





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapowaamrisha anawaamrisha katika matendo yale wanayoyaweza, wakasema: Sisi hatuna nafasi kama yako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu amekusamehe yaliyotangulia katika madhambi yako na yajayo, basi anachukia mpaka anaonekana usoni kuwa amechukia, kisha anasema: "Hakika mchamungu wenu na mwenye kumjua zaidi Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi ni mimi".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAnaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapowaamrisha watu amali miongoni mwa amali anawaamrisha kwa jambo ambalo ni jepesi kwao na si zito, kwa kuhofia wasijekushindwa kudumu nalo, na yeye pia anafanya mfano walile alilowaamrisha katika wepesi, lakini wao walimuomba kubebeshwa magumu, kwa kudhania kwao kuwa wana haja ya kuzidisha zaidi katika amali kwa sababu yeye amenyanyuliwa daraja zaidi. Wanasema: Hakika sisi hatuko katika hali kama ya kwako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu amekusamehe yaliyotangulia katika madhambi yako na yajayo, basi anakasirika mpaka hasira inajulikana usoni kwake, kisha anasema: Hakika mchamungu wenu zaidi na mjuzi wenu kwa Mwenyezi Mungu ni mimi, basi fanyeni yale ninayowaamrisha.
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Sisi ni Umma wa mwisho, na ndio wa kwanza kuhesabiwa, patasemwa: Uko wapi Umma usiosoma na Nabii wao? Sisi ni wa mwisho wa mwanzo".
Imepokelewa na Ibnu MaajahAlieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Umma wake ndio Umma wa mwisho kuwepo na zama pia, na ndio Umma wa kwanza katika Umma zote utakaohesabiwa siku ya Kiyama, patasemwa siku ya Kiyama: Uko wapi Umma usiosoma na Nabii wao? Umenasibishwa katika kutojua kusoma kwake rehema na amani ziwe juu yake kwa kutojua kusoma wala kuandika. Wataanza kuitwa mwanzo kwa ajili ya hesabu, sisi ni wa mwisho katika zama za kuwepo, na wa kwanza katika kuhesabiwa siku ya Kiyama na katika kuingia Peponi.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayeswali swala yetu na akaelekea kibla chetu na akala kichinjwa chetu basi huyo ni Muislamu mwenye dhima ya Mwenyezi Mungu na dhima ya Mtume wake, msimfanyie hiana Mwenyezi Mungu katika dhima yake".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayeshikamana na nembo za dini za wazi akaswali mfano wa swala yetu, na akaelekea upande wa Ka'aba Kibla yetu, na akala kichinjwa chetu kwa kuamini kuwa ni halali; basi huyu ndio Muislamu ambaye anadhima ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na ahadi yake, msitengue amani ya Mwenyezi Mungu na ahadi yake ndani yake.
Kutoka kwa Ummu Salama radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu: "Innaa lillaahi wa innaa ilaihi raajiuun" (Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea) [Baqara: 156], Ewe Mwenyezi Mungu nilipe katika msiba wangu, na unipe badala bora kuliko hili, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa badala bora kuliko hiyo" Akasema: Alipofariki Abuu Salama, nikasema: Ni Muislamu gani atakuwa bora kuliko Abuu Salama? Nyumba ya kwanza aliyohamia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha mimi nikasema maneno hayo, Mwenyezi Mungu akanipa mbadala wake ambaye ni Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza mama wa waumini Ummu Salama radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema siku moja: Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyopendezeshewa na Mwenyezi Mungu kwake kuyasema: "Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea" [Baqara: 156], "Ewe Mwenyezi Mungu nilipe" na unipe malipo ya subira yangu "katika msiba wangu", na unipe badala "na unirejeshee" kwa hilo "kheri kuliko hiyo"; isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa mbadala bora kuliko hilo. Akasema: Alipofariki Abuu Salama akasema: Ni nani katika Waislamu atakuwa bora kuliko Abuu Salama?! Nyumba ya kwanza iliyohama kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha mimi Mwenyezi Mungu alinisaidia nikaisema kauli hiyo, Mwenyezi Mungu akanipa badala Mtume rehema na amani ziwe juu yake bora zaidi kuliko Abuu Salama.
kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema kumwambia Bilali wakati wa swala ya Alfajiri: "Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye matarajio makubwa zaidi uliyowahi kuifanya ndani ya Uislamu, kwani mimi nilisikia mkanyago wa viavu vyako mbele yangu huko Peponi" Akasema: Sijawahi kufanya amali yoyote yenye matarajio kwangu isipokuwa sijawahi kutia udhu wowote, katika nyakati za usiku au mchana, isipokuwa ninaswali kwa udhu huo kiasi nilichoandikiwa niswali katika rakaa.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliona Mtume rehema na amani ziwe juu yake usingizini kuwa yuko Peponi, akasema kumwambia Bilal bin Rabaha: Nieleze kuhusu amali yoyote ya sunna yenye matarajio makubwa uliowahi kuifanya ndani ya Uislamu? kwani mimi nilisikia sauti ya chini ya viatu vyako wakati wa kuvitikisa kwa kutembea mbele yangu Peponi. Bilal akasema: Sikuwahi kufanya amali yoyote yenye matarajio makubwa yoyote kwangu zaidi yakuwa sijawahi kutengukwa udhu wakati wowote iwe usiku au mchana isipokuwa ninatawadha, kisha ninaswali kwa ajili ya Mola wangu kwa udhu huo swala za sunna zisizo na mpaka kiasi nilichoandikiwa kuswali.
Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake: Nikikuhadithieni kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi kuporomoka kutoka mbinguni ni bora zaidi kwangu kuliko kumsemea uongo, na nikikuhadithieni katika yale yaliko baina yangu na nyinyi basi tambueni kuwa vita ni ulaghai (uongo), nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Watatokea katika zama za mwisho watu wenye umri mdogo (vijana), wenye mawazo ya kipumbavu, watazungumza maneno mazuri kuliko maneno ya viumbe wote, (lakini) wanatoka katika Uislamu kama unavyotoka mshale katika upinde, imani yao haitovuka koromeo zao, mahali popote mtakapokutana nao basi wauweni, kwani kuwaua kwao kuna malipo siku ya Kiyama kwa atakayewaua".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba, mtakaponisikia ninakuhadithieni kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi hakika mimi sifichi wala sibuni, wala sifuniki haki, bali ninaweka wazi, na kuanguka kwangu kutoka juu mbinguni ni rahisi na ni bora sana kwangu kuliko kusimulia jambo la uongo nikasema kuwa limetoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na nikisimulia mambo yalio kati yangu mimi na watu wengine, basi vita ni udanganyifu, hapo ninaweza kusema kwa mafumbo au kubuni au kuficha, kwani nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Watatokea katika zama za mwisho vijana wenye umri mdogo, wasiojitambua (madhaifu wa akili) watakuwa wakisema maneno kutoka ndani ya Qur'ani na wakiisoma kwa wingi, watakuwa wakitoka ndani ya Uislamu na wakivuka mipaka yake, kama mshale utokavyo katika upinde, Imani yao haivuki koromeo zao, mahali popote mtakapokutana nao basi wauweni, kwani kuwaua kwao kuna malipo kwa atakayewauwa, siku ya Kiyama.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na anachukia kwenu mambo matatu, basi anaridhia kwenu: Mumuabudu yeye, na wala msimshirikishe na chochote, na mshikamane katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msifarakane, na anachukia kwenu mambo matatu: Umbeya, na kuuliza uliza sana, na kupoteza mali".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu anapenda kwa waja wake mambo matatu, na anachukia kutoka kwao mambo matatu, anapenda kutoka kwao: Wampwekeshe yeye pekee na wala wasimshirikishe na chochote, na washikamane na ahadi ya Mwenyezi Mungu na Qur'ani na mafundisho ya Nabii wake wote, na wala wasifarakane katika umoja wa Waislamu. Na anachukia kwao: Upuuzi na maneno yasiyokuwa na faida katika yale yasiyowahusu, na kuuliza jambo ambalo bado halijatokea, au kuwaomba watu mali zao, na vile wanavyovimiliki, na yale yasiyokuwa na ulazima wa kuyaomba, na kupoteza mali na kuzitumia katika njia zisizokuwa za kisheria, na kuziweka katika uharibifu.
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary-Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yeyote atakaetubebea silaha dhidi yetu, si miongoni mwetu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnamtahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yeyote atakayebeba silaha dhidi ya waislamu, kwa ajili ya kuwatisha au kuwapora, atakayefanya hivyo pasina haki, atakuwa ametenda kosa kubwa na dhambi miongoni mwa madhambi makubwa, na atakuwa kastahiki kemeo hili kali.
Kutoka kwa Omari -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba siku moja alikuja katika jiwe jeusi akalibusu, kisha akasema: Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama nisingemuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikuja kiongozi wa waumini Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake katika jiwe jeusi katika kona ya Kaaba akalibusu, kisha akasema: Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama mimi nisingelimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu.