





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, na likiwa si la mtu mwema basi husema: Ubaya ulioje, mnalipeleka wapi? Huisikia sauti yake kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angelisikia basi angezimia".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba Jeneza likiwekwa kitandani, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, kwa yale linayoyaona mbele yake katika neema, na likiwa si la mtu mwema, hupiga yowe kwa sauti mbaya ya kukera, na kusema: Nasikitika kwa maangamivu yake, mnalipeleka wapi?! kwa yale linayoyaona mbele yake miongoni mwa adhabu, inasikika sauti yake kwa kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angeliisikia basi angezimia kutokana na ukubwa wa kile alichosikia.
Imepokelewa kutoka kwa Mikidadi bin Aswadi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Jua litasogezwa karibu na viumbe Siku ya Kiyama mpaka liwe karibu nao umbali wa maili moja.", Sulaim bin 'Amir akasema: "Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, sijui (kiwango) alimaanisha nini kwa "maili"? Je, ni umbali katika ardhi au ni kile kijiti kinachotumiwa kupaka wanja wa manga kwenye jicho." (Mtume) Akasema: "Kisha, watu watakuwa ndani ya jasho yao kulingana na matendo yao. Miongoni mwao, kuna ambaye litakuwa hadi kwenye vifundo viwili vya miguu yake. Na miongoni mwao, kuna ambaye litakuwa hadi kwenye magoti yake mawili. Na miongoni mwao, kuna ambaye litakuwa hadi kwenye nyonga zake mbili. Na miongoni mwao, kuna ambaye jasho (lake) litammeza kabisa."
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Jua litasogezwa siku ya Kiyama karibu na viumbe, mpaka liwe vichwani mwao kwa kiasi cha maili moja. Amesema taabii (Mwanafunzi wa swahaba) Saidi bin Aamiri: Wallahi sijui ni maili mbili zipi alikusudia, je ni masafa ya ardhi, ama ni maili (wanja) ambao hutumika kupaka macho? Akasema: Watakuwa katika jasho kulingana na amali zao; yuko miongoni mwao ambaye jasho lake litatiririka mpaka chini ya kongo mbili zake za miguu, na yuko ambaye jasho lake litatiririka mpaka magotini, na yuko ambaye jasho litakuwa katika kitovu chake na kiunoni kwake, na yuko ambaye jasho litafika katika mdomo wake na litamzuia kuzungumza. Amesema: Na akaashiria rehema na amani ziwe juu yake kwa mkono wake katika kinywa chake.
Kutoka kwa Abuu Burda bin Abii Mussa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliumia Abuu Mussa maumivu makali, akazimia na kichwa chake kikiwa katika paja la mwanamke katika wake zake, akawa hakuweza kumjibu chochote, alipozinduka, akasema: Mimi najitenga mbali na yule aliyejitenga mbali naye Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alijitenga mbali na mpiga mayowe, na mnyoa nywele, na mchana nguo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmesimulia Abuu Burda radhi za Allah ziwe juu yake kuwa baba yake Abuu Mussa Al-Ash'ary radhi za Allah ziwe juu yake aliugua maradhi makali, akazimia, na kichwa chake kilikuwa katika paja la mwanamke mmoja katika wake zake, akapiga mayowe yule mwanamke kwa kumuita, akawa hakuweza kumjibu chochote kwa sababu ya kuzimia kwake. Alipozinduka akasema kuwa: Hakika yeye anajitenga mbali na yule aliyejitenga mbali naye Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hakika yeye rehema na amani ziwe juu yake alijitenga naye. Mpiga mayowe: Naye ni mwanamke anayenyanyua sauti yake wakati wa msiba. Na mnyoaji: Ni mwanamke anayenyoa nywele zake wakati wa msiba. Na mchana nguo: Ni mwanamke anayechana nguo zake wakati wa msiba. Kwa sababu haya ni katika mambo ya zama za ujinga, bali aliamrisha kuwa na subira wakati wa msiba, na kutaraji malipo yake kwa Mwenyezi Mungu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni sita" Pakasemwa: Na ni zipi hizo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?, akasema: "Ukikutana naye msalimie, na akikuita muitikie, na akikutaka nasaha mnasihi, na akipiga chafya akamhimidi Mwenyezi Mungu basi muombee dua ya rehema, na akiugua mtembelee, na akifariki msindikize".
