Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way






























Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
Amebainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni lazima kuzuia madhara kwa aina zake zote na sababu zake zote kwako na kwa wengine, ni haramu kwa yeyote kujiudhi mwenyewe na mwingine kwa kiwango sawa. Na ni haramu kwake kukabiliana na madhara kwa madhara; kwa sababu madhara hayaondoshwi kwa madhara, isipokuwa kama itakua katika njia ya kulipiza kisasi pasina kuvuka mipaka.
Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa lau watu wangelipwa kwa msingi wa madai yao tu, bila ya ushahidi wala vielelezo, basi watu watadai mali na damu za watu wengine, lakini mwenye kudai lazima awasilishe alama na ushahidi wa kile anachodai, ikiwa hana ushahidi basi madai hayo yanawasilishwa kwa mshitakiwa, na akikanusha ni lazima aape na kuachiliwa.
Anaeleza Abuu Musa Al-Ash'ari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma kwenda Yemen, akamuuliza kuhusu vinywaji vinavyo tengenezwa huko je ni haramu, akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hilo. Akasema Abuu Musa radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ni Bit'u: Yaani mvinyo wa Asali, na Muruuz: Ni mvinyo wa ngano. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake na alikuwa amepewa maneno machache yenye maana pana: "Kile chenye lewesha ni haramu".
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye hiji kwa kutaka radhi za Allah Mtukufu na akawa hakufanya yasiyofaa; Na yasiyofaa hapa maana yake ni tendo la ndoa na vitangulizi vyake, kama busu, kugusana, neno hili hutumika pia kumaanisha maneno machafu, na akawa hakufanya uovu; kwa kufanya maasi na madhambi, Na miongoni mwa uovu ni kufanya makatazo ya ihiramu (Hija), atarudi kutoka katika hija yake akiwa kasamehewa, kama azaliwavyo mtoto akiwa amesalimika kutokana na madhambi.
Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuswali kinapotengwa chakula kile anachokitamani mwenye kuswali, na moyo wake umefungamana nacho. Na vile vile amekataza kuswali mtu akiwa anazuia haja mbili -nazo ni mkojo na haja kubwa-, kwakuwa atashughulika na kuzuia udhia.
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika adabu za wajibu kwa atakayehudhuria hotuba ya Ijumaa: Ni kunyamaza na kumsikiliza hatibu; ili mtu azingatie mawaidha, nakuwa atakayezungumza walau kwa jambo dogo, na imamu akihutubu, akasema kumwambia mwenzie: "Nyamaza" na "Sikiliza", basi zitakuwa zimempita fadhila za swala ya Ijumaa.
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mambo matano katika dini ya Uislamu na sunna ya Mitume: La kwanza: Kutairi, nako ni kukata ngozi iliyozidi juu ya kichwa cha dhakari kwa mwanaume, na kukata kingozi katika tupu ya mwanamke juu ya malaha palipo tundu la uke. La pili: Kunyoa sehemu za siri, nako ni kunyoa nywele za kinena zinazozunguka tupu ya mbele. La tatu: Kupunguza masharubu, nako ni kupunguza kilichoota juu ya mdomo wa juu wa mwanaume mpaka mdomo uonekane wazi. La nne: Kupunguza kucha. La tano: Kunyofoa nywele za kwapa.
Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kupunguza sharubu na zisiachwe bali zipunguzwe, na azidi kupunguza zaidi. Na pamoja na hilo anaamrisha kufuga ndevu na kuziacha zikichanua.
Othman -Radhi za Allah ziwe juu yake- alifundisha sifa ya udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa njia ya vitendo; Ili ueleweka vizuri zaidi, akaomba maji katika chombo, akamimina katika mikono yake mara tatu, na baada ya hapo aliingiza mkono wake wa kulia katika chombo, na akachukua maji akayazungusha kinywani mwake na akayatoa, kisha akavuta kwa pumzi yake kuja ndani ya pua yake, kisha akayatoa na akayapenga, kisha akaosha uso wake mara tatu, kisha akaosha mikono yake pamoja na viwiko viwili mara tatu, kisha akapitisha mkono wake juu ya kichwa chake ukiwa umeloa kwa maji mara moja, kisha akaosha miguu yake pamoja na fundo mbili mara tatu. Alipomaliza radhi za Allah ziwe juu yake akawaeleza kuwa yeye alimuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha mfano wa udhu huu, na akawapa bishara -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayetawadha mfano wa udhu wake, na akaswali rakaa mbili, kwa utulivu na kuhudhuriasha moyo mbele ya Mola wake Mtukufu ndani yake, basi Allah atamlipa kwa udhu huu mkamilifu na kwa swala hii iliyotakaswa kwa kumsamehe yaliyotangulia katika madhambi yake.