thawabu, akikusudia kupata radhi za Allah Mtukufu si kwa kutaka kujionyesha au kusikika, yatasamehewa kwake madhambi yake yaliyopita.
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu fadhila za kusimama usiku wa cheo unaokuwa katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, nakuwa yeyote mwenye kujitahidi ndani yake kwa ibada ya swala na dua na kusoma Qur'ani na kumtaja Allah, akiwa na imani na hayo, na kwa fadhila zilizoelezwa kwayo, akitaraji kwa amali yake malipo ya Allah Mtukufu, si kwa kutaka kuonekana na kusikika, basi husamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake.
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kanuni kuu katika mambo, nakuwa zinagawanyika sehemu tatu katika sheria: Halali ya wazi, na haramu ya wazi, na mambo yenye kutatiza, hukumu yake haiko wazi upande wa uhalali na uharamu, watu wengi hawajui hukumu yake. Atakayeacha mambo hayo yenye kutatiza kwake, dini yake itasalimika kwa kuwa mbali na kuingia katika haramu, na heshima yake itasalimika kutokana na maneno ya watu, kwa yale wanayoweza kumuaibisha kwa kuyafanya kwake haya yenye kutatiza. Na asiyeyaepuka yenye kutatiza atakuwa kaitumbukiza nafsi yake, ima katika haramu, au watu kumkosea heshima yake. Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kapiga mfano ili abainishe hali ya mwenye kuyafanya mambo yenye kutatiza, nakuwa yeye ni sawa na mchunga mifugo, mwenye kuchunga karibu na ardhi ambayo kaihifadhi mwenye ardhi hiyo, inahofiwa mifugo yake kulisha katika mipaka hii kwa sababu ya ukaribu wake, na hivyo hivyo mwenye kufanya mambo yenye utata ndani yake, basi kwa kufanya hivyo anakuwa karibu na haramu na anahofiwa kutumbukia ndani yake. Na baada yake akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama (Nacho ni moyo) mwili hutengemaa kwa kutengemaa kwake, na huharibika kwa kuharibika kwake.
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuwajibishia kutenda wema katika kila kitu, na wema: Ni kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu daima, na katika ibada zake, na katika kutenda kheri na kuacha kuwaudhi viumbe, miongoni mwa hayo ni kutenda wema katika kuuwa na kuchinja. Wema katika kuuwa ni wakati wa kisasi: Achague njia nyepesi na rahisi zaidi na ya haraka zaidi kutoa roho kwa mwenye kuuawa. Na wema katika kuchinja ni wakati wa kuchinja: Amuhurumie mnyama kwa kunoa kifaa, na kisinolewe mbele ya mnyama akitazama, na asichinjwe hali yakuwa wanyama wenzake wanatazama.
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni lazima kuzuia madhara kwa aina zake zote na sababu zake zote kwako na kwa wengine,ni haramu kwa yeyote kujiudhi mwenyewe na mwingine kwa kiwango sawa. Na ni haramu kwake kukabiliana na madhara kwa madhara; kwa sababu madhara hayaondoshwi kwa madhara, isipokuwa kama itakua katika njia ya kulipiza kisasi pasina kuvuka mipaka. Kisha akabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- adhabu pale yanapotokea madhara kwa mtu mwenye kuwadhuru watu, na pale zinapotokea tabu kwa mtu mwenye kuwatia watu tabu.