





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Mwenyezi Mungu: Kila amali ya mwanadamu hiyo ni ya kwake isipokuwa swaumu, bila shaka hiyo ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa, na swaumu ni kinga, na itakapokuwa ni siku ya kufunga mmoja wenu basi asitamke machafu, wala asifanye fujo, na ikiwa kuna mtu atamtukana au akampiga, basi aseme, mimi nimefunga, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hakika harufu ya mdomo wa mfungaji ni nzuri mno mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko harufu ya Miski, mfungaji anafuraha mbili anazofurahia: Anapofuturu hufurahi, na akikutana na Mola wake atafurahi kwa swaumu yake"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika hadithil Kudsi kuwa: Amali zote za mwanadam mema huzidishwa jema moja kwa mara kumi mfano wake mpaka ziada mia saba, isipokuwa swaumu; kwani hiyo ni yangu kiasi kwamba huwa haifikiwi na ria, na mimi ndiye ninayeilipa, hivyo ninabaki peke yangu katika kujua kiwango cha thawabu zake na uzidishwaji wa mema yake. Kisha akasema: "Na swaumu ni kinga" Ni kinga na ni ngome madhubuti dhidi ya moto; kwa sababu ni kujizuia na matamanio na kutumbukia katika madhambi, na moto umezingirwa na matamanio. "Itakapokuwa ni siku ya kufunga kwa mmoja wenu basi asifanye machafu" kwa tendo la ndoa na vitangulizi vyake, wala kwa maneno machafu moja kwa moja. "Wala asifanye fujo" Kwa ugomvi na zogo. "Na ikiwa mtu atamtukana au kumpiga" Katika mwezi wa Ramadhani basi na aseme: Mimi ni mtu niliyefunga; huenda akamuacha, ikiwa ataendelea na kukawa hakuna namna zaidi ya kupigana naye pasina utani basi na amsukume kidogo kidogo kama anamtenza nguvu. Kisha akaapa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akamuapia yule ambaye nafsi yake iko mkononi mwake kuwa kubadilika kwa harufu ya kinywa cha mfungaji kwa sababu ya swaumu hiyo ni nzuri mno mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama kuliko harufu ya Misiki kwenu, na inamalipo mengi kuliko Miski iliyohimizwa katika swala za Ijumaa na vikao vya kumtaja Mwenyezi Mungu. Na mfungaji anafuraha mbili anazofurahia: Anapofungua anafurahia kufungua kwake kwa kuondoka njaa yake na kiu yake kwa kuhalalishiwa kufungua, na anafurahi kwa kutimia swaumu yake na kufikia kikomo kwa ibada yake, na wepesi kutoka kwa Mola wake Mlezi, na nimsaada kwa mustakabali wa swaumu yake. "Na akikutana na Mola wake Mlezi atafurahi kwa swaumu yake" Kwa malipo yake na thawabu zake.
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali swala zake za usiku, naye akiwa kajilaza mbele yake, inapobakia witiri, anamuamsha na anaswali witiri. Na katika riwaya yake: inapobakia witiri, anasema: "Simama na uswali witiri ewe Aisha".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimMaana ya hadithi: Nikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali swala za usiku, na Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akiwa kajilaza mbele yake, na katika riwaya ya Bukhariy na Muslim kutoka kwake: "Nikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali usiku na mimi nikiwa nimejilaza kati yake na kibla, kama linavyolazwa jeneza". Anapomaliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swala ya usiku (tahajjudi), na kabla hajaanza swala ya witiri anamuamsha kwaajili ya witiri, na katika riwaya ya Muslim: Inapobakia witiri, anasema: "Simama na uswali witiri ewe Aisha". Na katika riwaya ya Abiidaudi: "Mpaka anapotaka kuswali witiri basi anamuamsha na anaswali witiri". Na maana yake: Nikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akimuacha Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- mwanzo wa usiku wala hamuamshi, mpaka anapomaliza swala zake na ikawa haijabakia isipokuwa witiri anamuamsha ili naye apate witiri yake, na afanye haraka kuswali witiri baada ya kuamka ili uvivu wa usingizi usimzidie, lau kama akimzembea ikampita.
