





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Asmaa Bint Abii Bakari-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote na baba yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Kwa hakika mimi nitakuwa kwenye Birika langu namtazama kila mwenye kuja kwangu kunywa, na kuna watu watafukuzwa, na nitasema: Ewe Mola wangu huyu anatokana na mimi na ni katika umma wangu, basi ataambiwa: Hivi unajua waliyoyafanya baada yako? Namuapia Mwenyezi Mungu, hawakuacha kurudi nyuma na kutoka katika dini yao."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa siku ya Kiyama yeye atakuwa kwenye Birika lake ili amuone kila mwenye kuja kwenye Birika katika watu wa umma wake. Na watachukuliwa watu wakiwa karibu na Mtume -Amani iwe juu yake- basi atasema: Ewe Mola wangu hao ni wangu na nikatika umma wangu, Basi kutasemwa: Je unajua walichofanya baada ya wewe kuachana nao? Namuapia Mwenyezi Mungu hawakuwacha kurudi nyuma na kutoka katika dini yao, hivyo basi hao siyo watu wako wala si katika umma wako.
Imepokelewa kutoka kwa Abii Dharri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hicho chombo cha Birika kiko vipi? Akasema: "Namuapa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, kwa hakika vyombo vyake ni vingi kama wingi wa nyota mbinguni na sayari zake eleweni vyema kuwa kung'aa kwake kutakuwa katika usiku usio na mwezi, pako safi, vyombo vya peponi atakaye kunywa katika vyombo hivyo hatopatwa na kiu milele wala kiu hakitomrudia, na maji hayo yanaruka na kububujika kupitia mabomba mawili yaliyo juu ya peponi, yeyote atakaye kunywa katika Birika hilo hatopatwa na kiu, upana wake ni sawa na urefu wake ambao ni sawa kutoka Amman mpaka Aila (Ni katika miji ya Jordan, baina yake ni km 330) maji yake ni meupe mno kuliko maziwa, na ni matamu kuliko asali."
Imepokelewa Imamu MuslimAme apa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ya kuwa vyombo vya Birika lake siku ya kiyama, ni vingi kuliko nyota angani, na kuliko sayari za mbinguni, Na hilo litadhihiri katika usiku wenye kiza ambao hauna mwezi, kwa sababu usiku wenye kuangaza huwa hakuna ndani yake nyota zenye kuonekana kwa kujificha kwake kutokana na mwanga wa mwezi, ambao hauna mawingu, kwa sababu kuwepo kwa mawingu kunazuia kuonekana kwa nyota, Na kwa hakika vyombo vya peponi atakaye kunywa miongoni mwa vinywaji vilivyomo humo, inakuwa ndiyo mwisho kabisa kwa mnywaji kupata kinywaji kwa sababu ya kiu, Na Birika lake linachuruzisha kupitia mabomba mawili yatokayo peponi, na upana wake ni sawa na urefu wake; Hivyo Birika nguzo zake zote zipo sawa, urefu wake ni sawa na umbali ambao upo kati ya Amman mji ambao upo Sham mpaka Aila nao ni mji maarufu uliopo pembeni mwa mji wa Sham, Na maji ya Birika ni meupe sana kuliko maziwa, na ladha yake ni tamu zaidi kuliko Asali.
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam" Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ikiwa ni hivyo basi moto wa Duniani unatosha kuadhibu, akasema: "Umeongezewa ukali zaidi yake kwa mara sitini na tisa, na mara zote hizo sitini na tisa kila mara moja ni sawa na ukali wa moto wa duniani."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Moto wa Duniani ni sehemu moja tu kutoka katika Moto wa Jahannam, Hivyo basi moto wa Akhera ukali wake unazidi Moto wa Duniani mara sitini na tisa, kila sehemu moja ya moto huo upo sawa na ukali wa moto wa Duniani. Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa hakika Moto wa Duniani ulikuwa unatosha kuwaadhibu waliokuwamo humo, Akasema: Moto wa Jahannam umeuzidi moto wa Duniani kwa zaidi ya mara sitini na tisa, na mara zake zote hizo sitini na tisa ni sawa na mara moja kutokana na ukali wake.
