





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Qatadah -Mwenyezi Mungu amrehemu amesema: Alitusimulia Anas Bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtu mmoja alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu vipi kafiri atafufuliwa akitembea kwa uso wake? Akasema: "Hivi yule aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?" Akasema Qatadah: Kwa nini asiweze, ninaapa kwa utukufu wa Mola wetu anaweza kufanya hivyo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- vipi atafufuliwa Kafiri akitembea kwa uso wake siku ya Kiyama? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: Hivi Mwenyezi Mungu aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hapa Duniani hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?! Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimwambia baba yake mdogo: "Sema: Laa ilaaha illa llahu, nitakutolea ushuhuda wa kusilimu kwa maneno hayo siku ya Kiyama" Akasema: Ningetamka kama si kuogopea matusi ya Makuraishi wanasema kulichompelekea kusema maneno hayo ni kuogopa kifo, kama si hivyo ningeingiza furaha moyoni mwako, basi Mwenyezi Mungu akateremsha: "Hakika wewe huwezi kumuongoza umtakaye lakini Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye" (suratul Qaswas: 56)
Imepokelewa Imamu MuslimMtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimtaka Abuu Twalib ambaye ni baba yake mdogo akiwa katika kilevi cha mauti, atamke neno Laa ilaaha illa llahu, ili amuombee utetezi kwa neno hilo siku ya Kiyama, na amtolee ushuhuda wa kusilimu kwake, akakataa kutamka shahada kwa kuogopea kuwa Makuraishi watamtukana na watamsema kuwa: Amesilimu kwa sababu ya kuogopa mauti na unyonge! Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kama si huko kuogopa ningeingiza furaha katika moyo wako kwa kutamka kwako shahada na mauti yangekufika kwa namna ambayo ungeiridhia! basi akateremsha Mwenyei Mungu Aya ambayo inajulisha kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hamiliki uongofu wa kuukubali uislamu, bali Mwenyezi Mungu aliyetukuka peke yake humuwezesha amtakaye. Na kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake anawaongoza viumbe kwa ufahamu na kuwawekea wazi na kuwaongoza pamoja na kuwaita kwenye njia iliyonyooka.
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- siku moja alimkosa Thabiti bin Kaisi, mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi naweza kukupa taarifa zake, akamfuata akamkuta akiwa amekaa nyumbani kwake, akiwa ameinamisha kichwa chake, akasema: Ni jambo gani limekusibu? Akasema: Ni shari, alikuwa akinyanyua sauti yake juu ya sauti ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, tayari yameporomoka matendo yake, naye ni katika watu wa motoni, akarudi yule bwana kwa Mtume akamweleza kuwa kasema kadhaa wa kadhaa, mara ya pili akarudi kwake akiwa habari njema, akasema: "Nenda kwamwambie: Wewe si miongoni mwa watu wa motoni, bali ni katika watu wa peponi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlimkosa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Thabiti bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake, akamuulizia, mtu mmoja akasema: Mimi naweza kukupatia habari zake, na sababu ya kukosekana kwake, akamwendea akamkuta akiwa na huzuni na kainamisha kichwa chake nyumbani kwake, akamuuliza: Umepatwa na nini? Thabiti akamueleza shari aliyonayo; kwa sababu yeye alikuwa akinyanyua sauti yake juu ya sauti ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na Mwenyezi Mungu kamuonya mwenye kufanya hivyo kwa kubatilika matendo yake, na kwamba yeye ni katika watu wa motoni. Yule bwana akarejea kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na akamueleza hilo, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamuamrisha arudi kwa Thabiti na ampe habari njema, yakuwa yeye si miongoni mwa watu wa motoni bali ni katika watu wa peponi, na hii ni kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye sauti ya juu kimaumbile, nakuwa yeye ndiye alikuwa mzungumzaji wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na ni mzungumzaji wa Answari (Watu wa Madina).
kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Yakwamba amemsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake anasema: "Mtakapo msikia muadhini basi semeni mfano wa yale anayo yasema, kisha mnitakie rehema, ni kwamba yule atakaye nitakia rehema mara moja Allah atamtakia rehema mara kumi, kisha niombeeni kwa Allah ukaribu, hakika ukaribu huo ni daraja ndani ya Pepo, halipati daraja hilo isipokuwa mja miongoni mwa waja wa Allah, na ninatarajia niwe mimi ndiye huyo mja huyo, na atakayeniombea mimi ukaribu ataupata uombezi".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mwenye kumsikia muadhini kwa ajili ya swala basi naye amfuatilize nyuma yake, aseme mfano wa kauli zake, isipokuwa haiala mbili (Hayya alas-swalaa, na hayya alal falaah), atasema baada yake: Laa haulaa walaa quwwata illa billaah, kisha atamtakia rehema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kumalizika kwa adhana, kwani atakayemtakiwa rehema mara moja, basi Mwenyezi Mungu atamtakia rehema kumi kwa sababu ya dua hiyo moja, na maana ya Mwenyezi Mungu kumtakia rehema mja wake: Ni kumsifu mja wake mbele ya Malaika. Kisha akaamrisha kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ukaribu -Rehema na amani ziwe juu yake-, nayo ni nafasi iliyoko peponi, na ni daraja ya juu zaidi kuliko zote, haimstahiki na wala haiwezekani nafasi hiyo ila kwa mja mmoja katika waja wote wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ninataraji mimi kuwa ndiye mja huyo, na alisema hivyo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa sababu ya kujinyenyekeza; kwa sababu nafasi hiyo ikiwa haistahiki ila kwa mtu mmoja, hawezi kuwa mmoja huyo zaidi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-; kwa sababu yeye ndiye mbora wa viume wote. Kisha akabainsha -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayemuombea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nafasi ya ukaribu basi ataupata utetezi wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Kutoka kwa Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika shetani amekaa kati yangu na swala yangu na kisomo changu ananichanganya, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu", anasema: Nikafanya hivyo Mwenyezi Mungu akamuondosha kwangu.