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja nyakati za usiku nilimkosa kitandani Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikaanza kumtafuta ukaangukia mkono wangu ndani ya nyayo zake zikiwa zimesimamishwa akiwa ndani ya msikiti, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu ninajilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na salama yako dhidi ya adhabu zako, na ninajilinda kwako kutokana nawe, siwezi kuzidhibiti sifa zako kwa idadi maalum kama ambavyo wewe ulivyoisifu nafsi yako"
Imepokelewa Imamu MuslimAnasema Aisha radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nimelala pembezoni mwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikamkosa wakati wa usiku, nikagusa kwa mkono wangu sehemu aliyokuwa akiswalia ndani ya chumba; ghafla nikamuona amesujudu na miguu yake ikiwa imesimamishwa, mara nikamsikia akisema: "Ninajilinda" Na ninapitia "Katika radhi zako dhidi ya hasira zako" juu yangu au juu ya umma wangu, "na" ninaomba kinga "kwa salama yako" na msamaha wako mwingi "kutokana na adhabu zako", "na ninajilinda kwako kutokana nawe" na kwa sifa za uzuri wako kutokana na sifa za utukufu wako, kiasi kwamba hakuna awezaye kukinga dhidi yako ila wewe, hakuna pa kusalimika wala pa kujilinda kutokana na Mwenyezi Mungu ila kwake, "Siwezi kuzihesabu sifa zako" Sina uwezo wala siwezi kufikia kuzidhibiti na kuzihesabu kwa idadi kwa kushindwa kwangu kuzidhibiti kwa wingi neema zako na ihisani yako kama unavyostahiki, hata kama nikijitahidi katika hilo, "Wewe kama ulivyoisifia nafsi yako" wewe ndiye uliyeisifu dhati yako sifa zinazokustahiki, ni nani awezaye kutimiza haki ya sifa zako?!
Na kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Aliulizwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: Ni swala ipi bora? Akasema: "Ni kurefusha kisimamo".
Imepokelewa na Imamu MuslimWalimuuliza maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- : Ni swala ipi bora? Na swali hili ni kwasababu ya pupa yao ya kuhakikisha wanapata kiwango kikubwa cha mema,Na makusudio yake:Ni aina ipi ya swala zote ndio bora? Au: Yaani ni tendo lipi katika matendo ya swala ndio bora? Ni kusimama au kurukuu au kusujudu? Akaeleza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake kuwa ni kurefusha kisimamo ndani yake.
Kutoka kwa Shuraihi bin Hanii amesema: Nilimuuliza Aisha, nikasema: Ni kwa jambo gani alikuwa akianza nalo Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia nyumbani kwake? Akasema: Kwa mswaki.
Imepokelewa Imamu MuslimIlikuwa katika muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuanza na mswaki anapoingia nyumbani kwake wakati wowote, usiku au mchana.
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja aliyelala usiku mpaka pakapambazuka, akasema: "Huyo ni mtu aliyekojolewa na Shetani ndani ya masikio yake, au alisema: ndani ya sikio lake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja aliyelala mpaka pakapambazuka na Jua likachomoza na wala hakunyanyuka kwenda katika swala ya faradhi, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Huyo ni mtu ambaye Shetani kakojoa ndani ya sikio lake.
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mambo kumi ni katika maumbile: Kupunguza masharubu, na kuziachia ndevu,na kupiga mswaki, na kupandisha maji puani, na kupunguza kucha, na kuosha fundo za vidole, na kunyofoa nywele za makwapani, na kunyoa nywele za sehemu za siri, na kustanji kwa maji". Anasema mpokezi : na nimelisahau la kumi nahisi huenda ikawa ni kusukutua. Amesema Wakii -naye ni mmoja kati ya wapokezi wake na kupunguza maji: Yaani kustanji.
