





























Hadeeth Cards
Da'wa cards that highlight great meanings from the noble prophetic hadiths in a simple style and attractive display that helps the Muslim to have a deeper understanding of his religion in an easy way
All
Imepokelewa Kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fikisheni kutoka kwangu japokuwa aya moja, na simulieni kuhusu wana wa Israeli wala hakuna ubaya, na yeyote atakayenisemea uongo mimi kwa makusudi basi na ajiandae, makazi yake ni motoni".
Imepokelewa na Al-BukhaariyAnaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuifikisha elimu kutoka kwake katika Qur'ani na mafundisho yake (Sunna), hata kama kitu kitakuwa kidogo kama aya moja toka ndani ya Qur'ani au hadithi, kwa sharti mfikishaji awe mjuzi katika kile anachokifikisha na kuwalingania watu kwacho. Kisha akaweka wazi -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna ubaya kusimulia kuhusu wana wa Israeli kwa yale yaliyotokea kwao katika matukio, yale yasiyokinzana na sheria yetu. Kisha akatahadharisha kumzulia uongo, nakuwa yeyote mwenye kumzulia uongo kwa makusudi basi ajiandalie mwenyewe makazi yake motoni.
Imepokelewa kutoka kwa Mikdad Bin Maadi Karbi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kwa hakika imefikia wakati ambao mtu atafikiwa na hadithi yangu akiwa amekaa kwenye tandiko lake na akisema: Hakika kitakachotuhukumu kati yetu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu hivyo tukikuta halali ndani yake tutaihalalisha na tukikuta ndani yake kuna haramu tutaiharamisha, na kwa hakika chochote alichokiharamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na amani ziwe juu yake ni kama alichokiharamisha Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ibn MajahAmefahamisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake kuwa umefika wakati kutakuwa na kundi la watu, mmoja wao atakuwa amekaa na kuegemea katika tandiko lake, inamfikia hadithi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kusema: Kitakachotuamua kati yetu na nyie kwenye mambo yetu ni Qur'ani tukufu pekee ndiyo inatutosha, tukikuta ndani yake halali tunaifanyia kazi, na tukikuta ndani yake haramu tunajiepusha nayo. kisha akaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila kitu alichokiharamisha au kukikataza katika sunna zake basi mambo hayo hukumu yake ni kama alivyoharamisha Mwenyezi Mungu katika kitabu chake; kwa kuwa yeye ni mfikishaji kwa niaba ya Mwenyezi Mungu.
Na kutoka kwa Irbadhi bin Sariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja alisimama kwetu sisi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akatupa mawaidha makali mno, nyoyo zilisisimka kwayo, na macho yalibugujikwa machozi, pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Umetuwaidhi mawaidha ya mwenye kuaga, tuachie usia. Akasema: " Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, na usikivu na utii, hata kama (mzungumzaji) atakuwa mtumwa tena muhabeshi (Muethiopia), na mtakuja kuona baada yangu hitilafu nyingi, basi shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za makhalifa (watawala) waongofu, zing'ateni (mzikamatilie) kwa magego, na tahadharini sana na mambo ya kuzushwa, kwani kila uzushi ni upotevu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadMtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwapa mawaidha Masahaba, mawaidha makali, nyoyo ziliogopa kwa mawaidha hayo, na macho yalibugujikwa machozi, Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kana kwamba mawaidha haya ni ya mwenye kuaga, kwa sababu waliona ni jinsi gani alivyokuwa na umakini mkubwa katika mawaidha, wakaomba usia, ili washikamane nao baada yake, akasema: Nakuusieni kumcha Allah Mtukufu, nako ni kwa kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho. Na usikivu na utii, yaani: Kwa wenye mamlaka juu yenu, hata kama kiongozi wenu au aliyekutawaleni ni mtumwa, yaani mtu dhalili akawa kiongozi juu yenu, msilibeze hilo, na mtiini, kwa kuchelea kuamsha fitina, bila shaka atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona hitilafu nyingi, Kisha akawabainishia njia ya kutoka katika hitilafu hii, nayo ni kwa kushikamana na sunna yake na sunna za mahalifa wanne waongofu baada yake, Abuubakari Swiddiq, na Omari bin Khattwab, na Othman bin Affan, na Ally bin Abii Twalib, radhi za Allah ziwe juu yao wote, na kuzing'ata kwa magego, yaani meno ya mwisho: Anakusudia kwa kauli hii yaani kufanya bidii katika kubaki katika sunna na kushikamana nazo, Na akawatahadharisha na mambo ya kuzushwa yaliyobuniwa ndani ya Dini, kwani kila uzushi ni upotevu.
