





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia mwanamke mmoja miongoni mwa Ansari (Watu wa Madina) ambaye bin Abbas alimtaja kwa jina, lakini mimi nimelisahau jina lake: “Ni nini kilikuzuia kuhiji pamoja nasi?” Akasema: Sisi tulikuwa na vilemba viwili tu, basi baba wa mwanawe na mwanawe walihiji kwa kilemba hicho na akatuachia kilemba kimoja ili tukifue.” Akasema: «Basi itakapokuja Ramadhani, basi fanya Umra, kwani Umra ndani ya Ramadhani ni sawa na Hija.”
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMtume, rehema na amani ziwe juu yake, aliporejea kutoka katika Hija ya kuaga, alimwambia mwanamke mmoja wa Ansari ambaye hakuhiji: Ni nini kilikuzuia kuhiji pamoja nasi? Akatoa udhuru kwa sababu walikuwa na ngamia wawili, hivyo mume wake na mwanawe walihiji kwa mmoja wao, na kumwacha mwingine akichota maji kisimani. Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, akamwambia kuwa kufanya Umra katika mwezi wa Ramadhani ni sawa na malipo ya Hija.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa."
Imepokelewa na Al-BukhaariyMaswahaba Mwenyezi Mungu awawie radhi, waliona Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kupigana na maadui kuwa ni matendo bora, Basi Aisha Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akamuuliza Mtume Rehema na Amani zimshukie, je nao wapigane Jihadi? Basi rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akawaelekeza kwenye Jihadi bora zaidi kwao, ambayo ni Hija iliyokubalika kwa mujibu wa Qur’ani na Sunna, isiyo na dhambi na unafiki (Riyaa).
Kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Pindi atakapaowakusanya Mwenyezi Mungu wa mwanzo na wa mwisho siku ya Kiyama itanyanyuliwa bendera kwa kila haini, patasemwa: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama atakapowakusanya wa mwanzo na wa mwisho kwa ajili ya hesabu, atasimika kwa kila haini ambaye hakutimiza ahadi aliyokubaliana nayo kwa Mwenyezi Mungu au pamoja na watu, alama ambayo atamfedhehesha kwayo mbele za watu kwa sababu ya hiana yake, na kutanadiwa juu yake siku hiyo: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani; kwa ajili ya kutangaza ubaya wa kitendo chake mbele ya waliokusanyika katika uwanja halaiki (mahashari).
Kutoka kwa Baraa bin Azib radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alituamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo saba, na akatukataza mambo saba: Alituamrisha kumtembelea mgonjwa, na kusindikiza jeneza, na kumuombea mwenye kupiga chafya, na kukiepusha kiapo au kumuepusha (na tuhuma) aliyeapa, na kumnusuru aliyedhulumiwa, na kuitika wito wa mwenye kualika (au kuita), na kutoa salamu, na akatukataza kuvaa pete za dhahabu, na kunywa katika vyombo vya madini ya fedha, na kukalia matandiko ya hariri, na kuvaa kassi (nguo iliyotengenezwa kwa katani na hariri) na kuvaa hariri nyepesi na hariri nzito na dibaji.