Imepokelewa na Imamu MuslimAnaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- jumla ya sunna za kimaumbile. Na "Maumbile" ni umbile ambalo Mwenyezi Mungu kawaumba viumbe juu yake, na akawafanya kuumbika (kulazimika) kulifanya, nakuwa hilo ni katika kheri na makusudio yake na ni umbile salama; kwasababu umbile lililopinda halizingatiwi; kwa kauli ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:"Kila mwenye kuzaliwa huzaliwa katika maumbile basi wazazi wake humfanya kuwa Yahudi au Mkristo au mmajusi". La kwanza: "kupunguza masharubu": kuyapunguza mpaka mdomo uonekane, kwa kile kinachopatikana ndani yake katika usafi, na kujilinda na vile vinavyotoka puani, kwani nywele za masharubu zinaposogea katika mdomo hugusa kile ambacho mdomo unakipata katika vyakula au vinywaji, na kuharibu muonekano pale zinapokithiri, hata kama atalipendezesha hilo asiyejali. Ni lazima muislamu achunge sharubu zake kwa kuzinyoa au kuzipunguza na asiziache zaidi ya siku arobaini; kwa yale aliyoyapokea Muslim kutoka kwa Anasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-tuliwekewa muda sisi katika masharubu, na kupunguza kucha, na kukwapua nywele za kwapani, na kunyoa sehemu za siri, kuwa tusiziache zaidi ya siku arobaini" "Na kuziachia ndevu" Na ndevu: ni zile zilizoota katika kidevu au sharafa (nywele za shavuni), Na makusudio ya kuziachia: kuziacha zikiwa zimejaa asiziguse kwa kuzinyoa wala kuzipunguza,si kidogo wala kingi; kwasababu neno kuziachia limetokana na wingi na kujaza,kama kauli yake Mtukufu: (Mpaka walipoachilia), na zimekuja hadithi nyingi toka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- zikiamrisha kuzifuga kwa matamshi mengi; kwani imekuja kwa tamko:"jazeni ndevu" na kwa tamko:"Shusheni ndevu", na kwa tamko "Achieni ndevu", na kama inavyoonyesha amri ya kuziacha na kuzijaza na kutozigusa, na kwa msingi huu hairuhusiwi kwa muislamu kunyoa ndevu zake, ikiwa atafanya hivyo atakuwa kaenda kinyume na njia ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na atakuwa kaasi amri yake na kaangukia katika kujifananisha na makafiri."na mswaki" Yaani: katika mambo ya kimaumbile ambayo sheria imeyahimiza, Nikuwa "(mswaki) ni Kisafisha kinywa na humridhisha Mola" na ndio maana ni sheria kila wakati lakini inatiwa mkazo zaidi wakati wa udhu na swala na wakati wa kuamka toka usingizini na kubadilika kwa harufu ya mdomo, na meno kuwa ya njano na mfano wake. "na kupandisha maji puani" Yaani: nikuwa kupandisha maji ni katika maumbile, na kuondoa vilivyoko puani katika uchafu ambao unaweza kumsababishia udhia na madhara. Na kupandisha maji puani kunakuwa wakati wa udhu na kunakuwa nje ya udhu,kama mtu akihitaji kusafisha pua na kupandisha maji kwa kusafisha pua yake, na hii inatofautiana kulingana na watu, kuna baadhi ya watu hawahitaji hili isipokuwa katika udhu, na kuna watu wanalihitaji hili kwa wingi. Na miongoni mwa hilo pia: Yaani miongoni mwa sunna za maumbile ni kusukutua, kwani hilo ni katika maumbile; mdomo na pua mara nyingi vinazungukwa na uchafu, hivyo ikawa ni sehemu katika maumbile kuvizingatia."Na kupunguza kucha" Yaani katika mambo ya kimaumbile: ni kupunguza kucha, na makusudio yake ni kucha za mikono na miguu, zisiachwe zaidi ya siku arobaini; kwa mujibu wa hadithi iliyotangulia."Na kuosha fundo za mikono" Yaani na kuosha maungio ya vidole juu na ndani; kwasababu ni miongoni mwa sehemu unapokusanyikia uchafu; kwa kukunjamana kwake, hivyo huenda maji yasifike, na vikitiliwa umuhimu wa kuvisugua, na vikapitishwe tena mkono mara ya pili, basi maji yatavifikia, ikawa katika maumbile ni kuvitilia umuhimu. Na viunganishwe pamoja na fundo za vidole kila sehemu katika mwili inayokusanya uchafu kwa jasho au kinginecho kama mikunjo ya sikio na ndani ya mapaja na sehemu zinginezo zilizozidi kujikunja."Na kukwapua nywele za kwapani" Yaani: Katika mambo ya kimaumbile ni kukwapua nywele za kwapani, nako ni kuzivuta na kuzing'oa, na hiyo ni kwasababu ni sehemu inayokithiri jasho, na unakusanyika hapo uchafu, na harufu hubadilika, na zisiachwe zaidi ya siku arobaini; kwa kile kilichotangulia katika hadithi