





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika kundi la kwanza la watu watakaoingia peponi watakuwa katika sura ya mwezi usiku wa tarehe kumi na tano, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali ing'aayo na iangazayo mbinguni, hawatokwenda haja ndogo wala kubwa, na wala hawatotema mate wala kupenga kamasi, vitana vyao vitakuwa vya dhahabu, jasho lao litakuwa ni miski, na vitezo vyao vitakuwa vikinukia udi wenye harufu nzuri mno, udi wa marashi, na wake zao watakuwa ni katika Mahurulaini, na wote watakuwa katika umbile la mtu mmoja, watakuwa katika sura ya baba yao Adam, urefu kwenda juu ni dhiraa sitini (Dhiraa moja ni inchi 18)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kundi la kwanza la waumini watakaoingia peponi nyuso zao zitakuwa na sura ya mwezi unapokuwa usiku wa tarehe kumi na tano katika mg'ao, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali yenye mng'ao na mwangaza katika mbingu, watakuwa na sifa za ukamilifu kiasi kwamba hawatokojoa, wala kujisaidia haja kubwa, na wala hawatotema mate wala kupenga kamasi, vitana vyao ni vya dhahabu, na jasho lao ni miski, na vitezo vyao vitakuwa vinafuka hurufu nzuri mno, na udi mzuri zaidi, na wake zao watakuwa ni Mahurulaini, umbile lao litakuwa kama umbile la mtu mmoja, watakuwa katika sura ya baba yao Adam katika urefu na umbile; ulikuwa urefu wa mwili wake ni dhiraa sitini kwenda juu.
Kutoka kwa Ubaada bin Swaamit radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Peponi kuna daraja mia moja baina ya kila daraja mbili ni kama umbali wa mbingu na ardhi, na Firdausi iko daraja ya juu zaidi kuliko zote, na ndani yake ndiko inako chimbuka mito yote minne ya pepo, na juu yake ndiko inakokuwa Arshi, Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa peponi kuna daraja na vituo mia moja, na masafa yaliyopo kati ya daraja mbili ni kama masafa kati ya mbingu na ardhi, na Pepo ya juu zaidi miogongoni mwa Pepo hizi ni Pepo ya Firdausi, na ndani yake ndiko inapochimbuka mito yote minne ya Pepo, na juu ya Firdausi ndiko inakokuwa Arshi; mkimuomba Mwenyezi Mungu basi muombeni Firdausi; kwani ndiyo iko juu ya Pepo zote.
Kutoka kwa Mughira bin Shuuba -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Halitoacha kuendelea kudhihiri kundi katika Umma wangu, mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mungu nao wakiwa katika kudhihiri huko".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa hawatoacha watu katika Umma wake kuendelea kuwepo, na kuwashinda wanaopingana nao, na hilo litaendelea mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mungu kwa kuchukuliwa roho zao mwisho wa zama za dunia kabla ya kusimama kwa Kiyama.
Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtu yeyote atakayesema kumwambia ndugu yake: Ewe kafiri, basi utampata mmoja katika ya hao wawili, ikiwa atakuwa kama alivyosema (litathibiti hilo), na kama si hivyo utarejea kwake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmemtahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kusema kumwambia ndugu yake muislamu: Ewe kafiri, basi atakuwa kastahiki neno kafiri mmoja wao, na ikiwa ni kweli kama alivyosema (utamthibitikia), na kama si kweli ukafiri utarejea kwa msemaji aliyesema kumwambia ndugu yake.
Kutoka kwa Imrani bin Huswain radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Karne bora ni karne yangu, kisha wale wanaowafuata, kisha wale wanaowafuata" Amesema Imrani: Sijui alitaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadaye karne mbili au tatu, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika baada yenu kutakuja watu wanaofanya hiyana na wala hawaaminiwi, na wanatoa ushahidi na wala hawatakwi ushahidi, na wanatoa nadhiri na wala hawatimizi, na utadhihiri kwao unene".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa tabaka bora la watu waliokusanyika katika zama moja ni tabaka ambalo yuko ndani yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Maswahaba zake, kisha wale wanaowafuata katika waumini wale waliowapata Maswahaba na hawakumpata Mtume wa Mwenyezi Mungu, kisha wale wanaowafuata nao ni wafuasi wa wanafunzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akapata wasi wasi swahaba katika kutaja wale wanaowafuata kwa karne ya nne. Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika baada yao kuna kizazi (kaumu) watafanya hiyana na wala watu hawatowaamini, na watatoa ushahidi kabla ya kutakwa kutoa ushahidi, na wanatoa nadhiri na wala hawatimizi, na wanachupa mipaka katika ulaji na unywaji mpaka unadhihiri kwao unene.
Kutoka kwa Abuu Tha'laba Al-Khushani Jurthuum bin Naashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha faradhi basi msizipoteze, na akaweka mipaka basi msiivuke, na akaharamisha vitu basi msivivamie, na akayanyamazia mambo kwa kukuhurumieni si kwa kusahau basi msiyatafute".