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliwaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake waislamu mambo saba na akawakataza mambo saba; yale aliyowaamrisha ni: La kwanza: Kumtembelea mgonjwa. La pili: Kusindikiza jeneza na kushiriki katika kumswalia na kumzika, na kumuombea dua. La tatu: Kumuombea dua aliyepiga chafya na akamhimidi Mwenyezi Mungu, kwa kumuambia: Yar-hamukallaah (Akuhurumie Mwenyezi Mungu). La nne: Kumuepusha aliyetoa kiapo na kumuamini, yaani ikiwa litaapiwa jambo hali yakuwa unauwezo wa kumuepusha na tuhuma basi fanya hivyo; ili usimpelekee kulipa kafara kwa kiapo chake. La tano: Kumsaidia aliyedhulumiwa, kwa kumtetea na kuyazuia yanayotokea kwake miongoni mwa dhulma, kwa kadiri ya uwezo. La sita: Kumuitikia mwenye kualika katika walima wa chakula, kama walima wa harusi, au akika, au kinginecho. La saba: Kutangaza utoaji wa salamu na kuuneza na kujibu pia. Na aliyoyakataza ni: La kwanza: Kuvaa pete za dhahabu na kujipamba nazo. La pili: Kunywa kwa kutumia vyombo vya fedha. La tatu: Kukaa katika matandiko, nayo ni magodoro ambayo huwekwa juu ya mgongo wa farasi, na juu ya ngamia, yaliyotengenezwa kwa hariri. La nne: Kuvaa nguo iliyotengenezwa kwa katani ikachanganywa na hariri, na huitwa (Qassi). La tano: Kuvaa hariri. La sita: Kuvaa hariri nzito. La saba: Kuvaa dibaji, nayo ni: Aina bora zaidi ya hariri na ghali zaidi.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliingia Hindu binti Utba mke wa Abuu Sufiani kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika Abuu Sufiani ni mwanaume bahili sana, hanipi matumizi yanayonitosha mimi na wanangu isipokuwa kiasi ninachokichukua katika mali yake pasina yeye kujua, je kwa hilo nina tatizo? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Chukua katika mali yake kwa wema, kiasi kinachokutosha wewe na wanao".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlitaka kujua Hindu binti Utba radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mume wake Abuu Sufiani radhi za Allah ziwe juu yake, na kwamba yeye ni mwanaume bahili mwenye pupa sana na mali yake, hampi katika matumizi kiasi kinachomtosha yeye na wanaye, mpaka achukue katika mali yake kwa siri hali yakuwa hajui, je ana dhambi juu yake katika hilo?. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Chukua kwa ajili yako na watoto wako katika mali yake kiasi kinachojulikana katika mazingira ya kawaida na kwamba hicho ndicho kitakachomtosheleza hata asipojua.
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na sehemu ya mjeledi wa mmoja wenu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na kutoka asubuhi kwa mja katika njia ya Mwenyezi Mungu au kutoka mchana ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kubakia katika eneo ambalo liko kati ya waislamu na makafiri kwa ajili ya kuwalinda dhidi yao kwa siku moja, kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na kwamba mahali pa kuweka mjeledi unaotumika kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na kwamba malipo na thawabu za kutembea katika wakati wa mwanzo wa mchana mpaka mwanzo wa wakati wa adhuhuri, au mchana: Ni kwanzia adhuhuri mpaka usiku katika njia ya Mwenyezi Mungu mara moja, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alichinja Mtume rehema na amani ziwe juu yake kondoo wawili wazuri weupe wenye pembe, aliwachinja kwa mkono wake, akasema, Bismillahi Allaahu Akbar, na akaweka mguu wake ubavuni mwao.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Anasi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alichinja kwa mkono wake siku ya Idil Adh-haa kondoo wawili madume wenye mapembe, weupe wenye mchanganyiko na weusi, na akasema: Bismillaahi wallaahu Akbaru, na akaweka mguu wake katika shingo zao.