Kutoka kwa Samura bin Jundab na Mughira bin Shu'ba radhi za Allah ziwe juu yao, wamesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesimulia kutoka kwangu mazungumzo ambayo yanaonekana kuwa ni uongo basi huyo ni mmoja kati ya waongo"
Imepokelewa na Imamu Muslim katika Utangulizi wakeAnaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayenukuu Hadithi kutoka kwake hali yakuwa anajua au anadhani au dhana yake kubwa kuwa ni kumzulia uongo rehema na amani ziwe juu yake; basi mpokezi atashirikiniana na mwanzilishi wa uongo huu katika dhambi.
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayenisingizia mimi uongo kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake kuwa ni motoni".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeAnabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayemsemea uongo kwa makusudi kwa kumnasibishia kauli au kitendo kwa uongo, basi atambue kuwa Akhera atakua na makazi motoni; ndio malipo yake kwa kumsingizia kwake uongo.
Kutoka kwa Abuu Huraira kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kutakuwa mwisho wa umma wangu na watu, wakikuhadithieni mambo ambayo humkuwahi kuyasikia nyinyi wala baba zenu, ole wenu na ole wao".
Imepokelewa Imamu MuslimAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa watatokea watu katika zama za mwisho katika umma wake wakizua uongo, na wakisema mambo ambayo hakuyasema yeyote kabla yao, wataeleza simulizi za uongo na za kutunga, akatuamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake- tujiweke mbali nao na wala tusikae nao, na wala tusisikilize mazungumzo yao; ili hadithi hizo za kutunga tusiziweke ndani ya nafsi, tukashindwa kujiepusha nazo.
Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kukihifadhi, Makuraishi wakanikataza, na wakasema: Hivi unaandika kila kitu unachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwanadamu huzungumza wakati wa hasira na furaha? Nikaacha kuandika, nikamueleza hilo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akaashiria kwa kidole chake katika kinywa chake, akasema: "Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakitoki ndani yake ila haki".
Imepokelewa na Abu DaudAmesema Abdallah bin Amri radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ili nikihifadhi kwa kukiandika, mabwana wa kikuraishi wakanikataza, na wakasema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwanadamu anazungumza katika furaha na hasira, na huenda akakosea, nikaacha kuandika. Nikamueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- waliyosema, akaashiria kwa kidole chake kinywani kwake akasema: Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake haitoki ndani yake ila haki kwa hali zote, na katika furaha na hasira. Na alisema Mtukufu kumuhusu Nabii wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Na hatamki kwa matamanio * Si vinginevyo, ila huo ni wahyi anaofunuliwa" [An najm: 3-4].
Kutoka kwa Abuu Abdirahman Abdallah bin Omari bin Khattwab radhi za Mweneyzi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Umejengwa uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mja wake na Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba tukufu, na kufunga ramadhani".
