





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Kutoka kwa Zirri bin Hubaishi amesema: Nilikwenda kwa Swafwan bin Assali Al-Muraadi, ili nimuulize kuhusu kufuta juu ya khofu mbili, akasema: Ni nini kimekuleta ewe Zirri? Nikasema: Kutafuta elimu, akasema: Hakika Malaika huweka mbawa zao kwa mwenye kutafuta elimu; kwa kuridhishwa na kile anachokitafuta, basi nikasema: Hakika mimi nimepata uzito ndani ya kifua changu kuhusu kufuta juu ya khofu mbili baada ya kukidhi haja ndogo na kubwa, na wewe ulikuwa miongoni mwa wanafunzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hivyo nimekuja kukuuliza: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu hilo? Akasema: Ndiyo, Alikuwa kituamrisha tunapokuwa safarini tusivue khofu zetu kwa siku tatu (mchana na usiku) isipokuwa kwa ajili ya janaba, lakini ni kwa haja kubwa na ndogo na usingizi, nikasema: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu matamanio? Akasema: Ndiyo, tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, wakati tukiendelea kuwa naye ghafla, Bedui mmoja alimuita kwa sauti kubwa na ya juu. Ewe Muhammadi!!!, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kwa mfano wa sauti yake: "Ehee, niambie!" Tukasema kumwambia koma!, punguza sauti yako, kwani hapa uko mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na umekatazwa kufanya hivi, akasema: Wallahi siwezi kupunguza, kisha Bedui akasema: Utakuta mtu anawapenda watu fulani lakini hajawahi kukutana nao, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mtu atakuwa pamoja na yule anayempenda siku ya Kiyama" Basi akaendelea kutusimulia mpaka akautaja mlango ulioko Magharibi mwendo wa upana wake, au anaweza kutembea aliyepanda kwenye upana wake kwa miaka arobaini au sabini.
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadAlikuja Zirri bin Hubaishi kwa Swafwan bin Assali radhi za Allah ziwe juu yake, ili amuulize kuhusu khofu mbili, Swafwan akasema: Ni nini kimekuleta ewe Zirri? Akasema: Kutafuta elimu, akasema: Hakika Malaika huweka mbawa zao kwa mwenye kutafuta elimu; kwa kuridhishwa na kutukuza kile anachokifanya mwenye kutafuta elimu, Zirii akasema: Hakika nimepata shaka ndani ya nafsi yangu kuhusu kufuta juu ya khofu mbili baada ya haja kubwa na ndogo, na wewe ni katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na nimekuja hapa kukuuliza, je, uliwahi kumsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitaja chochote kuhusu hili?. Akasema Swafwan: Ndiyo, alikuwa akituamrisha tunapokuwa wasafiri tusivue khofu zetu kwa siku tatu (mchana na usiku) kwa sababu ya hadathi (uchafu) mdogo, kama haja kubwa na ndogo na usingizi, isipokuwa janaba hapo basi ni wajibu kuvua, nikasema: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu mapenzi? Akasema: Ndiyo: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, wakati tukiwa bado tuko pamoja naye mara ghafla Bedui mmoja aliita kwa sauti ya juu sana: Ewe Muhammadi!, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kwa sauti ya juu karibu na sauti yake: Njoo, nasi tukasema kumwambia: Koma! Shusha sauti yako, kwani hapa uko mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na umekatazwa kunyanyua sauti mbele yake. Akasema kwa sababu ya ukaidi wake: Wallahi siwezi kuishusha, Bedui akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, utakuta mtu anawapenda watu wema na hajafanya matendo mfano wa matendo yao? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Mtu atakuwa pamoja na anayempenda siku ya Kiyama, Anasema Zirri: Swafwan akaendelea kutuhadithia mpaka akataja mlango wa toba ulioko upande wa Sham aliuumba Mwenyezi Mungu siku aliyoumba Mbingu na Ardhi, anaweza kutembea aliyepanda juu ya kipando kwenye upana wake miaka arobaini au sabini, na wala haufungwi mpaka Jua lichomoze kutokea Magharibi yake.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ewe Abuu Dhari utakapopika mchuzi basi zidisha maji yake, na umkumbuke jirani yako".
Imepokelewa Imamu MuslimAlimhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Abuu Dhari Al-Ghifaari radhi za Allah ziwe juu yake atakapopika mchuzi basi azidishe maji yake na mchuzi wake, na amkumbuke na amtafute jirani yake.
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudri -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba Jibril alimjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Muhammad umetekesa kwa maumivu? Akasema: "Ndiyo" Akasema: "Bismillaahi Arqiika, Min kulli shai-in Yu-udhiika, min sharri kulli nafsin Au Aini Haasidin, Allaahu yash-fiika, bismillaahi Arqiika" Yaani: Kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakuombea, kutokana na kila kitu kinachokuudhi, na kutokana na shari ya kila nafsi au jicho la hasidi, Mwenyezi Mungu atakuponya, kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakusomea.