Imepokelewa Imamu MuslimAmebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa miongoni mwa haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu ni mambo sita: La kwanza: Amsalimie akikutana naye kwa kusema: Assalaam alaikum, naye atajibu salamu kwa kusema: Waalaikumussalaam. La pili: Kuitika wito wake atakapomuita kwa ajili ya sherehe ya harusi au nyingineyo. La tatu: Kumpa nasaha akizihitajia, na wala usimsifie bure, au kumfanyia udanganyifu. La nne: Akipiga chafya akasema: Alhamdulillaah, basi muombee dua kwa kusema: Yar-hamkallaah (Akuhurumie Mwenyezi Mungu), naye ajibu kwa kusema: Yah-diikumullaahu wayuslih baalakum (Akuongozeni Mwenyezi Mungu na kutengenezeeni hali zenu). La tano: Akamuone na amtembelee atakapougua. La sita: Amswalie atakapofariki, na alisindikize jeneza lake mpaka azikwe.
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa katika maradhi yake ambayo hakuweza kuamka tena: "Amewalaani Mwenyezi Mungu Mayahudi na Wakristo, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kusalia" Akasema: Na lau kama isingekuwa kauli hiyo basi lingenyanyuliwa kaburi lake, isipokuwa ilihofiwa kufanywa kuwa mahali pa kuswalia.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema akiwa katika maradhi yake ambayo yalikuwa makali na akafariki ndani yake: Mwenyezi Mungu aliwalaani Mayahudi na Wakristo, na aliwafukuza kutoka katika rehema yake; na hii ni kwa sababu wao waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kuswalia, na hii ni kwa kuyajengea au kuswali hapo au kwa kuyaelekea. Kisha akasema radhi za Allah ziwe juu yake: Na lau kama si katazo hilo na tahadhari hiyo kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na hofu ya Maswahaba kufanywa kaburi la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kama walivyofanya Mayahudi na Wakristo kwa makaburi ya Manabii wao, basi lingedhihirishwa na kunyanyuliwa kaburi lake.
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Kudry -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alituma Dhahabu Ally bin Abii Twalib kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokea Yemen, ikiwa ndani ya kipande cha ngozi iliyochubuliwa, ambayo haijapembuliwa kutoka katika udongo wake, akasema: Akaigawa baina ya watu wanne, kati ya Uyaina bin Badri, na Aqrau bin Haabisi, na Zaidul Khairi, na wa nne alikuwa kati ya Alqama au Aamiri bin Tufail, akasema: Likamfikia hilo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Hivi hamna imani na mimi hali yakuwa mimi ni muaminiwa wa yule aliyeko mbinguni, zinanijia habari za mbingu asubuhi na jioni" Anasema: Akasimama bwana mmoja mwenye macho yaliyotumbukia ndani, mwenye uso uliokunjamana na mwenye paji la uso lililotokeza, mwenye ndevu nyingi, mwenye kipara, aliyekunja kikoi chake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mche Mwenyezi Mungu. Akasema: "Koma! Hivi kwani mimi si mtu ninayestahiki zaidi kumcha Mwenyezi Mungu katika watu wa ardhini" Anasema msimulizi: Kisha yule bwana akaondoka. Akasema Khalidi bin Walidi: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi ni kwa nini nisikate kichwa chake? Akasema: "Hapana, huenda akawa anaswali" Akasema Khalidi: Na ni watu wangapi wanaoswali wanasema kwa ndimi zao