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Yeyote atakayetoa kiapo hali yakuwa ni muongo, ili ajikatie mali ya mtu Muislamu, basi atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia". Akasema: Akasema Al-Ash'athi: Kwangu mimi Wallahi kulitokea tukio hilo; kulikuwa na Ardhi baina yangu na bwana mmoja Yahudi, akanipinga kuwa si yangu, nikampeleka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuniambia: "Je una ushahidi?" Nikasema: Hapana: Akasema kumwambia Yahudi: "Toa kiapo". Anasema: Nikasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, sasa si ataapa na atachukua mali yangu!. Akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wale wanaouza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao kwa thamani ndogo..." mpaka mwisho wa aya.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmetahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoa kiapo kwa Mwenyezi Mungu huku muapaji akijua kuwa anaapia uongo ndani yake, ili ajipatie kwa kiapo hiki mali ya mwenzake; huyu atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia, akaeleza Ash'athi bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilisema hilo wakati ambao kulikuwa na mzozo kati yake yeye na bwana mmoja Yahudi katika umiliki wa Ardhi, wakashitakiana kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema kumwambia Ash'athi: Unatakiwa kuleta ushahidi ili kuthibitisha madai yako, ukishindwa kuuleta basi hutokuwa na haki zaidi ya kiapo cha hasimu wako mshitakiwa, Ash'athi akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, basi huyu bwana Yahudi si ataapa pasina hofu na mali yangu itapotea, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu kusadikisha hilo ndani ya Qur'ani kauli yake Mtukufu: "Hakika wale wanaouza" na wanabadilisha "ahadi ya Mwenyezi Mungu", na usia wake kwa waumini kwa kutimiza amana "na viapo vyao" na viapo vyao kwa jina lake kwa uongo "kwa thamani ndogo" kwa starehe za dunia "Hao hawana fungu lolote kwao Akhera" wala sehemu "Wala hatowasemesha Mwenyezi Mungu", kwa maneno yanayowafurahisha na kuwanufaisha, bali atawaghadhibikia, "wala hatowatazama siku ya Kiyama", mtazamo wa huruma na wema, "wala hatowatakasa" kwa kuwasifia kwa mazuri, wala hatowasafisha kwa kuwapa msamaha wa madhambi na machafu "na watakuwa na adhabu chungu" yenye kuumiza kwa sababu ya yale waliyoyafanya.
Kutoka kwa Raafi bin Khadiji radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake maeneo ya Dhul-Hulaifa, watu wakapatwa na njaa, wakapata ngamia na mbuzi, akasema: Na Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa mwisho wa watu wote, wakaharakisha, wakachinja, na wakabandika vyungu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaamrisha vyungu vikamiminwa, kisha akagawa na akalinganisha mbuzi kumi sawa na ngamia mmoja, ngamia mmoja akatoroka, wakamtafuta, akawashinda, na hawakuweza kumpata, na walikuwa na farasi wachache, mtu mmoja akarusha mshale, Mwenyezi Mungu akauzuia, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika wanyama hawa wafugwao ni wanyama kama walivyo wanyama pori, watakaokushindeni miongoni mwao (kuwachinja) basi fanyeni hivyo", Raafi akasema: Sisi tunawahofia maadui kesho, na hatuna visu, je tuchinje kwa miti mikavu iliyochongwa? Akasema: "Mnyama yoyote atakayemwagwa damu, na akatajiwa jina la Mwenyezi Mungu basi kuleni, isipokuwa jino na kwato, na nitakuelezeni kuhusu hilo: Ama jino ninamaanisha mfupa, na ama kwato ni visu vya wahabeshi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza Raafi bin Khadiji radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba wao walikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake eneo la Dhul-Hulaifa, watu wakapatwa na njaa, na walikuwa wamepata ngawira kutoka kwa washirikina, ngamia pamoja na mbuzi, wakafanya haraka kabla ngawira hazijagawanywa wakazichinja, na wakabandika vyungu jikoni, pasina ya kumuomba idhini Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitembea mwishoni mwa watu, alipojua hilo Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliamrisha vyungu vikamiminwa pamoja na mchuzi wake, kisha akawagawia ngawira baina yao, akafanya mbuzi kumi ni sawa na ngamia mmoja, ngamia mmoja katika hao akakimbia, wakashindwa kumkamata wala kumpata, na farasi walikuwa wachache, bwana mmoja akampiga yule ngamia kwa mshale, Mwenyezi Mungu akawazuilia, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika wanyama hawa wafugwao wana tabia kama tabia za wanyama pori, watakapokushindeni miongoni mwao na hamkuweza kuwakamata basi fanyeni hivyo. Akasema Raafi: Hakika sisi tunataraji kukutana na maadui zetu kesho na tunahofia kuharibu makali ya silaha zetu ikiwa tutazichinjia, na tunahaja kubwa ya kuchinja, na hatuna kisu, je tuchinje kwa miti ya mwanzi mikavu? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Kitakachomwaga damu na kikaitiririsha na kikaimwaga kwa wingi, na likatajwa jina la Mwenyezi Mungu, basi kuleni, isipokuwa jino na kwato, na nitakuhadithieni kuhusu hilo: Ama jino ni mfupa, na ama kwato hizo makafiri wa Ethiopia huzitumia.