Imepokelewa na Bukhari na MuslimAmeufananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Uislamu na jengo madhubuti kwa nguzo zake tano zenye kulibeba jengo hilo, na mambo mengine ya Uislamu kama nyenzo zenye kulikamilisha jengo hilo, Na nguzo ya kwanza katika nguzo hizo ni: Shahada mbili; Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hizo mbili ni nguzo moja; kila moja haitengani na nyingine, mja anazitamka kwa kukiri umoja wa Mwenyezi Mungu na kustahiki kwake kuabudiwa yeye pekee pasina mwingine, na kufanyia kazi makusudio ya nguzo hii, na kwa kuamini utume wa Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kumfuata yeye. Na nguzo ya pili: Ni kusimamisha swala, nazo ni swala tano za faradhi usiku na mchana: Alfajiri, Adhuhuri, lasiri, Maghribi, na Ishaa, kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake. Na nguzo ya tatu: Ni kutoa zaka ya lazima, nayo ni ibada ya mali ya wajibu katika kila mali iliyofikia kiwango maalumu katika sheria, ambayo hupewa wastahiki wake. Na nguzo ya nne: Ni Hija, nayo nikutia nia ya kwenda Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada, kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka. Na nguzo ya tano: Ni kufunga mwezi wa Ramadhani, nako ni kujizuia na kula na kunywa na vinginevyo miongoni mwa vyenye kufunguza kwa nia ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuzama jua.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Abdirahman Abdullahi Bin Masoud radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alituhadithia Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye ndiye mkweli mwenye kusadikika: "Hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake ndani ya tumbo la mama yake siku arobaini, kisha linakuwa pande la damu kwa mfano wake, kisha linakuwa pande la nyama mfano wake (siku arobaini), kisha linatumiwa Malaika analipulizia roho, na anaamrishwa kuandika maneno manne: Kuandika riziki yake, na umri wake, na matendo yake, na kuwa ni muovu au mwema; namuapa yule ambaye hakuna Mola isipokuwa yeye hakika mmoja wenu atafanya amali za watu wa Peponi mpaka ikawa baina yake na Peponi ni dhiraa moja (futi) kikamtangulia kitabu akafanya amali za watu wa motoni akauingia, na hakika mmoja wenu atafanya amali za watu wa motoni mpaka ikawa baina yake na Moto isipokuwa dhiraa, kitabu kikamtangulia akafanya amali za watu wa Peponi na akaingia".
Imepokelewa na Bukhari na MuslimAmesema Bin Masoud: Ametuhadithia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake naye ni mkweli kwenye maneno yake, na mwenye kukubaliwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemkubali, Amesema: Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake, na jambo hilo ni kuwa mtu akimuingilia mke wake basi yale manii yake yaliyosambaa hukusanywa kwenye tumbo la mwanamke kwa muda wa siku arobaini yakiwa ni tone la manii, Kisha hubadilika na kuwa pande la damu nzito iliyoganda, haya hufanyika katika arobaini ya pili, Kisha hubadilika kuwa pande la nyama, nacho ni kipande cha nyama chenye ukubwa wa kuweza kutafunwa, na mabadiliko haya ni katika arobaini ya tatu, Kisha Mwenyezi Mungu hulitumia pande hilo la nyama Malaika, kisha hulipulizia ndani yake roho baada ya kuisha siku arobaini za tatu, Na huamrishwa Malaika aandike maneno manne, nayo ni: Riziki yake, nacho ni kiwango ambacho atakipata miongoni mwake ni neema katika umri wake, Na pia huandikwa wakati wake, nao ni muda wa kubakia kwake Duniani, Na matendo yake, yatakuwa ni yapi? Na je atakuwa muovu au mwema. Kisha akaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yawezekana mtu akafanya matendo miongoni mwa matendo ya watu wa peponi, na yakawa matendo yake ni mazuri, yaani kwenye muonekano wa watu, na akabakia hivyo mpaka inakuwa kati yake na Pepo ni kiasi cha mkono, yaani kiasi kilichobaki kati yake mpaka kuifikia pepo ni kidogo sana kama vile ambavyo mtu amebakiza nafasi kati yake na ardhi kiasi cha mkono, mara Kitabu kinamtangulia na kile alichopangiwa, na wakati huo anafanya matendo ya watu wa motoni na akaandikiwa kuwa huo ndio mwisho wake na akaingia motoni; Kwa sababu sharti la kukubaliwa matendo yake ni kudumu katika matendo hayo na wala asibadilishe, na watu wengine wapo wenye kufanya matendo ya watu wa motoni mpaka mtu anakaribia kuingia motoni, mpaka inakuwa kati yake na kuingia motoni ni kiasi cha urefu wa mkono, basi kikamtangulia kitabu na alichopangiwa hivyo akafanya matendo ya watu wa peponi na akaingia peponi.