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ametuhadithia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- naye ni mkweli mwenye kukubaliwa: "Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake kwenye tumbo la mama yake mchana arobaini na nyusiku arobaini kisha anakuwa tone la manii kwa muda kama huo kisha anakuwa pande la damu kwa mfano wa siku hizo, kisha hutumwa Malaika na huamrishwa kufanya mambo manne; Hivyo basi ataandika riziki yake, na muda wa kufa kwake na matendo yake na ataandika kuwa ni muovu au ni mwema, kisha atampulizia roho, na kwa hakika mmoja wenu anaweza kufanya matendo ya watu wa Peponi kiasi ya kuwa haitobakia kati yake na kuingia Peponi isipokuwa usawa wa urefu wa mkono, basi kikamtangulia kitabu -Kadari- na akafanya matendo ya watu wa motoni na akaingia motoni, na kwa hakika mmoja wenu anaweza akafanya matendo miongoni mwa matendo ya watu wa motoni mpaka ikabakia kati yake na kuingia motoni kiasi cha usawa wa mkono kisha kikamtangulia kitabu -Kadari- akafanya mataendo ya watu wa peponi na akaingia peponi."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmesema Bin Masoud: Ametuhadithia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake naye ni mkweli kwenye maneno yake, na mwenye kukubaliwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemkubali, Amesema: Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake, na jambo hilo ni kuwa mtu akimuingilia mke wake basi yale manii yake yaliyosambaa hukusanywa kwenye tumbo la mwanamke kwa muda wa siku arobaini yakiwa ni tone la manii, Kisha hubadilika na kuwa pande la damu nzito iliyoganda, haya hufanyika katika arobaini ya pili, Kisha hubadilika kuwa pande la nyama, nacho ni kipande cha nyama chenye ukubwa wa kuweza kutafunwa, na mabadiliko haya ni katika arobaini ya tatu, Kisha Mwenyezi Mungu hulitumia pande hilo la nyama Malaika, kisha hulipulizia ndani yake roho baada ya kuisha siku arobaini za tatu, Na huamrishwa Malaika aandike maneno manne, nayo ni: Riziki yake, nacho ni kiwango ambacho atakipata miongoni mwake ni neema katika umri wake, Na pia huandikwa wakati wake, nao ni muda wa kubakia kwake Duniani, Na matendo yake, yatakuwa ni yapi? Na je atakuwa muovu au mwema. Kisha akaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yawezekana mtu akafanya matendo miongoni mwa matendo ya watu wa peponi, na yakawa matendo yake ni mazuri, yaani kwenye muonekano wa watu, na akabakia hivyo mpaka inakuwa kati yake na Pepo ni kiasi cha mkono, yaani kiasi kilichobaki kati yake mpaka kuifikia pepo ni kidogo sana kama vile ambavyo mtu amebakiza nafasi kati yake na ardhi kiasi cha mkono, mara Kitabu kinamtangulia na kile alichopangiwa, na wakati huo anafanya matendo ya watu wa motoni na akaandikiwa kuwa huo ndio mwisho wake na akaingia motoni; Kwa sababu sharti la kukubaliwa matendo yake ni kudumu katika matendo hayo na wala asibadilishe, na watu wengine wapo wenye kufanya matendo ya watu wa motoni mpaka mtu anakaribia kuingia motoni, mpaka inakuwa kati yake na kuingia motoni ni kiasi cha urefu wa mkono, basi kikamtangulia kitabu na alichopangiwa hivyo akafanya matendo ya watu wa peponi na akaingia peponi.
Imepokelewa kutoka kwa Twaausi kuwa yeye amesema: Niliwakuta watu miongoni mwa maswahaba wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- wakisema kuwa kila kitu huwa kwa namna ilivyopangwa, akasema: Na nimemsikia Abdullah bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake- anasema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kila jambo linakuwa kwa namna lilivyopangwa, mpaka kushindwa kufanya jambo fulani au kulifanya kwa ufanisi, au kufanya kwa ufanisi au kushindwa kabisa kufanya."
Imepokelewa Imamu MuslimAmeweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila jambo linakuwa kwa mujibu wa lilivyopangwa; Mpaka kushindwa: Nako nikuacha jambo ambalo ni wajibu kulifanya au kulichelewesha katika mambo ya kidunia au ya Akhera. Na hata kufanya jambo kwa ufanisi: Nako ni kufanya kwa uchangamfu na weledi katika mambo ya kidunia au ya Akhera. Na hakika Mwenyezi Mungu amepangilia jambo la kushindwa au kufanya kwa ufanisi na amepangilia kila kitu, hakuna chochote kinachotokea isipokuwa kinatokea kwa ujuzi wake Mwenyezi Mungu na kutaka kwake.
Imepokelewa kutoka kwa Matwar Bin Ukaamis -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Mwenyezi Mungu akimpangia mja afie sehemu fulani humfanya ahitajie kitu sehemu ile."
