





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiingia chooni, ninambebea mimi pamoja na kijana wa rika langu, chombo chenye maji na mkongojo, basi anastanji kwa maji.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba alikuwa yeye pamoja na mtumishi mwenye kukaribiana naye katika umri wake, wakimfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi anapotoka kwenda kikidhi haja yake, walikuwa wakibeba fimbo yenye meno (mkongojo) mfano wa meno ya mshale ili aifanye kuwa sitara ya kutundukia kitu chenye kusitiri, au sitara kwa ajili ya swala yake, na walikuwa wakibeba pia chombo kidogo cha ngozi kilichojaa maji , anapomaliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukidhi haja yake, basi mmoja wao anampa chombo, basi anastanji kwa maji.
Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akafika katika jalala la watu fulani akakidhi haja ndogo akiwa kasimama, nikasimama kando naye, alipomaliza akasema: “Sogea karibu” nikasogea mpaka nikasimama karibu naye, akatawadha, kisha akapangusa juu ya soksi (Khufu) zake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeImepokelewa kutoka kwa Hudhaifa bin Al-Yaman kwamba alikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akataka kukidhi haja ndogo, akaingia dampo la watu fulani; Napo ni mahali ambapo takataka na uchafu unaofagiliwa kutoka majumbani hutupwa hapo, hivyo akakidhi haja ndogo akiwa kasimama, na huwa anakidhi haja ndogo akiwa kachuchumaa. Basi Hudhaifa akajisogeza mbali naye, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Njoo karibu, basi Hudhaifa akamkaribia mpaka akasimama nyuma yake, nyuma ya miguu yake; Ili awe kama mstara kwake kutokana na watu kumtazama katika hali ile. Kisha akatawadha, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, na wakati wa kuosha miguu yake, alitosheka kwa kupangusa juu ya soksi (Khofu) zake - nazo ni zile zinazovaliwa miguuni, zilizotengenezwa kwa ngozi nyembamba na mfano wake na zinazofunika vifundo vya miguu, na wala hakuzivua.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba alikutana na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika barabara miongoni mwa barabara za mji wa Madina huku akiwa na janaba, akamkwepa na akaenda kuoga, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamtafuta hakumpata, alipomjia akasema: "Ulikuwa wapi ewe Abuu Huraira?" Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ulikutana nami, nami nikiwa na janaba, sikufurahishwa kukaa na wewe mpaka nioge, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, hakika muumini hanajisiki".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAlikutana Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika baadhi ya njia za Madina, na Abuu Huraira alikuwa na janaba, na kwa sababu ya kumuheshimu kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake alichukia kukaa naye na kuzungumza naye hali yakuwa yuko katika hali ile, kwa kudhani kwake kuwa yeye ni najisi, akaenda kwa uficho na akaoga, kisha akarejea na akakaa, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuuliza kuwa alikwenda wapi? Akamueleza kuhusu hali yake, na kwamba yeye alichukia kukaa naye hali yakuwa yeye ni najisi kwa sababu ya janaba, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akastaajabu, na akasema: Hakika muumini ni msafi na wala hanajisiki kwa hali yoyote; akiwa hai na hata wakiwa maiti.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Fanyeni haraka kulipeleka jeneza, likiwa ni la mtu mwema, basi mnaliwahisha kupata kheri, na likiwa kinyume na hivyo, basi hiyo nishari mnajiwekea shingoni kwenu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwenda mbio kuliandaa jeneza na kuliswalia na kuzika; jeneza likiwa jema basi mnaliwahisha kwenda katika kheri miongoni mwa neema za kaburi, na likiwa kinyuume na hivyo, basi hiyo ni shari mnaiweka katika shingo zenu.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba mtu mmoja aliingia msikitini siku ya Ijumaa kupitia mlango uliokuwa upande wa Dar Al-Kadhaa, na huku Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesimama akihutubu, akamuelekea Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa wima, kisha akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeteketea na njia zote zimekatika, muombe Mwenyezi Mungu atuletee mvua, akanyanyua Mtume rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: "Ewe Mola wetu tunyeshelezee, Ewe Mola wetu tunyeshelezee, Ewe Mola wetu tunyeshelezee". Akasema Anasi: Namuapa Mwenyezi Mungu, hatukua tukiona mbinguni mawingu wala dalili, na kati yetu na Mlima Sal'i hapakuwa na nyumba wala makazi, anasema: Likachomoza wingu nyuma yake mithili ya ngao, lilipofika kati kati ya mawingu likatanda kote, kisha mvua ikaanza kunyesha, namuapa Mwenyezi Mungu hutukuliona Jua kwa muda wa siku , kisha akaingia bwana mmoja kupitia mlango ule ule siku ya Ijumaa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa wima akihutubia, akamuelekea akiwa kasimama akasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeangamia, na njia zimekatika, muombe Mwenyezi Mungu aizuie kwetu mvua, anasema akanyanyua Mtume rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu inyeshe pembezoni mwetu na si juu yetu, ewe Mwenyezi Mungu inyeshe katika vichuguu na milima na ndani ya mabonde, na katika maoteo ya miti" Anasema: Mvua ikakata, na tukatoka tukitembea juani, amesema Shariki: Nilimuuliza Anasi, je ni yule yule mtu wa kwanza? Akasema: "Sijui".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAliingia bedui mmoja msikiti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Ijumaa kupitia mlango wa Magharibi upande wa nyumba ya Omari bin Khattwab radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa kasimama anahutubia, yule bwana akamuelekea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akasema, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wanyama wameangamia, na njia zote zimekatika kwa kufa mifugo inayobeba watu, au imedhoofika kutokana na njaa, basi muombe Mwenyezi Mungu atunyeshelezee mvua. Akanyanyua rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu tunyeshelezee, Ewe Mwenyezi Mungu tunyeshelezee, Ewe Mwenyezi Mungu tunyeshelezee. Amesema Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake: Wallahi hatukua tukiona mbinguni hata kipande cha mawingu, na hapakuwa kati yetu sisi msikitini na Mlima Sal'i ulioko Magharibi mwa msikiti upande ambao hujia mawingu nyumba wala makazi yanayoweza kutuzuia kuona mawingu. Amesema Anasi radhi za Allah ziwe juu yake: Likatokeza nyuma yake wingu la duara mfano wa ngao nayo ni mviringo mdogo, lilipofika kati kati ya mawingu ya Madina likatanda, kisha mvua ikaanza kunyesha, na namuapa Mwenyezi Mungu, hatukuliona Jua tena kutokana na mvua mpaka Ijumaa iliyofuata, kiasi kwamba aliingia tena yule bwana kupitia mlango ule ule, huku rehema na amani ziwe juu yake akiwa kasimama anahutubia, akamuelekea akiwa wima, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeangamia na njia zimekatika, basi muombe Mwenyezi Mungu aizuie mvua kwetu. Akasema: Akanyanyua rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu igeuze mvua iende pembezoni mwetu ewe Mwenyezi Mungu ielekee katika sehemu zenye miinuko katika Ardhi kama kichuguu, na milima midogo, na ndani ya mabonde, na maoteo ya miti. Akasema Anasi: Yakakatika mawingu ya mvua, na tukatoka tukitembea juani.
Kutoka kwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Tulikatazwa kusindikiza jeneza, na hatukusisitiziwa katazo hilo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnaeleza Ummu Atwiya Muanswari (mzaliwa wa Madina) radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwakataza wanawake kusindikiza jeneza; na hii ni kwa sababu ya mitihani inayohofiwa juu yao, na uchache wa subira yao, kisha akaeleza radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakutilia mkazo katika katazo hili kama anavyofanya katika matakazo mengine.
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alimsimulia akasema: Alinijia mwanamke mmoja akiwa na watoto wake wawili akiniomba, nikawa sikupata ndani kwangu zaidi ya tende moja, nikampatia, akaigawanya baina ya watoto wake, kisha akanyanyuka akatoka, muda si mrefu, akaingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamsimulia kisa hicho, akasema: "Atakayesimamia chochote kwa watoto wa kike hawa, akawatendea wema, basi watakuwa ni kinga kwake kutokana na moto".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake, ya kwamba mwanamke mmoja alimjia akiwa na mabinti zake wawili akimuomba chochote kinacholiwa, Aisha akawa hakupata kwake zaidi ya tende moja, akampatia basi mwanamke yule akaigawanya tende hiyo baina ya watoto wake, na yeye hakula chochote, kisha akanyanyuka na akaondoka, punde akaingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, Aisha akamsimulia kisa hicho, akasema: Atakayesimamia chochote katika malezi ya mabinti hawa, akawatendea wema na akawalisha na akawanywesha na akawavisha, na akawa na subira juu ya hilo, basi watakuwa ni sitara na kinga kwake dhidi ya moto.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa na mkazo mkubwa na kudumu na jambo kama alivyokuwa katika rakaa mbili za Alfajiri.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAmeeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwa na mkazo mkubwa katika swala za sunna zaidi ya jinsi alivyozikazia na kuzipupia na kuzihifadhi rakaa mbili za sunna ya kabla ya Alfajiri.
Kutoka kwa Muadha amesema: Nilimuuliza Aisha nikasema: Vipi kuhusu mwenye hedhi analipa swala na wala halipi swala? Akasema: Hivi wewe ni mtu kutoka Haruuraa? (mji walikozusha fitina baina ya waislamu) Akasema: Hapana: Mimi si mtu kutoka Haruuraa, bali mimi ninauliza tu, akasema: Tulikuwa tukipatwa na hilo, tunaamrishwa kulipa swaumu, na wala hatuamrishwi kulipa swala.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeMuadhi alimuuliza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Kwa nini mwenye hedhi analipa swaumu na wala halipi swala?. Akasema kumwambia: Hivi wewe ni katika Makhawariji (wanaotoka katika utiifu wa kiongozi wao) wa mji wa Haruuraa wanaokithirisha maswali kwa kutaka ugumu na kutia mkazo katika dini? Akasema: Mimi si mtu kutoka Haruuraa, bali mimi ninauliza tu, akasema: Tulikuwa tukipatwa na hedhi tukiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi tunaamrishwa kulipa swaumu, na wala hatuamrishiwi kulipa swala.