Imepokelewa na Addar- Alqutni katika Sunanu yake na wengineoAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu amewajibisha mambo na akafaradhisha faradhi basi shikamaneni nazo na wala msifanye uzembe katika hayo kwa kuyaacha au kuzembea ndani yake, na akakuwekeeni vizuizi na makemeo yaliyokadiriwa yanayokuzuieni na kukukemeeni katika yale asiyoyaridhia, msizidishe zaidi ya yale yaliyoamrishwa na sheria, na akaharamisha maharamisho kadhaa msiyachukue na wala msiyakaribie, na yasiyokuwa hayo kayaacha na akayanyamazia kwa kuwahurumia waja wake, hivyo yanabakia katika asili ya uhalali wake basi msiyatafute.
Kutoka kwa Abuu Muhammadi Al-Hasan bin Ally bin Abii Twalib mjukuu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na marashi yake (kipenzi chake), amesema: Nilihifadhi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia shaka."
Imepokelewa na Tirmidhiy na NasaaiAmeamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha lile linalokutia shaka ndani yake katika kauli na matendo kuwa limekatazwa au la, je ni halali au ni haramu, na ufanye yale usiyo na shaka nayo katika yale uliyo na uhakika na uzuri wake na uhalali wake.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Ya'la Shaddad bin Ausi -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alisema: "Hakika Mwenyezi Mungu amefaradhisha (kutenda) wema katika kila kitu, hivyo mtakapoua basi uweni vizuri (kwa wema), na mtakapochinja basi chinjeni vizuri, na anowe mmoja wenu kisu chake, na akistareheshe kichinjwa chake".
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuwajibishia kutenda wema katika kila kitu, na wema: Ni kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu daima, na katika ibada zake, na katika kutenda kheri na kuacha kuwaudhi viumbe, miongoni mwa hayo ni kutenda wema katika kuuwa na kuchinja. Wema katika kuuwa ni wakati wa kisasi: Achague njia nyepesi na rahisi zaidi na ya haraka zaidi kutoa roho kwa mwenye kuuawa. Na wema katika kuchinja ni wakati wa kuchinja: Amuhurumie mnyama kwa kunoa kifaa, na kisinolewe mbele ya mnyama akitazama, na asichinjwe hali yakuwa wanyama wenzake wanatazama.
Imepokelea kutoka kwa Abii Maalik Al-Ash-ariy radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi, na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye huiuza nafasi yake yuko anayeikomboa kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".
Imepokelewa Imamu MuslimAnafahamisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa twahara na usafi wa nje ambao ni udhu na kuoga ni sharti la usahihi wa swala. Na kuwa neno: "Alhamdulillah hujaza mizani" nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu aliyetakasika na machafu, na kumsifia kwa sifa za ukamilifu zitakazopimwa siku ya kiyama na kuijaza mizani ya matendo. Na kuwa neno: "Sub-hanallah na Alhamdulillah" na maneno hayo ni kumtakasa Mwenyezi Mungu na kumsifia kwa sifa zilizokamilika na zilizotimia ambazo anastahiki sifa hizo pamoja kumpenda yeye na kumtukuza hujaza sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi. Na kuwa "Swala ni nuru" ya mja katika moyo wake, na katika uso wake na kaburini mwake na siku ya kufufuliwa kwake. Na kuwa "Sadaka ni ushahidi" Na ni dalili ya ukweli wa imani ya muumini, na tofauti yake na mnafiki ambaye huzuia kutoa sadaka kwa kuwa mnafiki haamini malipo ya kutoa sadaka. Na "kuwa subira ni mwangaza" -na subira ni kuizuia nafsi kutoku papatika na kuwa na hasira, subira ni nuru inayokuwa na joto na kuunguza, kama vile mwanga wa Jua; kwa sababu subira ni tabu kubwa inahitaji kuilazimisha nafsi na kuizuia na kile inachokipenda; hivyo haachi kuwa na mng'ao mtu mwenye subira, mwenye kuongoka na mwenye kudumu katika usahihi, nako ni kusubiri katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kutomuasi yeye, na kuwa na subira kwenye matatizo na aina mbalimbali za mambo yenye kuchukiza katika Dunia. Na kuwa "Qur'ani ni hoja kwako wewe" kwa kuisoma na kuifanyia kazi, au yaweza kuwa " Hoja dhidi yako" kwa kuiacha pasina kuifanyia kazi au kuisoma. Kisha akafahamisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakuwa watu wote huenda mbio na hutawanyika na huamka toka usingizini mwao na wanatoka kwenye majumba yao kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali miongoni mwao kuna wenyekuwa na msimamo katika kumtii Mwenyezi Mungu, hivyo anakuwa ameikomboa nafsi yake na moto, na miongoni mwao kuna mwenye kwenda kinyume na kuacha kumtii Mwenyezi Mungu na akaingia katika maasi, hivyo akaiangamiza na kuingia motoni.