yasiyokuwa mioyoni mwao?, Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi sikuamrishwa kutoboa nyoyo za watu, wala kupasua matumbo yao" Anasema: Kisha akamtazama akiwa kampa kisogo, akasema: "Hakika watatoka katika kizazi cha huyu bwana watu wanaosoma kitabu cha Mwenyezi Mungu kikiwa kibichi (kwa uhodari), lakini hakivuki shingo zao, wanatoka katika dini kama mshale unavyotoka katika upinde", na ninadhani pia alisema: "Ikiwa nitakuwa hai nikawapata, basi nitawaua kifo cha Thamudi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliagiza Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kipande cha dhahabu kutoka Yemen, kikiwa katika ngozi iliyolowekwa na kukwanguliwa, na dhahabu ilikuwa haijapembuliwa kutoka katika udongo wake, akasema: Akaigawanya Mtume rehema na amani ziwe juu yake baina ya watu wanne: Uyaina bin Badri Al-Fazaari, na Aqrau bin Haabisi Al-Handhwali, na Zaidul-Khaili Al-Nab-haani, na Alqama bin Ulaatha Al-Aamiry, bwana moja katika Maswahaba zake akasema: Sisi ndiyo tulikuwa na haki zaidi kuliko hawa, akasema: Hilo likamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Hivi hamna imani na mimi hali yakuwa mimi ni muaminiwa wa aliyembinguni, zinanijia mimi habari za mbinguni asubuhi na jioni." Anasema: Akasimama mtu mmoja mwenye macho madogo, yaliyoingia ndani ya kope zake, mwenye mashavu makubwa, na mwenye paji refu lililotokeza, na ndevu zake ni nyingi lakini si ndefu, mwenye kipara, na kikoi chake kiko juu upande wa chini wa mwili wake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mche Mwenyezi Mungu, akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Koma!, hivi kwani mimi si mtu mwenye haki zaidi kwa viumbe wa ardhini kumuogopa Allah?!". Anasema: Kisha yule bwana akaondoka, akasema Khalidi bin Walidi: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi ni kwa nini nisikate kichwa chake? Akasema: Hapana, huenda akawa anaswali, Khalidi akasema: Kwani wa ngapi wanaoswali lakini wanasema kwa ndimi zao yasiyokuwa mioyoni mwao?, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Mimi sikuamrishwa kutoboa nyoyo ili kutazama yaliyoko ndani ya nyoyo za watu, wala kupasua matumbo yao; bali nimeamrishwa nichukue yale yanayodhihiri katika mambo yao, akasema: Kisha akamtazama yule akiwa kampa kisogo, akasema: Hakika watatoka watu kutoka katika kizazi cha huyu au kabila lake, watu mahiri katika kusoma kitabu cha Allah, tena kwa sauti nzuri, ndimi zao saa zote ni mbichi kwa wingi wa kukisoma kwake, lakini Qur'ani haivuki koo zao nyoyo zao zikaifahamu ikazitengeneza, na wala Mwenyezi Mungu hainyanyui wala haikubali Qur'ani hiyo wasomayo, watakuwa wakitoka ndani ya Uislamu kama utokavyo mshale katika upinde, kwa kasi na wepesi. Na ninadhani alisema: Nikifika kuwa hai wakati wanatoka dhidi ya waislamu kwa mapanga nitawaua kifo kibaya kama kaumu ya Thamudi.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira Allah amridhie kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika, mwenye kiwango cha chini zaidi kati yenu katika Pepo ni kwamba ataambiwa: "Tamani!" Basi atatamani na atamani, na ataambiwa: "Je umeshatamani?" Atasema: "Nidyo." Ataambiwa: "Ni vyako vyote ulivyotamani, na mfano wake pamoja navyo."