Imepokelewa Imamu MuslimAlikuja Malaika Jibril amani iwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamuuliza: Ewe Muhammad, unalalamika kwa maradhi? Akasema: Ndiyo. Jibril akamsomea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwa kusema: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu" Kwa kutaka msaada kwa jina hilo "Ninakusomea" na ninakukinga, "kutokana na kila kitu kinachokuudhi" Kiwe kikubwa au kidogo, "kutokana na shari ya kila nafsi" chafu, "au jicho la hasidi" lisije kukufika, basi Mwenyezi Mungu "atakuponya" na akukinge na akuhifahdi dhidi ya kila maradhi, "kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakuombea" amelikariri neno hili kwa ajili ya ziada, na ameanza nalo na amemaliza nalo akiashiria kuwa hakuna awezaye kunufaisha isipokuwa Yeye Mtukufu.
Kutoka kwa Abuu Humaid Assaaidi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alimpa kazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana mmoja ya kukusanya Zaka kutoka kwa Banii Suleim, akiitwa bin Lutbia, alipokuja akampa mahesabu, akasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Si ungelikaa nyumbani kwa baba yako na mama yako, mpaka zawadi zikujie ikiwa wewe ni mkweli" Kisha akatuhutubia, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu, kisha akasema: "Ama baada ya hayo, hakika mimi ninampa kazi mtu miongoni mwenu miongoni mwa kazi alizonikabidhi Mwenyezi Mungu, kisha baadaye anakuja anasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi yangu niliyopewa, kwa nini asingelikaa nyumbani kwa baba yake na mama yake mpaka zawadi yake imfuate, Wallah hatochukua chochote yeyote miongoni mwenu pasina haki yake, isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa amekibeba alichochukua siku ya Kiyama, na namuapa Mwenyezi Mungu nitakuja kumtambua mmoja wenu aliyekutana na Mwenyezi Mungu akiwa kabeba Ngamia akitoa mlio, au Ng'ombe akitoa mroromo, au Mbuzi akitoa mlio" Kisha akanyanyua mkono wake mpaka ukaonekana weupe wa kwapa lake, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu, je, nimefikisha" Limeona jicho langu na limesikia sikio lango.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlimpa kazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana mmoja akiitwa: Bin Lutbia ya kukusanya Zaka kutoka katika kabila la Bani Suleim, aliporejea Madina akampa mahesabu ya mali aliyokusanya na aliyotumia, akasema bin Lutbia: Hii ndio mali yenu niliyoikusanya kutoka katika Zaka, na mali hii nimepewa zawadi mimi. Akasema rehema na amani ziwe juu yake kumwambia: Hivi si ungelikaa nyumbani kwa baba yako na mama yako ili uone je utapewa zawadi ikiwa wewe ni mkweli; kwani hakika haki ulizozifanyia kazi ndio sababu ya kupewa kwako zawadi, na kwamba lau ungekaa nyumbani kwako usingezawadiwa chochote, hupaswi kuihalalisha kwakuwa tu imekufikia kwa njia ya zawadi. Kisha akapanda Mimbari rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya kuhutubia huku akiwa na hasira, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu, kisha akasema: Ama baada ya hayo, hakika mimi ninampa kazi mtu miongoni kama mfanya kazi na muajiriwa katika kile ambacho Mwenyezi Mungu kanipa maamuzi ndani yake miongoni mwa Zaka na Ngawira, kisha anakuja kutoka katika kazi yake na anasema: Hii ni yenu na hii ni zawadi yangu nimezawadiwa! Kwa nini asikae nyumbani kwa baba yake na mama yake ili zawadi yake imfuate, Wallah, namuapa Mwenyezi Mungu, hatochukua yeyote chochote katika vile anavyopewa isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kakibeba siku ya Kiyama juu ya shingo yake, ikiwa alichokichukua ni Ngamia mwenye sauti, au Ng'ombe mwenye sauti ya mroromo, au mbuzi mwenye mlio, basi atapiga kelele. Kisha akanyanyua mikono yake kwa kasi mpaka waliokaa wakaona weupe wa kwapa lake, kisha akasema: Shuhudieni kuwa nimefikisha hukumu ya Mwenyezi Mungu kwenu. Kisha Abuu Humaidi Assaaidi akaeleza radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Kuwa haya ni miongoni mwa mambo ambayo macho yake yaliyashuhudia na masikio yake yakayasikia.
Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwapige vijakazi wa Mwenyezi Mungu" Akaja Omari kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hivi sasa wanawake wamepata ujasiri kwa waume zao, basi akaruhusu kuwapiga, baada ya muda wakaanza kuzunguka katika familia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika wamekuja katika familia za Muhammad wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, (wanaume) hao si bora kati yenu".