Imepokelewa Imamu TirmidhiyAnaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kuwa Mwenyezi Mungu akimpangia mtu kuwa afie katika ardhi fulani na hali yakuwa yeye hayupo katika ardhi hiyo; Basi humfanya ahitajie kitu katika ardhi ile hivyo ataenda katika ardhi ile, basi huchukuliwa roho yake akiwa huko.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Wakati mmoja tulipokuwa tumekaa Msikitini pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliingia mtu mmoja akiwa juu ya Ngamia, akampigisha magoti Ngamia ndani ya Msikiti kisha akamfunga, kisha akawaambia Maswahaba: Kati yenu Muhammad ni nani? Na wakati huo Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake- akiwa kati yao amekaa kwa kuegemea, tukasema ni huyu mtu mweupe aliyeegemea, yule mtu akamwambia: Ewe mtoto wa Abdul Muttwalib, basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: "Nimekuitikia" Yule bwana akamwambia Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- Hakika mimi nitakuuliza nanitatia mkazo katika kuuliza, hivyo usinichukie kwenye moyo wako, na wala usiona tabu kunijibu, akasema: "Uliza unachotaka" Akasema: Nanakuuliza kwa jina la Mola wako na Mola wa waliokuwa kabla yako, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekutuma kwa watu wote? Akasema: "Ndiyo, ni kweli" Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu ametuamrisha sisi tusali sala tano usiku na mchana? Akasema:"Ndiyo, ni kweli" Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa sisi tufunge Mwezi huu kila Mwaka? Akasema: "Ndiyo, ni kweli" Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa uchukue hizi sadaka kutoka kwa matajiri na uzigawanye kwa mafukara wetu? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ndiyo, ni kweli" Basi yule bwana akasema: Nimeamini yote yale uliyokuja nayo, na mimi ni mjumbe kuna wanaonifuata nyuma yangu, na mimi ndiye ninaitwa Dhwamam Bin Thaalaba ndugu wa Banii Saad Bin Bakri."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnatoa habari Anas Bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Wakati mmoja Maswahaba walikuwa wamekaa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Msikitini aliingia mtu mmoja akiwa juu ya Ngamia, basi akampigisha magoti kisha akamfunga Ngamia wake, Kisha akawauliza: Kati yenu Muhammad ni nani? Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa amekaa kati ya watu na ameegemea, tukamwambia: Ni mtu huyu mweupe aliyeegemea, Yule bwana akamwambia: Ewe mtoto wa Abdul Muttwalib, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nimekusikia, basi uliza nitakujibu. Yule bwana akamwambia Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake-: Mimi nitakuuliza na nitakuuliza kwa msisitizo mkubwa hivyo usinichukie wala usione dhiki katika nafsi yako. Yaani: Usinikasirikie wala usione dhiki, Akasema: Uliza unachotaka, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mola wako na Mola wa waliokuwa kabla yako, Je ni kweli Mwenyezi Mungu amekutuma kwa watu wote? Akasema: Ndiyo ni kweli, hali ya kutilia mkazo ukweli wake, Yule bwana akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha yakuwa sisi tusali sala tano usiku na mchana? Nazo ni sala za faradhi, Akasema: Ndiyo ni kweli, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha yakuwa sisi tuufunge Mwezi huu katika kila Mwaka? Yaani Mwezi wa Ramadhan, Akasema: Ndiyo ni kweli, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa uchukue hizi sadaka kutoka kwa matajiri wetu kisha uzigawe kwa mafukara wetu? Na sadaka hiyo ni Zaka, Basi akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-Ndiyo ni kweli, Basi Dhwamamu akasilimu, na akamwambia Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atawalingania watu wake kuingia kwenye uislamu, kisha akajitambulisha kuwa yeye ni Dhwammam Bin Thaalabah atokanae na kabila la Banii Saad Bin Bakri.
Imepokelewa kutoka kwa Ziyaad Bin Labiid -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitaja jambo fulani, akasema: "Jambo lenye kuogopesha litakuwa wakati itakapo ondoka elimu" Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni vipi inaondoka elimu, na hali yakuwa sisi tunaisoma Qur'ani na tunawasomesha watoto wetu na watoto wetu wanawasomesha watoto wao mpaka siku ya Kiyama? Akasema: "Akukose mama yako ewe Ziadi ikiwa nitakuzingatia wewe ni miongoni mwa wajuzi katika mji wa Madina, hivi hawa siyo Mayahudi na Manaswara wanaisoma Taurati na Injili, na hawafanyii kazi chochote katika yale yaliyomo?!"
Imepokelewa na Ibnu MaajahAlikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amekaa kati ya Maswahaba zake, akasema: Huu ndiyo wakati ambao itaondolewa na kupokonywa elimu kutoka kwa watu, Hivyo akashangaa Ziyaad Bin Labiid Al-Answaariy-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Akasema: Ni vipi itaondolewa elimu na kutupotea sisi?! Na hali yakuwa tumeisoma Qur'ani na tukaihifadhi; Namuapia Mwenyezi Mungu kuwa tutaisoma, na kuwasomesha wake zetu na watoto wetu, na wajukuu wetu, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa anaona ajabu: Amekukosa mama yako ewe Ziyaad! kama ikiwa nitakuzingatia wewe ni katika wajuzi wa mji wa Madina! Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akaweka wazi kuwa kuiokosa elimu siyo kuikosa Qur'ani, bali kukosa elimu ni kuacha kuifanyia kazi, Kwa mfano hii hapa Taurati na Injili ipo kwa Mayahudi na Manaswara; na pamoja na hivyo haiwanufaishi, wala hawapati faida kutokana na makusudio yake; na faida yenyewe ni kufanyia kazi walicho jifunza.
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yao- amesema: Uliteremshwa Wahyi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka arobaini, akakaa Makkah miaka kumi na tatu, kisha akaamrishwa kuhama, hivyo akahama kwenda Madina, akakaa Madina miaka kumi, kisha akafariki Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: kuwa Wahyi uliteremshwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na akatumwa akiwa na umri wa miaka arobaini, basi akakaa Makkah miaka kumi na tatu baada ya kuteremshiwa wahyi, kisha akaamrishwa kuhama kwenda Madina na akakaa huko miaka kumi, kisha akafariki -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka sitini na tatu.