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye nafasi na daraja ndogo zaidi kwa wale watakaoingia peponi, ataambiwa: Tamani, basi atatamani, na atatamani tena, mpaka atafikia mahali ataishiwa yote ya kutamani isipokuwa atayataja, hapo ataambiwa: Je, umetamani umefika mwisho? Atasema: Ndiyo, hapo ataambiwa: Basi ni vyako vyote ulivyotamani na mfano wake pamoja navyo.
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliletewa nyama, akaletewa mkono wa mbuzi, na alikuwa akiupenda, akang'ata kiasi kidogo katika nyama ile, kisha akasema: "Mimi ndiye bwana wa watu siku ya Kiyama, na je, mnajua ni kwa sababu gani hilo? Mwenyezi Mungu atawakusanya watu wa mwanzo na mwisho katika udongo mmoja, atawasikilizisha mwenye kunadi, na atawapa upeo wa kuona, na jua linaposogea, watu watafikwa na tabu na matatizo kiasi ambacho hawatoweza kuvumilia, watu watasema: Hivi hamuoni kilichowafikia, hivi hamtafuti wa kukuteteeni kwa Mola wenu Mlezi? Hapo watasema baadhi yao kuwaambia baadhi: Nendeni kwa Adam, watamuendea Adam amani iwe juu yake, watasema kumwambia: Wewe ndiye baba wa wanadam, Mwenyezi Mungu alikuumba kwa mkono wake, na akakupulizia katika roho yake, na akawaamrisha Malaika wakakusujudia, tutetee kwa Mola wako Mlezi, hivi huoni hali tuliyonayo, na huoni hali iliyotufika? Adam atasema: Hakika Mola wangu leo hii ameghadhibika ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake, na hatoghadhibika tena baada yake mfano wake, na hakika alinikataza kuhusu mti mimi nikamuasi, leo nalia na nafsi yangu nafsi yangu, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Ibrahim, watamuendea Ibrahim na watasema: Ewe Ibrahim wewe ni Nabii wa Mwenyezi Mungu na mwandani wake katika wakazi wa Ardhini, tutetee kwa Mola wako, hivi kwani huoni hali tuliyonayo? Atasema: Hakika Mola wangu leo hii ameghadhibika ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake, na hatoghadhibika tena baada yake mfano wake, na hakika mimi nilisema uongo mara tatu, leo ninalia na nafsi yangu nafsi yangu, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Issa bin Mariam, watamuendea Issa na watasema: Ewe Issa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ni neno lake alilolipeleka kwa Mariam na ni roho kutoka kwake, na uliwasemesha watu ukiwa mtoto mchanga katika mbeleko, tutetee kwa Mola wako, hivi huoni hali tuliyonayo? Issa atasema: Hakika Mola wangu leo hii ameghadhibika ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake, na hatoghadhibika tena baada yake mfano wake katu, na hatotaja dhambi, leo nalia na nafsi yangu nafsi yangu, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Muhammadi, watamuendea Muhammadi na watasema: Ewe Muhammadi wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na ni mwisho wa Manabii, na alikwisha kusamehe Mwenyezi Mungu madhambi yako yaliyotangulia na yajayo, tutetee sisi kwa Mola wako, hivi huoni hali tuliyonayo?, hapo nitaondoka na nitakwenda mpaka chini ya Arshi, nitaporomoka kumsujudia Mola wangu Aliyetakasika na kutukuka, kisha atanifungulia Mwenyezi Mungu katika sifa zake na himdi zake, na sehemu katika kumtukuza, kwa kiasi ambacho hajawahi kumfungulia yeyote kabla yangu, kisha patasemwa: Ewe Muhammadi nyanyua kichwa chako, omba upewe, na omba utetezi ukubaliwe, hapo nitanyanyua kichwa changu, na nitasema: Umma wangu ewe Mola wangu, Umma wangu ewe Mola wangu, Umma wangu ewe Mola wangu, patasemwa: Ewe Muhammadi waingize peponi katika