Imepokelewa na Abu Daud na Ibn MajahAlikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga wanawake, akaja kiongozi wa Waumini Omari bin Khattwabi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wanawake wamepata ujasiri kwa waume zao, na wamekuwa na tabia mbovu. Akaruhusu rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga kipigo kisichojeruhi inapopatikana sababu ya hilo, kama kukataa kwao kutimiza wajibu wao kwa waume zao na kuwaasi, na mfano wa hayo. Baada ya hapo wakaja wanawake kwa wake wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakishitakia kupigwa na waume zao kipigo chenye kujeruhi, na matumizi mabaya ya ruhusa hii, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Wanaume hao, wanaowapiga wake zao kipigo chenye kujeruhi, si watu bora kwenu.
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakuna haki yoyote ya mtu muislamu anayotakiwa kuitolea usia, isipokuwa ahakikishae halali siku tatu, isipokuwa usia wake uwe umeandikwa kwake", akasema Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: "Haukuwahi kupita usiku mmoja tangu nilipomsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akilisema hilo isipokuwa usia wangu nilikuwa nao".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa haitakiwi kwa muislamu anapokuwa na kitu cha kutolea usia katika haki au mali hata kama ni ndogo, alale siku tatu, isipokuwa ahakikishe usia wake umeandikwa kwake. Akasema Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Sikuwahi kulala hata usiku mmoja tangu nilipomsikia rehema na amani ziwe juu yake akilisema hilo isipokuwa nilikuwa nikikaa na usia wangu.
Imepokelewa kutoka kwa Ummu Atwiya -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Asiache mapambo na kupendeza mwanamke yeyote kwa maiti zaidi ya siku tatu, isipokuwa kwa mume wake atakaa miezi minne na siku kumi, na wala asivae nguo yenye urembo isipokuwa nguo yenye urembo kiasi, wala asipake wanja, wala asiguse manukato, isipokuwa atakapotwaharika anaweza kuchukua kiasi kidogo cha Qustwi au Adhfar (aina ya marashi ya kufukiza, hutumiwa na wanawake)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliwakataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanawake kuacha mapambo kwa kuacha urembo kama marashi au wanja na mapambo mengine na nguo nzuri kwa ajili ya maiti, sawa sawa awe baba au kaka au mtoto au wengineo, zaidi ya siku tatu, isipokuwa kwa atakuwa mume ni miezi minne na siku kumi, na hatovaa katika kuacha mapambo kwa ajili ya mumewe nguo zote zelizo na urembo isipokuwa nguo yenye urembo kiasi, nayo ni nguo iliyokuwa ikitengenezwa Yemen wakati huo, hutiwa urembo kabla ya kushonwa, na wala hatopaka wanja machoni kwa ajili ya urembo wa macho, wala hatojipaka kwa harufu za marashi na nyinginezo, isipokuwa kama akioga kutokana na hedhi yake kwa kutumia kipande kidogo cha Qustwi au Adhfar, nazo ni aina mbiili maarufu za udi (anaweza kutumia udi mwingine pia) ambao lengo lake si kujipamba, umeruhusiwa kwa mwenye kuoga kutokana na hedhi, kwa ajili ya kuondoa harufu mbaya, ambayo hufuatana na athari ya damu katika tupu na si kwa ajili kujitia manukato.
Kutoka kwa Abdallah bin Yazidi Al-Khatmiy amesema: Alinisimulia Al-Baraa naye si mtu wa kukadhibishwa, akasema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema: Sami'allaahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi) alikuwa hanyanyui yeyote miongoni mwetu mgongo wake mpaka aporomoke Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kusujudu, kisha nasi tunaporomoka baada yake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Baraa bin Azibi radhi za Allah ziwe juu yake naye ni mkweli, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu anasema: Sami'allahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi), walikuwa wakiendelea kusimama walioko nyuma yake, na hainamishi yeyote miongoni mwao mgongo wake kwa ajili ya kusujudu mpaka aweke rehema na amani ziwe juu yake paji lake la uso katika Ardhi, kisha wanaporomoka wote kwa kusujudu baada yake.
Kutoka kwa Aswadi bin Yadizi amesema: Nilimuuliza Aisha, nini alikuwa akifanya Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyumbani kwake? Akasema: Alikuwa akishiriki katika kazi za familia yake (anakusudia kuhudumia familia yake), unapofika wakati wa swala anatoka kwenda katika swala.
Imepokelewa na Al-BukhaariyAliulizwa mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuhusu hali ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyumbani kwake, na alikuwa akifanya nini? Akasema: Alikuwa ni mtu kama watu wengine, na anafanya wanayofanya wanaume katika majumba yao, anashughulika na kujihudumia yeye na familia yake; anakamua mbuzi wake mwenyewe, na anashona nguo yake, na anashona kiatu chake, na anatengeneza ndoo yake, na ulikuwa unapofikia wakati wa kusimamishwa swala anatoka kwa ajili yakusali rehema na amani ziwe juu yake bila kuchelewa.