ya Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, na bora zaidi ni kuzinyofoa ikiwa ataweza, na ikiwa kunyofoa ni vigumu, basi hakuna tatizo kama atazinyoa na akatumia mafuta ya kuziondoa; kwasababu lengo ni kuziondoa na kusafisha mahali hapo, na tayari limefanyika."Na kunyoa sehemu za siri" Yaani: Katika mambo ya kimaumbile ni kuondoa nywele za sehemu ya siri, nazo ni nywele zinazoota sehemu ya siri ya mbele, kwa mwanaume na mwanamke, hivyo ni katika maumbile kuziondoa, sawa sawa iwe ni kwa kuzinyoa au kuzinyofoa au kuzipunguza au kwa kutumia vyombo vya kisasa; kwasababu lengo ni kusafisha, na tayari lengo limetimia, na wala asiziache kwa muda wa siku arobaini kwa hadithi ya Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Na kupunguza maji" Yaani ni katika maumbile kupunguza maji, na imefasiriwa kwa maana ya: kustanji, na inapewa nguvu maana hii kwa riwaya ya Abuudaudi na bin Majah kutoka Ammar bin Yaasir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:"Ni katika maumbile: Kusukutua, na kupandisha maji puani. Na kusafisha", Na kusatanji: ni kuondoa kilichotoka katika moja ya njia mbili kwa kitu kilichosafi, kama maji na jiwe na vitambaa, na mfano wa hivyo katika vile ambavyo vinahusika na kusafisha."Amesema mpokezi: Na nimesahau jambo la kumi, huenda likawa ni kusukutua "Hii ni shaka toka kwa mpokezi. Na uhakika wake nikuwa mambo haya yote, yanakamilisha muonekano wa mwanadamu na yanamsafisha na yanamtwaharisha, na yanamuondolea mambo yenye kumdhuru na machafu.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anafunga katika kila fundo usiku kucha na husema : basi lala, pindi anapoamka na akamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu linafunguka fundo moja, akitawadha, linafunguka fundo jingine, na akiswali, yanafunguka mafundo yake yote, anaamka akiwa na uchangamfu na moyo mkunjufu, na vinginevyo basi anaamka akiwa na nafsi chafu tena mvivu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya shetani na mapambano yake na mwanadam anayetaka kusimama kwa ajili ya swala ya usiku au Alfajiri. Muumini anapokwenda kulala shetani hufunga katika kisogo chake -yaani mwisho wa kichwa chake- mafundo matatu. Muumini atakapoamka na akamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akawa hajatii wasi wasi wa shetani; fundo moja hufunguka. Akitawadha linafunguka fundo jingine. Na ikiwa atasimama akaswali yatafunguka mafundo yote matatu, na atakuwa na uchangamfu wa nafsi; na kufurahi kwake kwa yale aliyoafikishwa na Mwenyezi Mungu katika ibada, akijipa bishara kwa yale aliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu katika thawabu na msamaha, ikiwa ni pamoja na hivyo vilivyomuondokea katika mafundo ya shetani na vikwazo vyake, na asipofanya hivyo atakuwa na nafsi chafu, atakuwa na moyo wenye huzuni, mvivu katika mambo ya kheri na mambo mema; kwa sababu atakuwa kafungwa kwa pingu za shetani, na atakuwa kawekwa mbali na kumkaribia Rahmani (Mwingi wa rehema).
Kutoka kwa Ma'adan Bin Abi Twalha Alya'mary amesema: Nilikutana na Thauban muachwa huru wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikasema: 'Niambie matendo nitakayo yafanya (iwe sababu kwa Allah) kuniingiza Peponi' au alisema, nikasema: matendo mazuri yanayopendeka zaidi kwa Allah, akanyamaza, kisha nikamuuliza akanyamaza, kisha nikamuuliza kwa mara ya tatu akasema: Nilimuuliza hayo Mtume wa Allah rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Shikamana na kusujudu kwa wingi kwa ajili ya Allah, kwani hakika wewe huta sujudu kwa ajili ya Allah isipokuwa Allah atakupandisha kwa sijida hiyo daraja, na atakufutia kwa sijida hiyo makosa" Akasema Maadan: Kisha nikakutana na Abuudardaa nikamuuliza, akanambia mfano wa hayo alionambia Thauban.
Imepokelewa Imamu MuslimAliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu matendo yanayopelekea kuingia Peponi au kuhusu matendo yanayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu? Basi rehema na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia muulizaji: Dumu na sijida kwa wingi, kwani kila unapomsujudia Mwenyezi Mungu anakunyanyua daraja kwayo, na anakusamehe dhambi kwa sababu ya sijida hiyo.