Umma wako wale wasiokuwa na hesabu kwa kupitia mlango wa kulia katika milango ya pepo, nao watashirikiana na watu wengine pia kupita katika milango mingine tofauti na huo, kisha akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika masafa yaliyoko baina ya fremu mbili katika fremu za milango ya pepo ni sawa na masafa kutoka Makka kwenda Himyari (Yemen) au ni kama masafa ya kutoka Makka kwenda Basra (Iraq) (Km. 1287)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake pamoja na Maswahaba zake katika mwaliko wa chakula, akaletewa mguu wa mbuzi, na nyama yake alikuwa akiipenda, akang'ata sehemu katika nyama hiyo kwa ncha ya meno yake, kisha akawahadithia, akasema: Mimi ndiye bwana wa watoto wa Adam siku ya Kiyama; na alisema hili kama kusimulia neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kisha akasema: Hivi mnajua hilo ni kwa sababu gani? Akasema: Hii ni kwa sababu watu watakusanywa siku ya Kiyama katika Ardhi pana iliyolingana sawa ilinyooka kikamilifu, na walio katika eneo hilo itawafikia sauti ya mwenye kunadi, na mwenye kuwatazama atawaeneza hakuna chochote kitakachofichikana kwake; kwa sababu ya Ardhi kulingana, hakuna kinachoweza kumkinga mwenye kutazama, na macho yanaweza kuona vizuri, maana yake lau kama mtu atazungumza sauti yake itamfikia wa mwisho wao, na macho yatawaona, na Jua litasogea karibu na viumbe kwa kiasi cha maili moja, na watakumbwa na msongo na matatizo kiasi ambacho hawatayaweza wala hawawezi kuvumilia, hapo watataka kujinasua kwa kupata utetezi. Mwenyezi Mungu atawafungua fikra waumini waende kwa Adam baba wa watu, watamuendea na watataja fadhila zake, huenda akawatetea mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, watasema kumwambia: Wewe ni Adam baba wa wanadam, Mwenyezi Mungu alikuumba kwa mkono wake, na akawafanya Malaika wakusujudie, na akakufundisha majina ya kila kitu, na akapuliza kwako katika roho yake, hapo ataomba udhuru na atasema: Hakika Mola wangu ameghadhibika leo ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika kabla yake mfano wake, na wala hatoghadhibika baada yake mfano wake, kisha atataja dhambi lake, nalo nikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimkataza asile kutoka katika mti ila yeye akala, na atasema: Nafsi yangu ndiyo inahaki zaidi ya kutetewa, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Nuhu. Watakwenda mpaka kwa Nuhu; na watasema: Wewe ndiye mtu wa mwanzo aliyemtuma Mwenyezi Mungu kuja kwa watu wa Ardhi, nakuwa Mwenyezi Mungu alikuita kuwa wewe ni mja mwenye shukurani, lakini naye atatoa udhuru kuwa: Mwenyezi Mungu ameghadhibika leo ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake kabla ya hapo, na wala hatoghadhibika baada yake mfano wake, nakwamba yeye kulikuwa na dua mbaya ambayo aliwaombea watu wake, na atasema: Bali nafsi yangu ndiyo inastahiki kuombewa utetezi zaidi, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Ibrahim. Watamwendea Ibrahim na watasema: Wewe ndiye kipenzi mwandani wa Mwenyezi Mungu katika Ardhi, tutetee sisi kwa Mola wako, kwani huoni hali tuliyonayo?! Atasema kuwaambia: Hakika Mola wangu leo ameghadhibika ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake kabla ya hapo, na wala hatoghadhibika baada ya hapo mfano wake, na hakika mimi nilisema uongo mara tatu; nayo ni kauli yake: Hakika mimi ni mgonjwa, na kauli yake: Amefanya mkubwa wao huyu, na kauli yake kwa mke wake Sara: Mwambie kuwa mimi ni kaka yako, ili