Imepokelewa Imamu MuslimAlikuja Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake- kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika Shetani ameziba kati yangu na swala yangu, na amenizuilia na kupata utulivu ndani yake, na amenichanganyia kisomo changu na amenitia wasi wasi ndani yake, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Huyo ni Shetani aitwaye Khinzab, ukihisi hali hii basi taka kinga kwa Allah, na utake ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme mate kushotoni kwako mara tatu, Othman anasema: Nikafanya aliyoniamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mwenyezi Mungu akaniondolea hali hiyo.
Kutoka kwa Abbasi bin Abdil Muttwalib radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Amekwisha ionja ladha ya imani, yule mwenye kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola wake, na Uislamu ndiyo dini, na Muhammad ni Mtume"
Imepokelewa Imamu MuslimAnaeleza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kuwa muumini mkweli katika imani yake uliyetulizana moyo wake kwa imani yake, atapata ukunjufu na wasaa na furaha ndani ya moyo wake na utam na ladha ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu endapo ataridhia kwa mambo haya matatu: La kwanza: Akiridhika kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wake Mlezi, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake kwa yale yanayomfikia kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa muktadha wa ulezi, ikiwemo kugawa riziki na hali za waja, asipate upinzani kwa kitu chochote ndani ya nafsi yake, na asitafute Mola Mlezi zaidi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. La pili: Aridhie kuwa Uislamu ndio Dini ya kweli, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake kwa yale yanayofungamana na Uislamu kama sheria na wajibu, na asipite njia nyingine isiyokuwa Uislamu. La tatu: Aridhie kuwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake ni Mtume, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake na afurahie yote aliyokuja nayo pasina kusitasita wala kutia shaka, na asipite ila njia inayokwenda sambamba na muongozo wake rehema na amani ziwe juu yake.
Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Amry -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mambo manne yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na itakayekuwa kwake sifa moja kati ya hizo, atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiingia makubaliano hufanya hiyana, na akiahidi anakwenda kinyume, na akigombana huvuka mipaka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeTabia nne amezitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zitakapokusanyika kwa muislamu atakuwa na mfanano mkubwa na wanafiki kwa sababu ya tabia hizi, na hili linakuwa kwa yule ambaye sifa hizi ndio tabia yake mara kwa mara, ama atakayezifanya mara chache huyu haingii katika sifa hizi, nazo ni: Ya kwanza: Akizungumza husema uongo kwa makusudi na kutokuwa mkweli katika maneno yake. Ya pili: Akitoa ahadi katika makubaliano haitimizi, na humfanyia hiyana aliyeahidiana naye. Ya tatu: Akiahidi ahadi yoyote haitimizi na huenda kinyume. Ya nne: Akizozana na akagombana na yeyote ugomvi wake huwa mkali sana, na hupotoka katika haki, na hufanya hila ya kuipinga na kuibatilisha, na husema maneno ya batili na uongo. Unafiki ni mtu kudhihirisha tofauti na yale anayoyaficha, na maana hii ipo kwa mtu mwenye sifa hizi, na unafiki wake unamuhusu yule anayezungumza naye, na akamuahidi, na akamwamini, na akagombana naye, na akamuahidi mtu, si kwamba atakuwa mnafiki katika Uislamu anaudhihirisha na kuficha ukafiri, hapana, na atakayekuwa na sifa moja katika sifa hizi; basi atakuwa na sifa ya unafiki ndani yake hadi atakapoiacha.
Kutoka kwa bin Abbasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, yeye na baba yake: Ya kwamba pindi aliposema kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Hivi je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa wanawake wa Peponi? Nikasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika mimi huanguka, na nguo zangu hufunuka ninapoanguka, nakuomba uniombee kwa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ukipenda unaweza kuvumulia na utapata malipo ya Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye" Akasema: Bali nitavumilia, akasema: Lakini mimi huwa nafunuka nguo, basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke, basi akamuombea.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlisema bin Abbasi Mwenyezi Mungu amuwie radhi kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa watu wa Peponi? Atwaa akasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke muethiopia mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: akasema: Hakika mimi nina maradhi, huanguka na kufunuka nguo zangu, na kuonekana sehemu ya mwili wangu pasina mimi kujielewa, basi muombe Mwenyezi Mungu aniponye, akasema: Ukipenda unaweza kuvumilia na utakuwa na malipo ya Pepo, na ukipenda nitamuomba Mwenyezi Mungu akuponye, akasema: Basi nitavumilia, kisha akasema: Basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke nikianguka, basi akamuombea kwa Mwenyezi Mungu.
Kutoka kwa Ummu Dardaai na Abuu Dardaai radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Dua ya mtu muislamu kwa ndugu yake, anapokuwa hayupo, hujibiwa, kichwani kwake huwa kuna Malaika aliyepewa kazi, kila anapomuombea ndugu yake kwa heri, Malaika aliyepewa kazi hiyo husema: Ewe Mwenyezi Mungu pokea dua, na kwako pia upate mfano wake".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa dua ya muislamu kwa ndugu yake muislamu, anapokuwa hayupo anayeombewa dua, hujibiwa; kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha utakasifu (Ikhlaswi) na kwamba kichwani kwa muombaji huwa kuna Malaika aliwakilishwa, kila anapomuombea ndugu yake kwa heri, basi anasema Malaika alipewa kazi hiyo: Mwenyezi Mungu apokee dua, na upate pia mfano wa hayo uliyoomba.