asalimike na shari zake. Na ukweli nikuwa maneno haya matatu yalikuwa ni katika maneno ya majibizano, lakini kwakuwa sura yake ilivyokuwa ni sura ya uongo alihofia kwa kuiona ndogo nafsi yake katika swala la utetezi; kwa sababu mwenye kumtambua Mwenyezi Mungu na akawa na nafasi ya karibu zaidi basi huwa na hofu kubwa, na anasema: Nafsi yangu ndiyo inastahiki zaidi kuombewa utetezi, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Mussa. Watamwendea Mussa na watasema: Ewe Mussa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu alikufanya kuwa bora kwa ujumbe wake na kwa kuzungumza naye, tutetee sisi kwa Mola wako, kwani huoni hali tuliyonayo?! Atasema: Hakika Mola wangu leo ameghadhibika ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake kabla ya hapo, na wala hatoghadhibika baada ya hapo mfano wake, na hakika mimi niliua nafsi ambayo sikuamrishwa kuiua, basi nafsi yangu ndiyo inastahiki zaidi kuombewa utetezi, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Issa bin Mariam. Watamwendea Issa na watasema: Ewe Issa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ni neno lake alilopeleka kwa Mariam na ni roho kutoka kwake, na uliwasemesha watu ukiwa mtoto mchanga katika mbeleko, tutetee sisi kwa Mola wako, kwani huoni hali tuliyonayo?! Atasema: Hakika Mola wangu leo ameghadhibika ghadhabu ambayo hajawahi kughadhibika mfano wake kabla ya hapo, na wala hatoghadhibika baada ya hapo mfano wake katu, na hakutaja dhambi, nafsi yangu ndiyo inastahiki zaidi kuombewa utetezi, nendeni kwa mwingine, nendeni kwa Muhammadi. Watamuendea Muhammadi na watasema: Ewe Muhammadi wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na ni mwisho wa Manabii, na alikwisha kukusamehe wewe Mwenyezi Mungu madhambi yako yaliyotangulia na yajayo, tutetee sisi kwa Mola wako, kwani huoni hali tuliyonayo?! Hapo nitaondoka nitakwenda mpaka ntafika chini ya Arshi, nitaporomoka kwa kumsujudia Mola wangu Aliyetakasika na kutukuka, kisha atanifungulia Mwenyezi Mungu katika himidi zake, kumsifia vizuri kwa kiasi kidogo, kiasi ambacho hakuwahi kumfungulia yeyote kabla yangu, kisha patasemwa: Ewe Muhammadi, nyanyua kichwa chako, omba upewe, taka utetezi ukubaliwe, hapo nitanyanyua kichwa changu na nitasema: Umma wangu ewe Mola wangu, Umma wangu ewe Mola wangu, Umma wangu ewe Mola wangu, basi utapokelewa utetezi wangu. Na ataambiwa: Ewe Muhammadi waingize katika Umma wako wale wasiokuwa na hesabu juu yao kupitia mlango wa kulia katika milango ya pepo, nao watashirikiana na watu wengine katika milango mingine usiokuwa huo katika milango. Kisha akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika masafa yaliyopo baina ya mlango mmoja katika milango ya pepo, ni sawa na masafa kati ya Makka na Sanaa Yemen, au kama baina ya Makka na Basra ya Sham ambao ndio mji wa Hauraa.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amemlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume anayevaa vazi la mwanamke, na mwanamke anayevaa vazi la mwanaume.
Imepokelewa na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah kwa maana yake na AhmadAliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu kwa kila mwanaume atakayejifananisha na mwanamke katika mavazi maalumu kwa ajili ya wanawake; sawa sawa iwe katika muonekano au rangi au jinsi au namna ya uvaaji na kujipamba. Au kwa mwanamke kujifananisha na mavazi maalumu kwa wanaume vile vile, nalo ni dhambi katika madhambi makubwa.